Ridhiwani 'awapa' ulaji marafiki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ridhiwani 'awapa' ulaji marafiki

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, May 27, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  May 27, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [h=1][/h]

  [​IMG]
  Na Alfred Lucas - Imechapwa 16 May 2012

  [​IMG][​IMG]
  MARAFIKI sita wa Ridhiwani Kikwete, yule mtoto wa rais, wameteuliwa kuwa wakuu wa wilaya (ma-DC), MwanaHALISI limeambiwa.

  Wanaotajwa kuwa marafiki wa Ridhiwani na wameteuliwa kuwa ma-DC ni pamoja na Ulega Abdallah aliyepelekwa Kilwa, mkoani Lindi; na Paul Mzindakaya aliyepelekwa wilaya mpya ya Busega, Mwanza.


  Wengine ni Mrisho Gambo (Korogwe), Elibariki Kingu (Kisarawe), Anthony Mtaka (Mvomero) na Hassan Masala (Kilombero).


  Wachambuzi wa mambo ya siasa wanasema uteuzi huo unaweza kuwa sehemu ya mpango maalumu wa CCM kuandaa safu yake katika mbio za uchaguzi kuelekea 2015.


  Mtoa taarifa ambaye ameomba jina lake lisitajwe gazetini, alisema juzi Jumatatu, “Hapo kuna mtu mmoja tu aliyeachwa katika kundi hilo; ni Anthony Peter Mavunde.


  “Huyu hawamwelewi. Mara yuko kwa Ridhiwani, mara kambi ya Benno Malisa; na unajua Benno na Ridhiwani bado hawaelewani vizuri,” alisema mtoa habari.


  Malisa ni kaimu mwenyekiti wa UV-CCM; Ulega mwenyekiti wa umoja huo mkoa wa Pwani; Mzindakaya mwenyekiti Rukwa; Masala mwenyekiti Lindi, na Gambo, Kingu na Mtaka ni wajumbe wa Baraza Kuu la UV-CCM.


  Ulega ndiye kiongozi wa UV-CCM aliyepata kutoa tamko la mkoa kwamba “…rais ajaye wa Tanzania, hatatoka Kaskazini.”


  Wachambuzi wanaona kuteuliwa kwake kuna maana kwamba uongozi wa juu wa chama na serikali, unaunga mkono tamko hilo.


  Kwa upande wa Mzindakaya, ambaye ni mtoto wa kada maarufu wa CCM na mbunge wa zamani wa Kwela, Chrisant Mzindakaya, uteuzi wake unachukuliwa kuwa ni kuendeleza urafiki.


  Hata hivyo, kuna malalamiko kuhusu wabunge viti maalum kupewa u-DC “…wakati kuna watu waliosotea chama kwa muda mrefu na ambao wameachwa,” zimeeleza taarifa.


  Wakuu wa wilaya ambao ni wabunge wa viti maalum ni Lucy Mayenga (Uyui), Subira Mgalu (Muheza), Martha Umbulla (Kongwa), Rosemary Kirigini (Meatu) na Agnes Hokororo (Ruangwa).


  Mayenga kwao ni Shinyanga, Mgalu anatoka Pwani, Umbulla (Manyara), Kirigini (Mara) na Hokororo (Mtwara).


  Taarifa zinasema kuna orodha ndefu ya vijana ambao walitarajia kuwa ma-DC lakini hawakuteuliwa.


  Miongoni mwao ni Marwa Mathayo (Mara), Jonas Nkya (Morogoro), Fadhili Ngajiro (Iringa) na Robert Kamoga (Tabora) ambao wametajwa kutoiva na Ridhiwani.


  Wamo pia mwenyekiti wa sasa wa UV-CCM taifa, Benno Malisa, mkuu wa Wilaya ya Chemba (Dodoma) Francis Isaac; Said Sambara na Hussein Bashe aliyewahi kutuhumiwa kutokuwa raia. Hata hao wanadaiwa kutoiva na Ridhiwani.


  Mwingine aliyetajwa ni Katibu Mkuu UV-CCM, Martine Shigella ambaye mbele ya hadhara hutamba kwamba “…ndani ya UV-CCM hakuna matatizo.”


  Hata hivyo, Malisa anayekwepa kuzungumzia wimbi hilo, anasema anayepaswa hasa kufanya hivyo ni Shigella ambaye anawabeza wote waliohama CCM kuwa wamejivua gamba.


  Lakini, Ngajiro anaonya mara moja, “…kuhama kwa Millya (James ole) kusibezwe. Unajua anapoondoka mtu kama yule anahama na watu, sasa lazima watu wakae chini kufikiria namna ya kujenga chama. Kuondoka kwake ni pigo.”


  Mwenyekiti mwingine wa mkoa aliyezungumza na gazeti hili anasema, “Ridhiwani ni tatizo kaka. Kuna kukandamizana na Ridhiwani ndiye anayesababisha yote haya.”


  “Ninyi wenyewe mmeandika kwamba Millya alilalamikia ikulu kutotoa karipio la kauli ya vijana wa mkoa wa Pwani.


