Return Of Undertaker
JF-Expert Member
- Jun 12, 2012
- 4,572
- 26,885
Taasisi ya REPOA imesema ili ndoto ya Tanzania ya viwanda ifanikiwe ni lazima kuwe na Mpango wa miaka mitano.
Mkurugenzi wa Mipango na Utafiti kutoka Taasisi hiyo, Dk Abel Kinyondo alisema kingine kinachohitajika ni kuwa na taasisi zenye nguvu ya kusimamia ndoto hiyo badala ya kutegemea mawazo ya kiongozi.
Akizungumza leo wakati wa maandalizi ya warsha itakayoanza kesho jijini hapa, Kinyondo alisema taasisi hizo zinatakiwa kufanya juhudi za kubadili fikra za watanzania juu ya matumizi ya bidhaa zinazozalishwa ndani.
Chanzo: Mwananchi