RFA mnakera mnafikiri WANANCHI hawajui kinachoendelea kati ya CCM na CDM

RFA mnakera mnafikiri WANANCHI hawajui kinachoendelea kati ya CCM na CDM

Ushauri wa bure sikiliza redio maria utabarikiwa zaidi.
 
Radio one na Itv ndo habari ya mujini,Rfa tulishawachia wachunga ng'ombe wa Simiyu na Igunga!
 
Jana asubuhi katika kipindi cha magazeti mtangazaji alisoma maoni ya mhariri yanayohusu kukamatwa kwa Msigwa na Kasulumbayi kwamba wamefanya vurugu.

Na leo pia katika kipindi hicho hicho kafanya hivo kwa kusoma maoni katika katika gazeti la Mtanzania mhariri akiwaponda wabunge wa CHADEMA waliokamatwa.

Kama hiyo haitoshi leo katika kipindi cha MATUKIO ikaripotiwa habari ya wanachama wa CCM waliojeruhiwa wakiwa hospitalini lakini cha kilichonishangaza ni pale watangazaji walipoanza kuikoleza hii habari kwa kuunga mkono kauli ya mwenyeketi wa CCM-Shinyanga ili kuisafisha CCM na kuiharibu taswira ya CHADEMA.

Maswali yangu kwa RFA:
1. Hamkuona Machemli na Kiwia (wabungu wa CHADEMA) hapo mwanza walipokatwa mapanga? Mbona hamkufanya hivo?
2. kule arusha bomu lilirushwa mkutanoni (CHADEMA) lakini hamkwenda Mount meru wala Seliani?
3. Aliuawa Masud Mbwana huko Igunga kwenye kampeni, lakini ninyi mnaona vurugu akiumia wa CCM?

Maoni yangu:
Ni bora mkafanye kazi za CCM kuliko kuwa chombo cha habari bila kuwa biased kuliko kueneza propaganda chafu dhidi ya CHADEMA.

Kupitia RFA Mgeja anasema vyama vingine vinashindana kwa hoja, sasa mimi naona chama kizuri kwa CCM ni ambacho hakina nguvu. Tunakumbuka NCCR na CUF walivopakaziwa uchafu wa kila aina lakini leo Mgeja anasema ni vya kistaarabu?

Kama RFA mnaona propaganda zina msaada mbona Anton Diallo mwenye redio hamkuweza kumnusuru 2010?

Mwisho kabisa nasema endeleeni kutumika ila tutawaonyesha njia.
.Nashangaa wanafanya watu wajinga utafkiri Mungu alishakufa.Kwa kweli Mungu atawaumbua pamoja uwezo wa kumiliki vyombo vya habari karibia vyote.Hata Ghadafi alicheza Muda mrefu lakini kwa siku moja umaarufu wake ulipotea na yeye mwenyewe.
 
Rfa, na SMG kwa hili mjirekebishe. Taaluma ya habari mnaipeleka kichakani. Tunawapenda, lkn msiwe kama wale wengine wanaaojiita public media
 
doto bulendu kabaki peke yake pale ambaye anaweza kunishawishi kumsikiliza wengine hewaa


Doto Bulendu, amejaa weledi. Ni mtanagazaji anayebeba uwezo mkubwa katika tasnia ya habari

Chochote aongeacho huwa yupo makini sana kubalance habari nakama anamhoji mtu lazima ahakikishe anafanya

hivyohivyo kwa upande wa pili, na inapotokea kupotoka kwa mhojiwa katika vipindi vyake yeye huweka mambo sawa

pamoja na kuomba radhi kwaniaba ya mgeni wake awapo studio.


Kwa siku za hivi karibuni Star TV hasa kipindi cha magazeti asubuhi kinaniboa sana kiasi kwamba jana na leo nimelazimika kuhama

kituo kwa maudhi, habari kwao ni zile za mipasho na propaganda hasa za kuinadi ccm na kuponda wapinzani. Inaniudhi

kwasababu nyingi za habari wanazo zipa airtime ni za upotoshaji na uwongo na kwamba nawaza kufikiria vinginevo juu ya

chombo hiki.
 
Ushauri wa bure sikiliza redio maria utabarikiwa zaidi.

Hii ndio redio yangu, nikibadili nasikiliza BBC. Niliacha kusikiliza RFA kwa kuwa watangazaji wanajitahidi kupaka CCM mafuta kwa mgongo wa chupa ili wapate ukuu wa Wilaya. Nahisi mmiliki anayajua haya, na yeye ananufaika kwa kupata matangazo na punguzo kubwa la kodi.
Kushindwa kuwianisha habari kunanifanya nichuke chombo husika siku nzima.
Nashukuru ITV/Radio One wanajitahidi kuweka habari za vyama vyote, pia watangazaji wake si waropokaji kama wale jamaa wa Clouds.
 
Back
Top Bottom