  “Hilo jambo lilimpa jibu Millya kwamba ikulu inahusika kwa namna moja au nyingine. Katika kikao cha Baraza la Vijana Pwani inadaiwa Ridhiwani alikuwamo.


  Taarifa ambazo gazeti hili limeambiwa ni kuwa Ridhiwani “hajaacha kuwa na makundi” hasa kwa mtu anayetofautiana naye kimawazo kuendeleza chama hicho kikongwe.


  “Vijana wanaona wananyimwa fursa ambayo sasa wanaisaka kupitia upinzani,” anasema mwenyekiti huyo na kuongeza, “Yaani ukikosana na Ridhiwani utatuhumiwa kuwa ni fisadi.”


  Naye Ridhiwani alipotafutwa kuzungumzia tuhuma hizo, simu yake iliita bila kupokelewa. Alipopelekewa ujumbe mfupi (sms), alijibu haraka akisema, “Waulize hao wenyeviti kaka.”


  Ridhiwani alikuwa ameulizwa, “Kuna tuhuma kwamba umekorofishana na wenyeviti wa UV-CCM wa mikoa ipatayo 10…tunataka utoe kauli yako.”


  Sasa hata wimbi la wanachama, hususan vijana kuihama CCM kwenda upinzani, kunadaiwa kusababishwa na kile kinachoitwa “kuvunjika kwa matumaini kwa vijana wengi.”


  Mmoja wa viongozi ambaye alihama mapema na kuhama kwake kumetikisa chama, ni aliyekuwa Mwenyekiti wa UV-CCM mkoa wa Arusha, James ole Millya aliyejiunga Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) hivi karibuni.


  Mtoa habari wa gazeti hili anasema kuwa hata kitendo cha kuenguliwa kuwania ubunge wa Afrika Mashariki mwaka huu, kwa hoja kuwa amepewa karipio na chama, kimetafsiriwa kuwa ni uonevu.


  “Kama onyo, mbona kuna mgombea alikuwa na onyo kama la Millya na akapitishwa. Iweje kwa Millya? Wamasai wanaona kuwa hawana fursa ndani ya CCM,” alisisitiza.


  “Ndiyo maana wanahama. Wanakwenda CHADEMA. Chama chenye kutoa fursa, chenye matumaini kwa vijana. Ushahidi uko wazi,” amesema.


  Millya alisema hivi karibuni kwamba CCM imefilisika kimawazo na haitoi matumaini kwa Watanzania kwa kuwa imekosa demokrasia na kupuuza maoni na mawazo ya wadau wengine.


  Alidai ya kuwa Ridhiwani hakuanza sasa kuhusika “kufinyanga mawazo ya vijana,” wengine akiwamo Hamad Yussuf Masauni ambaye alijiuzulu kwa sababu za umri wake kupita.


  Kuondoka kwa Millya kunaelezwa kuwa ni mwendelezo baada ya kuondoka kwa aliyekuwa mwenyekiti wa umoja huo, Hamad Yussuf Masauni, mbunge wa Kikwajuni, Zanzibar.


  Masauni alipoulizwa kuhusu hali katika umoja wa vijana alisema, “Hizi ni changamoto tu. Kama kuna chama ambacho hakina changamoto hilo ni tatizo. Ukiniuliza mimi kuhusu CCM naona ni chama bora kwa msingi wake, historia, sera na ilani.”


  Inadaiwa kuwa mgogoro kati ya Ridhiwani na makada wenzake ulianza mara baada ya baraza kuu la vijana kumteua Bashe, anayeelezwa kuwa mfuasi wa karibu wa Mbunge wa Monduli Edward Lowassa, kuwa mwenyekiti wa kamati ya kutafuta mpasuko ndani ya umoja huo.


  Aidha, hatua ya Shigella kuridhia baadhi ya vijana kutoa kauli, tena nje ya vikao, kuituhumu serikali ya baba yake na CCM, inatajwa kuwa ni kiini kingine cha mivutano kati ya Ridhwani na kigogo huyo.


  “Shigella na Benno hawataki kumtumikia Ridhiwani, badala yake kukitumikia chama. Kuona hivyo, Ridhiwani na kundi lake wakaamua kutafuta njia ya mkato kuvunja uongozi wa sasa wa UV-CCM,” ameeleza mtoa taarifa.


  Pia alisema wanachama wengi watajiweka kando kwa sababu ya mfumo mbovu wa uendeshaji wa chama hicho ikidaiwa kuwa “kama huna fedha, huna nafasi ya kushiriki uchaguzi wala huwezi kushinda…mfumo huu hauvutii vijana; CHADEMA inawavutia, wanakwenda huko.”


  Amesema kwamba CCM haina budi kubadilika kwa sasa. Badala ya kujadili watu ijikite kwenye kujadili na kutafuta ufumbuzi wa matatizo ya watu.   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  May 27, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Hii inaniogopesha kweli Mtoto wa Rais ana nguvu zaidi ya Makamu wa Rais, ina onyesha ameteua Wakuu wa Wilaya wengi zaidi hata ya Waziri Mkuu.

