Richard kasesela ndani ya TBC anaongea

Amesema MAT si chama rasmi cha masaktari. Amesema ni NGO tu. Mbunge huyu wa zamani ametoa kauli hizi akiwa kwenye jitihada za kuitetea serikali kupitia TBC. Hawa ndio wazee walioitafuna nchi na kuiacha mifupa leo hii wameitwa kupiga propaganda. So saad.

Hivi ni lini na yeye atarudisha zile pesa alizokopa BoT kwa ajili ya kwenda kujenga kiwanda chake cha kusindika Nyama kule Sumbawanga? Bora ameongea tumekumba deni letu tunalomdai tukawalipe Madaktari wetu.
 
wewe unategemea mtu anayealikwa na TBC atazungumza nini kuhusu jambo lolote linaloihusu serikali?
 
inashangaza hatukumsikia wakati wananchi walivyotiwa risasi huko sumbawanga.
 
Siyo mkopo wa bilion 9 tu bali amejimilikisha mradi wa maji uliofadhiliwa na serikali kwa ajili wa wananchi wa huko kwela sumbawanga. eti mradi uko kwenye shamba lake.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Mzindakaya anatowa wapi moral authority ya kukashifu madaktari? Ana uadilifu gani huyu mzee? Ni zile hela za walipa kodi alizokwepua BOT? Au ni ubanafsi wake wa kugeuza mradi wa maji wa wanakijiji kuwa wake?

Kinachomfanya aone hii serikali ni ya maana ni kwa sababu wamempa cheo huko NDC? Mzee mchumia tumbo anajua adha wanayopata wagonjwa kwa kulazwa sakafuni?

Eti MAT sio chama rasmi cha madaktari? Hata kama MAT ni NGO, ina maana watu walio kwenye NGO hawana haki nchi hii? Kumbe madaktari wanateswa kwa sababu wako chini ya NGO?

Mzindakaya anaweza kuwa kwenye list ya wateule wa safari za Apolo, lakini kwa mambo ya mifupa atakuja MOI. Na hapo ndio utajua MAT ni NGO au la?
 
Mjadala unaendelea na Dr Kasesela anaonekana anaunga mkono uamuzi wa serikali tena amejipambanua kuwa mwanasiasa na anashangaa kwanini madaktari wagome ilhali watanzania wanapoteza maisha?
Wote wanaolaumu madaktari ni vipofu? Mbona hawataki kuangalia upande wa pili wa shilingi ambao ni serikali, kwanini serikali isiwajibike kuokoa maisha ya watanzania kwa kutekeleza madai ya madaktari?

My take:
Serikali sikivu iwajibike kuokoa maisha ya watanzania ambao ni maskini na hawana uwezo kupata huduma kwenye hospitali za binafsi na nje nchi, vinginevyo tuendelee kuamini kuwa serikali yetu sio sikivu.

Huyu Kasesela unamtambulisha wewe kama Dr. ama alijitambulisha mwenyewee?? Nasikitika kusoma comments zao, kwani wanahusika na hiyo meza ya majadiliano? Wanatoa ufumbuzi, ama wanaeneza propaganda na kukuza/KUPANDIKIZA chuki kwa madaktari DHIDI YA WANANCHIß Wanafikiri madaktari wakirudi mahospitalini bila vifaa na mazingira bora ndiyo TIBA. Au wanataka Madaktari warudi tu Mahospitalini wakaidhinishe vifo vyetu. Hayaa bwana, ngoja tumsikie mzee wa kaya kesho, labda ataongea kitu. Hayaaa......
 
Wana jamii forum angalieni tbc sasa hivi mtaalam.Richard Kasesela anavyoshusha pumba kuhusu mgomo.wa madaktari

Ni aibu na fedheha kwa serikali kutetewa na mtu kama Richard Kasesela? How low can this government go?
 
Kasema alivyoenda mwanza kwenye sherehe za CCM.
Alikwamwa na mfupa kooni, akaenda hospital 3 hakupata huduma. Akaamua kwenda Bugando, akaja daktari wa kwanza, badala ya kumtibu akaanza kumuuliza mambo ya chama.
Akaja daktari wa pili aliyekuwa zamu, akaongea kingereza na mwenzi kama vile wanamteta maana amesema unajua watu wakituona na sare za chama wanadhani hatujui kingereza.

Afu wakamwambia njoo kesho bila kumtibu, akarudi na mfupa wake wa samaki kooni. Ikabidi akale ugali mfupa ukaenda.

Akawa anasema TZ ndo nchi pekee ambayo madaktari hawashtakiwi.

Hii stori yake sikuielewa, nisaidieni.
 
Umeniwahi... Kongosho...
 
Madaktari hawakuwa na vitendea kazi, wangewezaje kumtoa mfupa, wangemtoa kwa kijiti?
 
Wala msipoteze muda kujadili pumba za Kasesela,jamaa ni mweupe na mara nyingi huwa anapenda kujipendekeza. Alikua CR darasa MBA pale milimani.
 
Kwanini tbc wawaite wana siasa waongelee mgomo wa madr,hawawaoni hao madr waje waseme na watanzania wawaelewe,hao waliopo hapo ni mamluki wenye fani wapo wapewe nafasi wasikike.
 
amesema MAT si chama rasmi cha madaktari.amesema ni NGO tu.amepondea NGOs kwa kusema ni vikundi vya vurugu.mbunge huyu wa zamani ametoa kauli hizi akiwa kwenye jitihada za kuitetea serikali kupitia TBC.hawa ndio wazee walioitafuna nchi na kuiacha mifupa leo hii wameitwa kupiga propaganda.so saad.....

Mzindakaya....Huyu ndiye yule kiumbe aliyechimba BWAWA la KIJIJI kwenye shamba lake?
 
Amesema ana degree mbili kabla hata kabla hajaulizwa kiwango cha elimu yake
Akina misifa wapo wengi kaka ,Dully hayupo peke yake,jamaa kazitungia mashairi hizo degree zake mbili,popote aendapo ndio zimekuwa Intro
 
Anasema kuwa udaktari ni wito na wote wanaogoma ni kutokana kushuka maadili

Yuko sahihi kabisa na we unalijua hilo. Kama kweli umeshawahi kwenda hospitalini kwa kuugua mwenyewe au kuuguza ana jua fika jinsi wanavyo toa huduma. Maadili yamekuwa mabovu na hiki ni kizazi cha migomo ya ud miaka iliyopita. Hapa kuna haja ya kubadili mitaala inayotumika kwani haiwajengi kuwa waadilifu.
 
Back
Top Bottom