Restituta Mbogo: Wakina Mama hakikisheni Wanaume wanaandika majina yenu pindi wanaponunua ardhi

Mbunge wa Viti Maalum Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Katavi, Mhe. Taska Restituta Mbogo, ametoa wito kwa akina mama nchini kuhakikisha wanaume zao wanaandika majina yao wanapokwenda kununua ardhi ili kuepuka matatizo ya baadaye pindi mmoja wao anapofariki dunia.

Mhe. Restituta ametoa ushauri huo wakati akiwasilisha hoja Bungeni, Dodoma na kueleza kuwa wakina mama huwa wana tabia ya uvivu wakuweka majina yao kwenye ardhi ilihali sheria inaruhusu watu wanawake kumiliki ardhi.

“Ningependa kutoa ushauri wa jumla kwa wakina mama wa Tanzania, waume zetu wanavyonunua ardhi na sisi tuhakikishe majina yetu yanakuwepo pale pembeni, kwasababu wamama wengi wamekuwa wakidhulumiwa nyumba na mashamba,” amesema Mbunge Taska Restituta.

Mbunge huyo ameongeza kusema kuwa, “Tusiwe wavivu kununua viwanja, tusipende kuwatuma akina baba halafu hawaandiki jina lako unakaa pale kwa miaka 40 unaonekana wewe ni mpangaji,” amesema Mhe. Restituta.

Naye Mbunge viti maalum Mhe. Sophia Mwakagenda akitoa taarifa bungeni ameungana na hoja iliyowasilishwa na Mhe. Restituta.

“Mhe. Spika lakini waume hawa wanapoenda kununua viwanja hawatuagi, na wakati mwingine ananunua akiwa amefariki bahati mbaya, unashangaa kumbe wake mko sita wakati unajua uko peke yako,” amesema Mhe. Sophia Mwakagenda.
Huyu Na Kaka Yake Wote Ni Wabunge, Kaka'ake Alikuwa Ni Mlinzi Wa Mwendazake. Wanatokea Katavi
 
Hoja murua na iko makini, safi sana. Wamama hoyeeeeeeh.

Ila mie nasemaga mwanamke anaye yumbishwa na mwanaume labda kapenda au anakwama sehemu.

Mbinu zote hizi tena nyingi mno za kumdhibiti mwanaume, khaaaaah.

Sent from my Infinix X652C using JamiiForums mobile app
 
Angesema mali ziandikwe kwa majina ya wanandoo tungeelewa siyo kudai wanaume waandike kigezo wakifa? Amekuwa ungu
Upumbavu Sana huu,

Tena UPUUZ Kama huu huu uliwai sababisha nmeish na mke miaka 12 sijafunga nae kabisa Ndoa,

Unakaa zako Unawaza ukishaweka mambo sawa Ubariki ndoa.

Unashangaa mwanamke anakuamsha usiku kukuambia
"Baba D, fanya tufunge ndoa mme wangu. Endapo ikitokea Mungu amekuchukua gafla nitabaki katika mazingira gani"

Unabaki unajiuliza,
"Ina maana uyu mtu anajua kabisa Mimi ndo ntakaetangulia?"

Unaghairi, Unafanya Mambo mengine.

Kuna siku niliwai kukosana na ba mkwe, kisa kunitumia tumia watu wanipush tufunge ndoa.

Ba mkwe anakuita kukuambia
"Mwanangu, fanyeni mfunge Ndoa,
Kuna kesho na keshokutwa Unaweza usiwepo wajukuu wangu uyu akakosa haki zao za msingi"

Nikamjibu TU kwa kifupi Kisha nikaondoka zangu,
"Nikiwa tayar nitakujuza mzee"

sikU moja ikatokea harusi ukweni, tumehudhuria shemej yangu mmoja anafunga Ndoa ya kimila.

Nashangaa Wazee wananiita chumba Cha kumuandaa bwana harusi, nakunikaribisha kiti jirani na bwana harusi mhusika.

Nashangaa kuona wanaingia waandaaji wanaanza kuniandaa Kama alivokua bw.harusi,

Nikamwambia,
"Ebu subiri, Nini kinaendelea hapa"

Wakajibu,
"Tumeelekezwa na mkwe wako tukuandae Kama P na wewe ufunge Ndoa leo leo."

Nikanyanyuka nikatupa makorokoro yao nikaondoka nje.

Niko nje ba mkwe ananifata,
"Vipi kijana mbona umetoka nje wkt Kila kitu Kisha kishaenda sawa"

Nikamwambia,
"Mzee mbona hamkuniandaa kwa zoezi la Ndoa, ninachojua nimekuja hapa kujumuika Kama wanafamilia wengine Kwenye harusi ya shemej yangu"

Akasema,
"Mi mbona mkeo nilimwambia na anajua na maandaliz yote anafahamu"

Nikamuita,
alipokutwa nae akaanza kujiuma Uma eti akajua kwa sababu Nilikua nawasiliana na mzee wake Basi alijua tayar ashaniambia, nikampuuza.

Nikamwambia mzee,
"Kwanza sijawai kufikiri kufunga Ndoa ya kimila, pia siwez kufungia Ndoa ya ukweni nilikooa na pia siwez funga Ndoa bila wazazi wangu au Ndugu zangu kuwepo"

Akasema,
" Sasa itakuaje, na tumeshatumia gharama"

Nikamwambia mzee,
"Mzee wangu Ilo la gharama zenu halinihusu,nnachojua Mimi siwez funga Ndoa sijajiandaa Kama nilivokueleza.
Maandaliz yangu yakiwa tayar nitakueleza na sitegemei kufunga Ndoa ya kimila,ilo sahau kabisa"

Nikapanda zangu usafiri nikarudi zangu KWANGU.

Niliporudi nyumban, na wife akarudi nikamuwakia Sana, nikamwambia
"Kwa mlichokua mnataka kunifanyia uko kwenu. Sitaki kuskia Tena habar za Ndoa nyumba hii, vinginevyo unatafuta ugomvi mkubwa Sana na mimi. hutak kuish na Mimi Basi Rudi kwenu wakakutafutie mwanaume mwingine"

Tangu hapo, Kulikaa kimya Kama Miaka 5 hivi mbele bila habar Tena za kupush Ndoa.

Na ndipo nilipoamua mwenyewe kufunga Ndoa rasmi kabisa ya KIDINI.


MWAKA WA 9 Sasa Kwenye Ndoa Rasmi
 
Hivi kwanini kwenye Ndoa WANAWAKE akili zao sikU zote wanawazaga Mwanaume tu ndie atakae tangulia Kufa
Leo nilikuwa nafanya research ndogo ya maeneo niliokulia,wababa karibia wote wameshakufa ila wake zao wote wapo hai,hapa nimeangalia familia zaidi ya 20 za majirani zetu,nadhani wanalijua hili kuwa sisi tunatangulia kufa zaidi kuliko wao,ndio maana wanapambana sana inapokuja swala la mali...
 
Back
Top Bottom