Report ya UNDP yaitaja Tanzania kuwa na Low Human Development index

OLS

JF-Expert Member
Oct 12, 2019
419
669
Human development index(HDI) inawezekana kuwa msamiati mpya kwa walio wengi kama moja ya kiashiria cha maendeleo ya nchi. Kwa walio wengi itakuwa tumesikia mara nyingi kuhusu ukaji wa uchumi (GDP) lakini GDP haikuwahi kuwa kiashiria cha maendeleo ya kiuchumi bali ni quantitative increase ya National Output. Siajabu watu wengi tumekuwa tukiikataa ule ukuaji wa 7% wa GDP kwa sababu hatuoni wananchi wakiakisi ukuaji huo.

Kutokana na sababu nyingi zilizoonekana kwa GDP katika upimaji wa maendeleo ya wananchi, the United Nations Development Program (UNDP) mwaka 1990 walianzisha kipimo kingine cha kuangalia ubora wa maisha ya watu kwa kuangalia viashiria vitatu vya uchumi, Kipato(Real percapital Income), afya na elimu. Tangu hapo UNDP ikawa inatoa kila mwaka kuona wananchi wanaendelea kiasi gani.

Nimeanza na utangulizi huo kwanza ili mtu apate picha ya maendeleo ya uchumi kwa hiki kipimo ambacho si maarufu sana. Mwaka 2010 UNDP ikaanza kutumia new Human Developmemnt index, haina tofauti na Human development index ya kwanza japo kuliwa na refinements kidogo, lakini report zao hadi sasa huwa zinaandikwa tu, Human development Index.

Human development Index (HDI) huanzia 0 – 1. Hivyo HDI huziweka nchi kwa makundi manne, low human development , medium human development, high human development, and very high human development

Report ya mwaka huu inaonyesha Tanzania kwanza ikiwa ni katika fungu la Low human Development Index, ni nchi ya 159 huku ikiwa na HDI ya 0.528, (Shhh! Tumefungana na Uganda, wote ni wa 159).

Ili nieleweke ngoja niwafanishia nan chi yenye HDI kubwa, nchi iliyoshika namba moja, ambayo yenyewe HDI yake ni 0.954, Norway hiyo, life expectancy yake ni 82.3, expected years of schooling 18.1, adjusted per capita income, zingatia Purchasing Power Parity(PPP) ni 68059$, sisi tuna life expectancy 65.5, expected years of schooling ni 8.1 huku per capita income ikiwa 2805.

Hii ina maana ya kwamba tunakufa mapema, lakini pia tuna wasomi wachache ndio maana expected years ni kidogo mno.

Hii ieleweke kwa wale wote ambao huangalia GDP kama kigezo cha kuangalia maendeleo ya watu.



NB: GDP inaonyesha economic growth (Kukua kwa uchumi) sio Economic Development( Kuendelea kwa Uchumi)
 
Back
Top Bottom