  Ni kwanini nchi yetu inaendeshwa kama MAFIA CULT? a family business? Hii ni hatari sasa 2015 kwa CCM nani ni Raisi?

  Inaogopesha Familia ya Rais ina Nguvu sana.
   
 3. Tango73

  Tango73 JF-Expert Member

  #3
  May 27, 2012
  Joined: Dec 14, 2008
  Messages: 1,678
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 135
  Mimi ningekataa post za ukuu wa wilaya mpaka serikali inihakikishie kuwa inapeleka au kujenga maktaba nyingi wilayani.
  maana mkoa au wilaya bila maktaba ni sawa na mbuga za wanyama bila kuwepo huduma za maji.
   
 4. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #4
  May 27, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Hivi taarifa ya Kamati ya Bashe kuhusu mifarakano na minyukano ndsni ya UVCCM ilishawahi kutolewa?
   
 5. g

  gpluse JF-Expert Member

  #5
  May 27, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 394
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 80
  Upumbafu!
   
 6. K

  Kidogo chetu JF-Expert Member

  #6
  May 27, 2012
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 1,381
  Likes Received: 771
  Trophy Points: 280
  kaa karibu na waridi unukie
   
 7. B

  BigMan JF-Expert Member

  #7
  May 27, 2012
  Joined: Feb 19, 2007
  Messages: 1,097
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  kama wewe ni mkereketwa wa maktaba ukichaguliwa kuwa dc ni wajibu wako kwa ubunifu wako kuhakikisha unajenga hizo maktaba na siyo kusubiri serikali
   
 8. m

  mzee wa njaa JF-Expert Member

  #8
  May 27, 2012
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 1,368
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Takataka hii. Unafiki mkubwa kwenye habari hii. Mimi si muumini wa kushabikia udaku. Mwanahalisi=udaku.
   
 9. B

  Bangoo JF-Expert Member

  #9
  May 27, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 5,594
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Serikali ya kishikaji
   
 10. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #10
  May 27, 2012
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Kuna kipengele chochote cha katiba kilichovunjwa katika uteuzi huo?
  Kumbukeni katiba inmruhusu rais kumteua hata kimada wake kuwa mkuu wa mkoa au wilaya, sembuse marafiki wa mtoto wake!!
   
 11. myao wa tunduru

  myao wa tunduru JF-Expert Member

  #11
  May 27, 2012
  Joined: Mar 9, 2010
  Messages: 615
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 35
  Imekaa kidhana sana hii habari!siipi nafasi!
   
 12. Andrew Nyerere

  Andrew Nyerere Verified User

  #12
  May 27, 2012
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 3,025
  Likes Received: 1,203
  Trophy Points: 280
  Hapo sijaelewa. Ridhiwani anajiandaa kugombea nafasi gani 2015? Nauliza hivi kwa sababu Jumamosi iliyppita walifika Waislamu wawili hapa Msasani,wamevaa kanzu,wanasema wamepotea njia,wameambiwa Ridhiwani anaishi hapa. Nikiwaelekeza,nendeni mkapande daladala,nendeni hivi,nendeni hivi,mtafika nyumbani kwake Ridhiwani. Wakasema 'asante' wakaondoka.
   
 13. MNAMBOWA

  MNAMBOWA JF-Expert Member

  #13
  May 27, 2012
  Joined: Oct 17, 2011
  Messages: 1,984
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  msiwaaminishe wa tz vitu ambavyo havipo,, kwani ni kosa rais kuwa na mtoto?
   
 14. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #14
  May 27, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,437
  Likes Received: 19,791
  Trophy Points: 280
  ana nguvu kwa sababu alipiga kampeni
   
 15. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #15
  May 27, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Halafu mtu anataka kunishawishi kwenye KATIBA mpya tuendelee na hawa ma-CD aka ma-DC
   
 16. mchuziwanyoka

  mchuziwanyoka JF-Expert Member

  #16
  May 27, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 374
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  ulitaka ampe mama yako
   
 17. Mchochezi

  Mchochezi JF-Expert Member

  #17
  May 27, 2012
  Joined: Feb 29, 2012
  Messages: 6,953
  Likes Received: 1,155
  Trophy Points: 280
  nahisi huyu Ridhiwani naye ni waziri asiye na wizara maalum
   
 18. wagaba

  wagaba JF-Expert Member

  #18
  May 27, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 829
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  cheo cha DC ni fadhila tu inatolewa. sioni kama ni tatizo Riz1 kuwapa ulaji washikaji. katiba haijavunjwa. shughulika na katiba mpya kutokomeza fadhila hizi. futa hiki cheo, it will be the lasting solution.
   
 19. alberaps

  alberaps JF-Expert Member

  #19
  May 27, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,450
  Likes Received: 804
  Trophy Points: 280
  Huyu anashikilia kile kiti cha Mrema cha Naibu waziri Mkuu
   
 20. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #20
  May 27, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Kama ni kweli Ridhwani alisaidia kuteua Ma DC pasi tunatawaliwa na serikali ya wajinga!!
   
Loading...