Mimi sio sana shabiki wa mambo ya siasa, lakini kwa yale yanayoendelea nchini imenipasa na mimi nitoe neno kidogo.
Matokeo ya utawala wa kidikteta ni mabaya sana. CCM ni Watanzania kama sisi, lakini kwanini waone ni sawa nchi kuingia kwenye machafuko makubwa kisa tu kupenda madaraka?
Ni vyema wakumbuke kuwa yote yanayotokea leo katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ni matokeo ya uroho wa madaraka wa Mobutu, uliosababisha wananchi wake kuunda vikundi vya waasi ili kumuondoa madarakani. Hadi leo, DRC imebaki kwenye mateso na machafuko yasiyoisha.
Sitashangaa hali kama hiyo kuanza pia Tanzania endapo kulazimisha madaraka kutaendelea. Kwa sababu sidhani kama ndugu ambao watapigwa na kuuliwa watakubali kirahisi bila kupambana.
CCM waangalie njia ya kuokoa taifa, maana madaraka yapo tu – lakini maisha ya wananchi hayana mbadala.