Result slips za Form Four 2015/2016

katima

Member
Aug 22, 2012
96
58
Ndugu wadau wa JF nina mdogo wangu amemaliza kidato cha nne mwaka jana matokeo yake siyo mazuri sasa ametaka kujiunga na chuo cha ualimu ila mpaka leo anafuatilia results slip mpaka leo hajapata shuleni kwao.....mwenye maoni zaidi ya hapa anisaidie!!!nimefika hadi NACTE wamesema washazituma shule ila tukienda shuleni wanadai bado na mwisho wa ku-apply vyuo ni 31/05
 
ImageUploadedByJamiiForums1459171516.473130.jpg
 
Ni kweli walimu wakuu wanabania sana hata mimi nimefatlia ya mdogo wangu bila mafanikio
 
Huyo mwalimu wao mkuu ni mzembe,wamkomalie
Nashindwa kuelewa hizi shule za private huwa wanapata result slips tofauti na zinazotolewa na serikali au nini!! Maana haiwezekani matokeo yatoke then wasitoe results slips zao.
 
Ni kweli walimu wakuu wanabania sana hata mimi nimefatlia ya mdogo wangu bila mafanikio
Kuna kila sababu ya kumtafta afisa elimu wa mkoa aiseeeeee hapa maana mtu unaharibu nauli kufatilia bado unaambiwa eti bado hazijatoka na ukienda NACTE wanakwambia tumeshazituma
 
Mkuu NACTE hawatoi results slips. Anayetoa ni NECTA.
Pill,results slips zinatoka wiki mbili baada ya matokeo. Hivyo mpaka kufika Shuleni itakuwa wiki ya tatu mpaka ya nne. Huyo mwalimu mkomalieni,azifatilie haraka
Kuna kila sababu ya kumtafta afisa elimu wa mkoa aiseeeeee hapa maana mtu unaharibu nauli kufatilia bado unaambiwa eti bado hazijatoka na ukienda NACTE wanakwambia tumeshazituma
 
Huitaji result slip kuapply.. application zote zinapitia nacte, unaingiza jina na namba ya muombaji system inalink na NECTA
 
Samahan wadau naomba msaada kwa anayefahamu kuhusu hili, kuna dogo wangu amemaliza form four mwaka jana 2015 kila akiingia NACTE kwa ajili ya kufanya application ya Kozi anaambiwa namba yake ishatumiwa na mwombaji mwingine lkn huyo dogo hajawahi omba nacte zaidi ya siku hiyo na kwa mara ya kwanza lkn anaambiwa namba yake ishatumiwa, msaada kuhusu hili wadau.
 
Back
Top Bottom