Restituta Mbogo: Wakina Mama hakikisheni Wanaume wanaandika majina yenu pindi wanaponunua ardhi

na wanaume tuhakikishe yanaandikwa majina yetu akinamama wanaponunia ardhi na mali myinginezo...au ndio "changu-chetu, chako-chako mwenyewe"...

Ni vyema akapambana ianzishwe sheria kila mali inayotafutwa mkiwa kwenye ndoa badi iandikwe majina ya watoto na mkiachana mali ibaki chini ya mahakama mpaka watoto wafikishe miaka 25.... kama mmeachana hamna watoto basi kila mtu achukue kile alichochuma kwa jacho lake....

Kuwe na mikataba kabla ya ndoa inayosema nani amekuja na nini kwenye ndoa, nani anafanya kazi gani, kila kipato cha mtu kiwe wazi...ili mwisho wa siku kila mtu abaki na chake...na ndoa iwe ni sehemu ya kuburudishana tu na kutafuta watoto.....
 
Nanyi mkinunua andikeni majina ya akina baba vivyohivyo!!!
 
Hivi kwanini kwenye Ndoa WANAWAKE akili zao sikU zote wanawazaga Mwanaume tu ndie atakae tangulia Kufa
Uzoefu unawafundisha hivyo katika jamii kwa kutafakari tangu ngazi ya kaya mpaka TAIFA !

Mfano angalia wajane na wagane ni akina nani wengi kwenye jamii ? Anza kwa wanasiasa maarufu na wafanya biashara wakubwa Tanzania !
 
Wabunge wa ccm kuchangia hoja zenye maslahi ya taifa ni 0% ,wao wapo kwa ajili ya matumbo yao tu
 
Dah, Weee jamaaaa
 
Wanaume mnaoona kama wake zenu watawaibia au watawafilisi, msiowe. Bakini kuwa ma bachelors, bakini na vimada wenu, zaeni hovyo hovyo kama wanyama pori. Maisha yanaendelea. Familia zenu zitawapeni presha tuu lakini haziwezi kuwalazimisha kuowa. Mambo ya ndoa waachieni wanaume wanaoyaweza na ambao wako tayari kuungana na wake zao wawe kitu kimoja. Hakuna cha kwangu, hakuna cha kwake, vyote ni vyetu pamoja.
 
kwa lile tukio la kufungishwa ndoa ya kimila, kama ndo mimi, wala nisingemuoa.
 
Ukweli ni kwamba, baada ya safari ngumu ya kutafuta na kulea watoto wakafikia utu uzima, siku za mwanaume huwa zinaanza kuhesabika.

Ndio maana wazee wa zamani ilikuwa mtoto wa kwanza, hasa wa kiume akielekea au akioa. Nae anaoa mke wa pili. Na kuhamishia kila kitu kwa mke mdogo.

Kwa sababu, wanawake wanajuana. Ndo maana wazungu wanakamsemo kao "it takes a monster to fight a monster". Mkubwa akitaka kukutoa relini, mdogo anajibu mapigo.

Siku chache zilizopita kuna jirani yetu kafariki kwa ukweli uliowazi. Akauawa na mkewe.

Tuishi nao kwa akili.
 
Huyu Mbunge mjinga sana.
Na mchepuko huandika wapi?
 
Hivi kwanini kwenye Ndoa WANAWAKE akili zao sikU zote wanawazaga Mwanaume tu ndie atakae tangulia Kufa
... kuna ukweli wa kisayansi na kijamii kwenye hili. Kisayansi, jini (genes) za kiume ziko weak kuliko za kike hivyo probability ya mwanaume kufa mapema ni kubwa zaidi. Kijamii, ni utamaduni kwamba wanaume huwazidi wenza wao umri.

Ni nadra sana kukuta mke wanalingana au kamzidi mume umri. In most cases wanaume kuwazidi wake zao by 5 to 10 years, even beyond, is very common. Kutokana na umri mkubwa, probability ya mume kufa kabla ya mke ni kubwa.

Pia kijamii, life style ya wanaume inawaweka kwenye risk kubwa ya kufa mapema kuliko wanawake. Kwa mfano, ulevi uliopindukia, uvutaji sigara, wake wengi/vimada na kote huko ni lazima uhudumie pamoja na kubeba kero zao inaongeza msongo wa mawazo hatimaye pressure, visukari, etc.

So, ukichanganya dimensions zote, men are in a high risk to die earlier than women. Wala haihitaji ushahidi wa kisayansi.

Na ukichunguza utakuta lugha za "ukifa nitaishije na watoto" hutolewa zaidi na wake ambao wamezidiwa sana kiumri na waume zao; au wale ambao life style za waume zao zime-deviate sana from normal! Yaani wewe ni kawaida kupotea nyumbani wiki nzima bila maelezo ya kueleweka halafu mke awe na amani; how?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…