Yericko Nyerere
Platinum Member
- Dec 22, 2010
- 17,027
- 20,518
Chama cha upinzani nchini Msumbiji kimesema hakitayapokea matokeo ya uchaguzi yanayotarajiwa kutangazwa jumatano ya wiki ijayo.
Mpaka asubuhi hii matokeo yaliyokwisha tangazwa ni 24.58% ya kura zote, Nyusi anamzidi Dhlakama kwa 63.02% dhidi 29.42%. Simango ana 7.56%.
Kumekuwa na dosari nyingi ikiwemo udanganyifu, vitisho vya dola, watu wengi kukosa haki ya kupiga kura kwa sababu lukuki zinazotolewa na mamlaka, na ucheleweshaji wa matokeo bila sababu za msingi. Hii inapelekea kusema uchaguzi haukuwa huru na haki
Nimezungumza na Dhlakama anasema hataki kurudi mstuni, lakini uhuru wa Wanamsumbiji ikibidi utatafutwa mstuni tena.
Source: BBC
http://www.bbc.co.uk/swahili/habari/2014/10/141017_renamo_msumbiji

Alfonso Dlakama
Chama cha kikuu cha upinzani nchini Msumbiji cha RENAMO,kimetoa yake ya moyoni kuwa hawatayakubali matokeo yajayo ya uraisi na ubunge pamoja na serikali za mitaa.
Msemaji wa chama hicho Antonio Muchanga amesema kwamba kumekuwa na ukiukwaji wa taratibu katika upigaji kura huo na udanganyifu wa kura.
Matokeo ya awali katika uchaguzi huo zinaonesha kwamba chama cha FRELIMO kinaongoza katika uchaguzi huo.Wakati haya yakitokea kumekuwa na uvunjifu wa amani wakati polisi walipo ingia katika ghasia na waandamanaji waliokusanyika nje ya vituo vya kupigia kura kufuatilia zoezi la uhesabuji wa kura .
Ingawa wafuatiliaji wa uchaguzi nchini Zimbabwe wanaeleza kuwa pamoja na yote hayo,uchaguzi huo ulikua huru na wa haki.ikumbukwe kuwa chama cha Renamo na chas Frelimo walipigana vita ya wenyewe kwa wenyewe vilivyomalizika mnamo mwaka 1982.
Source: BBC
http://www.bbc.co.uk/swahili/habari/2014/10/141017_renamo_msumbiji