Kipenzi Changu
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 57,954
- 134,034
VIROBA VYA MADARAKA.
Imeandikwa na Richard Mabala.
MPENZI Frank,
Njoo mpenzi wangu. Siku nyingi sijakuona jamani? Nahitaji sana kukuona, kukukumbatia kama binadamu halisi, binadamu wa kawaida ili niweze kulinda akili yangu dhidi ya maajabu yote yanayotendeka hapa.
Mara Bosi ashike fimbo kuwachapa watu ambao hawakubaliani naye, mara amtwange mke wake licha ya uvumilivu wake wote, mara atake kumtwangilia mbali dada wa mke wake. Umchape shemeji kweli? Jamani.
Kitu cha mwisho kilichowatibua watu wote ni Bosi kurudi juzi na kudai kwamba hakuna kumkosoa, wala kumkejeli, wala kumpinga kwa sababu yeye ni mteule wa Bosi Mkuu hivyo, kumkejeli yeye ni sawa na kumkejeli Bosi Mkuu jambo ambalo ni sawa na uhaini kabisa.
Kumkejeli yeye ni dalili tosha kwamba mtu anayekejeli si mzalendo, ni msaliti. Duh! Si tu umpende bosi wa nchi, ni sawa, lakini upende pia watu wote wanaomzunguka.
Basi nakuambia mpenzi, ilikuwa patashika baada ya hapo. Kwanza, ingawa Bosi alisema hawezi kutingishika kwa sababu ni mwamba wa mwamba mkuu, imebidi atumie ile fimbo yake ya kumchapa SB kwa namna tofauti. Bado anachechemea kutokana na nguvu alizotumia katika kufukuzana naye.
Nadhani misuli imeshtuka maana hajazoea kufanya mazoezi yoyote zaidi ya ya mdomo anapopiga kelele jukwaani. Kwa hiyo inabidi atembee na fimbo tehe tehe tehe.
Ndipo hapo, Mama Bosi alipomkejeli akatoa tamko lake la ajabu. Alionesha wazi kwamba asingekuwa anachechemea, angemzaba MB kibao kingine tena.
Basi safari hii MB hakuvumilia kabisa. Alinyamaza kwanza lakini, kesho yake, sote tukamsikiliza Bosi akiondoka kwenda kazini na wimbo wa majivuno:
We unayeringa
Eti wanipinga
Wewe ndiwe mjinga
Hutapata kinga
Mbele ya tingatinga
Huko nyuma, MB akampigia makofi kwa kejeli kabisa kisha akatuita mimi na Binti Bosi.
‘Mimi sijui baba yenu amepandwa na wazimu gani hadi anashindwa kuelewa hali halisi. Hivyo sioni sababu kuendelea kukaa hapa nyumbani na kudhurika bila sababu. Uliona alitaka kupiga hata mdogo wangu? Kwa hiyo kusanya nguo na vitu vingine mnavyovihitaji, twende tukakae kwa mjomba wangu kwa siku chache, hadi baba arudiwe na akili.’
BB alimkumbatia mama yake.
‘Asante mama. Yaani nyumba yetu imekuwa kama jela. Hujui ni wakati gani utatishwa na hata kupigwa. Bora kumwacha baba hadi akili zake zirudi.’
‘Sawa mwanangu. Tusisahau kwamba bado kuna viongozi wengi wanafanya kazi vizuri. Unajua madaraka ni kama mvinyo.’
‘Si ndiyo pombe mama.’
‘Wewe! Nilijua utaanza kuleta maneno yako tehe tehe tehe. Mimi nimesema mvinyo. Wengine wanaweza kunywa huu mvinyo taratibu na bado wakazidi kuchangamkia kazi vizuri. Naamini tumeona mifano yao.
Lakini wengine wakinywa madaraka kidogo tu, wanalewa vibaya na kutaka kufanya na kusema mambo ya ajabu kabisa. Mtu kama huyu ni kumwacha hadi aamke huku kichwa kinawanga. Hebu fanyeni haraka twende.’
Basi mpenzi wangu, tukaondoka kwa furaha ingawa mimi nilisikitikia kitu kimoja tu. Ningelipenda sana kuona sura ya Bosi aliporudi jioni na kukuta nyumba imehamwa. Sijui alianza kuzungukazunguka huku akiita. Au alihisi mara moja?
Potelea mbali. Tupo hapa kwa mjomba wake MB. Hadi sasa Bosi amejaribu kupiga simu mara kadhaa lakini MB anamjibu kwa SMS tu.
‘Acha ufyatu kwanza.’
Wakati huu nakula raha tu, maana kuna msichana mwenzangu hivyo tunasaidiana kufanya kazi zote za nyumbani.
Naomba hii likizo iendelee … na hata wewe uje kwa wakati huu maana nina muda zaidi na sijui itachukua muda gani hadi Bosi ashtuke kweli na kujitafakari.
Sijui kweli maana naona kama ni ugonjwa wa kuambukiza. Kuna siku kijibosile fulani alimchapa mtu kwa kutojua jina lake, au kuwatia watu ndani kwa sababu za ajabu kabisa.
Mwisho nadhani mtendaji wako wa kata ataanza na yeye kwamba haturuhusiwi kuhoji mchango wa vyoo vya shule umekwenda wapi maana yeye naye ni mteule wa wateule wa bosi mkuu. Haya mambo yataishia wapi mpenzi?
Au labda mimi nikienda sokoni, na hawa vijana wasio na staha wakianza kunipigia miluzi nidai wakamatwe maana mimi ni mwajiriwa wa mteule wa mwenyewe tehe tehe tehe.
Maana kweli hii ni njia ya kuwakomesha na limfumo dume lao. Ingawa kwa kweli naona hata huu ubabe wa hawa viongozi ni limfumo dume pia, tena limfumo dume la watu wasiojiamini kabisa.
Mwenye kujiamini ataogopa wapi mawazo mbadala au hata kejeli. Nakumbuka ile hadithi ya chekibobu wa sokoni alipopigwa mkumbo kwa bahati mbaya na lijitu la nguvu. Wacha chekibobu aanze kutukana na hata kutaka kulipiga lile jitu.
Jitu likaomba radhi kumbe bahati mbaya lakini chekibobu akazidi kupayuka.
‘Lione. Jitu zima linaniogopa. Njoo tupigane tuone nani dume.’
Hata sisi tulishangaa kidogo hadi rafiki yake yule chekibobu akamvuta mwenzie.
‘Wewe mjinga nini? Hujui huyu ni bingwa na ndondi Tanzania. Ameshawachapa watu wa nchi kibao.’
Kumbe anayejua nguvu yake hana haja ya kuitambia.
Akupendaye daima dume wangu wa maisha.
Hidaya.