RIO & RC (Arusha) nina mashaka na KIAPO chenu.... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

RIO & RC (Arusha) nina mashaka na KIAPO chenu....

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Meitinyiku L. Robinson, Mar 12, 2012.

 1. Meitinyiku L. Robinson

  Meitinyiku L. Robinson JF-Expert Member

  #1
  Mar 12, 2012
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwenu Namomba & Mulongo;

  Kwa watumishi wa Serikali jambo kubwa kabla ya kuanza utumishi wao ni wao kula kiapo cha Utumishi kwa nafasi ile wanayokwenda kuitumikia. Utaratibu huu unalindwa na Sheria No. 8 ya Mwaka 1962 "The Official Oaths Act" kifungu kilichonigusa zaidi ni kile cha 12 (oath of Secrecy) ambacho naamini watu kama kina Mulongo wanawajibika kwacho.

  Nilishangazwa na tamko la Mulongo (ambaye ni Mwakilishi wa Raisi na vile vile Mwenyekiti wa Ulinzi na Usalama wa Mkoa) kwamba ati yeye si muhifadhi nyaraka, naamini kwa nafasi aliyonayo yeye ndiye Muhifadhi Mkuu wa Kwanza wa Nyaraka za Serikali na sintashangazwa kesho kutwa nikisikia Raisi kadhurika akiwa katika himaya ya Mulongo kwa uzembe kama huo wa kutapakanya nyaraka za SIRI kama ambavyo hugongwa mihuri yenye neno "SIRI" na kwa tafsiri ya kawaida ni kwamba waraka huo unapaswa kusomwa ama kumfikia mlengwa tu kinyume na hapo itakuwa ni aibu si kwa mtumaji ama mtumiwaji bali kwa Serikali.

  Sasa hawa Waheshimiwa kama si wamemchoka huyo aliyewatuma kumwakilisha basi thamani ya kiapo wao hawaijui na wako tayari hata kuuza Nchi......... Aki ya Ngai Mwalimu angekuwepo sijui leo hii Namomba au Mulongo mngekuwa wapi......
   
 2. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #2
  Mar 12, 2012
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,290
  Likes Received: 598
  Trophy Points: 280
  Katika hili siwezi kumlaumu Mulongo. Kwa Bongo huo waraka wa siri kufikia kule unakohifadhiwa, umepita kwenye mikono si chini ya mitatu. Kwa njaa tulizonazo ni rahisi sana kwa sekretari aliyeuchapa au mtunza masjala ya siri kuuvujisha kwani malipo yao ni duni sana.
   
Loading...