Ridhiwani Kikwete afichuka kukandia Millya

Ridhiwani Kikwete afichuka kukandia Millya

Candid Scope

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2010
Posts
11,897
Reaction score
6,933
RidhiwanKikweteJr.jpg

Ridhiwani Kikwete


Ridhiwani amshukia Millya

Mtoto wa Rais, Dk. Jakaya Kikwete, Ridhiwani Kikwete amemshukia aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Arusha, James Ole Millya.Millya alijiengua kutoka CCM na kujiunga CCM kutokana na kile alichoeleza kuwa chama tawala kimekuwa mfano wa gari lililosheni pancha, hivyo halifai kwa safari.

Hata hivyo, baada ya Millya kuondoka CCM, taarifa zilizopatikana mkoani humo zilieleza kwamba aliondoka akiwa na takribani Shilingi milioni 2, mali ya UVCCM. Taarifa hizo ndizo zimemuibua Ridhiwani akichangia katika mtandao wa kijamii wa Tunuru la Afrika na kusema Millya asubiri utaratibu unafuata. Ridhiwani aliandika maneno hayo juzi kupitia simu yake ya mkononi na kuyatuma kwenye mtandao huo akisema, “nilidhani utani, kumbe James (Millya) tunamdai hela za Umoja wa Vijana mkoa wa Arusha.”
Aliongeza, “nawashukuru vijana makini wa mkoa wa Arusha kwa umakini wa hali ya juu. Utaratibu waja bwana Millya kama unasoma post hii.

Hata hivyo ujumbe huo wa Ridhiwani ulichangiwa na washiriki mbalimbali, wengi wao wakimpinga na kumhusisha (Ridhiwani) na familia yake kwa tuhuma zenye nia ovu. Baadhi ya tuhuma hizo zimewahi kuchapishwa na kutangazwa kwenye vyombo vya habari, zikikariri vyanzo tofauti.


Millya alitangaza kujiudhuru uwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Arusha hivi karibuni na kuhamia rasmi katika Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Aidha, siku iliyofuata viongozi wa CCM kwa nyakati tofauti walikaririwa na vyombo vya habari wakimwelezea Millya kuwa, alikuwa gamba na mzigo ndani ya chama umoja huo.

IPPMedia
 
Kwa nini huyu dogo anahaha hivyo kwa kutumia kivuli cha baba yake? Analinda ulaji wake?
 
Hivi huyu riz1.. Alishamfksha dr slaa na mtikila mahakamani.
 
Hahahahah Hako kajamaa katampata yanayompata El-sayif wa ghadafi we kaache tu
 
Du! Ingekuwa kipindi hatujamjua JK basi Millya ange geuka babu seya ila kwa sasa huyu dogo awe makini maana mdingi kanazidi kuharibu. Nchi ikikombolewa atakipata cha moto
 
Like father like son!

nasikia ole millya hana kazi wala sehemu ya kuishi inadaiwa anashinda katika club moja inaitwa via via nina clip ya viongozi wa ccm ebu nisaidieni jinsi ya kuiingiza humu maana nifanyeje ili kila mmoja aisikilize mwenyewe
 
Ni pesa gani huyu **** anasema Millya kuwaibia! ambazo zinamuuma kuliko zetu anakomba yeye na babake mnyonyaji huyu!
 
Ni pesa gani huyu **** anasema Millya kuwaibia! ambazo zinamuuma kuliko zetu anazokomba yeye na babake mnyonyaji huyu!
 



Ridhiwani amshukia Millya


Mtoto wa Rais, Dk. Jakaya Kikwete, Ridhiwani Kikwete


"
Aliongeza, "nawashukuru vijana makini wa mkoa wa Arusha kwa umakini wa hali ya juu. Utaratibu waja bwana Millya kama unasoma post hii.


IPPMedia

Nahisi sielewi, anaongea kwa wadhifa upi?
 
Ni pesa gani huyu **** anasema Millya kuwaibia! ambazo zinamuuma kuliko zetu anakomba yeye na babake mnyonyaji huyu!

CCM ilishabadilisha utaratibu wa dhamani ya mhasibu kushikiliwa na Mwenyekiti? Hii ni dalili tosha ya kuchanganyikiwa, mwenye akili timamu hawezi kukubaliana na dhana ya Mwenyekiti kukimbia na pesa wakati zinatunzwa na wahasibu.
 
Kuna mtu amewahi kuniambia wapinzani waki hukua nchi, anadhani watu watakao pata tabu zaidi ni
. Nape Nnauye
. Ridhwan Kikwete.
Ni watu wanao ishi maisha yasiyo yao, na huku kweli wakiifahamu.
 
Ridhiwani anaongea kama Mwenyekiti mwenza wa UV CCM Taifa !
 
Kuna mtu amewahi kuniambia wapinzani waki hukua nchi, anadhani watu watakao pata tabu zaidi ni
. Nape Nnauye
. Ridhwan Kikwete.
Ni watu wanao ishi maisha yasiyo yao, na huku kweli wakiifahamu.

JK na familia yake ni wezi wakubwa na wamelitesa sana taifa hili, yaani watafute mahali pa kuishi haki ya mungu! baada ya 2015 si hapa tz!
 
Mwizi huyoooo!!!!!!!!!
Ridhiwani subiri ujambazi wako ulioufanya hapa Arusha kwa kuwanyang'anya wananchi wa Arusha ardhi yao.
Siku itakapofika labda uhame hii nchi. kwa sasa tunaanza na baba yako anayewatetea wezi wa mali ya umma.
Badala ya kupiga kura ya kutokuwa na imani na Pinda kibao kinamgeukia Baba yako!
 
Last time huyu **** Riziwani nimemwona pale Palace Hotel ars usiku, kaja kuikagua hotel yao! this time ukitia maguu utatukoma pusi wewe!
 
Back
Top Bottom