TANZIA: Producer Joshua Magawa "Pancho Latino" wa B hitz records afariki dunia

Hance Mtanashati

JF-Expert Member
Sep 7, 2016
17,459
21,179
BUhDecxls8w.jpg

Pancho Latino maarufu 'Mafia' amefariki dunia kwenye ajali ya kuzama kwenye maji wakati anaogelea kwenye kisiwa cha Mbudya, jijini Dar es Salaam

Pancho alikuwa mtayarishaji wa muziki katika studio za B’ Hitz Record.

Na miongoni mwa kazi zake maarufu ni pamoja na "MDANANDA" wimbo aliouimba Shetta na Tunda man, pamoja na wimbo wa "DAR ES SALAAM STAND UP" wa Chid Benzi, na ngoma nyingine nyingi kali.

Mwili wa mtayarishaji wa muziki Pancho Latino umehifadhiwa katika Hospitali ya Lugalo, Dar es Salaam kwa uchunguzi wa kifo chake.

Kul nafs dhaaika tul maut. Nyuma yako mbele yetu.

Upumzike salama .

RATIBA YA KUAGA:
1- Tunaaga ijumaa 12/10/2018 Lugalo Hospital..

2- kutakua na ibada ya kumuaga JOSHUA SIMON MAGAWA “ PANCHO LATINO ” itaanza saa nne asubuhi ikifuatiwa na kuaga kwa mwili wa marehemu kisha safari ya kuelekea GAIRO itaanza..
 
Back
Top Bottom