Revised question: Kosa la Gwajima ni lipi?

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
371,548
Reaction score
860,611
Mimi si muumini wa kanisa la ufufuo na uzima wala Gwajima sio role model wangu.. Lakini kitendo chake cha kukemea utekaji wazi wazi na kutaka hatua stahiki zichukuliwe kiliwagusa wengi
Baada ya hapo alipata mashambulizi ya kutosha hasa ndani ya chama chake.. Naye hakukaa kimya bali alirejea na kutangaza maombi kwa wahanga mbalimbali nchini wenye kesi za uhaini, waliotekwa na hata wanasiasa pia..
Maombi yalianza jana na hapohapo ikatoka barua ya kulifungia kanisa lake
Je kosa la Gwajima ni lipi mpaka sasa?
Kukemea utekaji?
Kutaka wahusika watafutwe?
Kuwafanyia maombi wahanga mbalimbali?
Hivi tumefika mahali hata maombi tunayaogopa?
Your browser is not able to display this video.
 
Sw
Swali zuri,ila majibu hutopata!
 
Gwajima angekemea utekaji bila kumshambulia Rais na vyombo vya usalama yasingemkuta yote haya. Mbaya zaidi akatumia kanisa lake kupiga propaganda za kisiasa na vitisho. Kajilipua kijinga mno. Acha DOLA imshikishe adabu.
 
Kukemea utekaji, mauaji hovyo ya raia, nk.! Na pia kuijulisha jamii ya kwamba wakuu wa vyombo vya usalama wanatakiwa kuteuliwa kwa kufuata mfumo bora zaidi kuliko huu wa sasa wa kuteuliwa na mwanasiasa mmoja tu.
Kwa makosa haya anaweza kupewa kesi ya uhaini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…