Reli Standard Gauge: Ujenzi umeshaanza Mkoani Pwani, katika eneo la Soga

Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
13,185
18,513
KATIBU MKUU WA UCHUKUZI ATEMBELEA ENEO INAPOJENGWA RELI MPYA YA KISASA YA STANDARD GAUGE

Tuesday, November 03, 2015

Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shaaban Mwinjaka,akiteta jambo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu Rwanda, Rwakunda Christian,wakati walipotembelea ujenzi wa reli mpya ya kisasa, iliyoanza kujengwa Mkoani Pwani, katika eneo la Soga.

Muonekano wa ujenzi wa reli mpya wakisasa Standard Gauge, ambayo inaendelea kujengwa katika eneo la soga mkoani Pwani.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shaaban Mwinjaka (wa tatu kutoka kulia), akiwa katika picha pamoja na Uongozi wa Taasisi inayosimamia usafirishaji katika Ukanda wa Kati pamoja na Viongozi wa Nchi zinazotumia ukanda wa Kati, wakati walipotembelea ujenzi huo hivi karibuni, katika eneo la Soga, Pwani.

Muonekano wa Vituo vya Reli hiyo Mpya ya kisasa ya standard Gauge, itakapokamilika.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu Rwanda, Rwakunda Christian, akiteta jambo na maafisa kutoka nchi zinazotumia ukanda wa kati kusafirisha bidhaa zao, wakati wakiangalia ramani ya reli mpya ya kisasa, walipotembelea ujenzi wa reli mpya ya kisasa yastandard gauge,hivi karibuni Mkoani Pwani. Viongozi hao walifurahishwa na maendeleo ya ujenzi huo kwa sababu utarahisisha usafirishaji wa mizigo kwani itapitisha mzigo zaidi na ukubwa wa reli hiyo utaongeza spidi ya treni.(Habari Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Uchukuzi)
 
Attachments

  • 1453801953921.jpg
    1453801953921.jpg
    32.2 KB · Views: 120
  • 1453801974553.jpg
    1453801974553.jpg
    33.1 KB · Views: 101
Hicho kinachoitwa "muonekano" tumeshavichoka jamani, tunaletewa mionekano kila siku, mara muonekano wa DART, muonekano wa fly over, muonekano wa kigamboni nk. alafu baadaye vinakua havionekani
mpaka sasa hivi DART haionekani
am sick and tired of mionekano
 
Pole sana kwa uchovu. Ujenzi wa reli umeanza, sijui ulitaka nini tena!?
 
KATIBU MKUU WA UCHUKUZI ATEMBELEA ENEO INAPOJENGWA RELI MPYA YA KISASA YA STANDARD GAUGE

Tuesday, November 03, 2015

Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shaaban Mwinjaka,akiteta jambo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu Rwanda, Rwakunda Christian,wakati walipotembelea ujenzi wa reli mpya ya kisasa, iliyoanza kujengwa Mkoani Pwani, katika eneo la Soga.

Muonekano wa ujenzi wa reli mpya wakisasa Standard Gauge, ambayo inaendelea kujengwa katika eneo la soga mkoani Pwani.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shaaban Mwinjaka (wa tatu kutoka kulia), akiwa katika picha pamoja na Uongozi wa Taasisi inayosimamia usafirishaji katika Ukanda wa Kati pamoja na Viongozi wa Nchi zinazotumia ukanda wa Kati, wakati walipotembelea ujenzi huo hivi karibuni, katika eneo la Soga, Pwani.

Muonekano wa Vituo vya Reli hiyo Mpya ya kisasa ya standard Gauge, itakapokamilika.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu Rwanda, Rwakunda Christian, akiteta jambo na maafisa kutoka nchi zinazotumia ukanda wa kati kusafirisha bidhaa zao, wakati wakiangalia ramani ya reli mpya ya kisasa, walipotembelea ujenzi wa reli mpya ya kisasa yastandard gauge,hivi karibuni Mkoani Pwani. Viongozi hao walifurahishwa na maendeleo ya ujenzi huo kwa sababu utarahisisha usafirishaji wa mizigo kwani itapitisha mzigo zaidi na ukubwa wa reli hiyo utaongeza spidi ya treni.(Habari Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Uchukuzi)
[/

Safi sana. endeleeni kukaza buti ili kazi ikamilike kwa wakati na kwa ufanisi. Unaihitaji sana reli hiyo hivi sasa kuliko wakati mwingine wowote
 
Kwa nini isiboreshwe kwanza iliyopo ndo tuwazie huko? Tunakuwa na mambo mengi kwa wakati mmoja mwisho wake atufanyi vizuri kwa kila jambo
 
mkuu hayo si ndio maboresho.. ulitaka waweke lami
 
Hii iliyopo inawashinda huu ni mwezi wa pili haitoi huduma yoyote.. Hapa kazi tu ya Magufuli Kama imedolola hivi.. Maskini Tanzania
 
Safiii.. tujulishwe inaisha lini. Tumechoka na reli ya mkoloni..mafuriko kidogo treni zinakwama.
 
Hicho kinachoitwa "muonekano" tumeshavichoka jamani, tunaletewa mionekano kila siku, mara muonekano wa DART, muonekano wa fly over, muonekano wa kigamboni nk. alafu baadaye vinakua havionekani
mpaka sasa hivi DART haionekani
am sick and tired of mionekano
Mkuu hiyo hisikupe shida, mionekano ya majengo/Stations ni secondary cha muhimu ni ujenzi wa reli - ndiyo hivyo tena mambo safi kabisa picha ya ujenzi wa RELI inaokena wazi wazi hapo - mataluma na ballast fresh kabisa kilicho baki ni kukabidhiwa reli in a recordtime.
 
Kwa ukubwa wa huo mradi mbona hatuambiwi wakandarasi wako wangapiiiiiii? Kuna kujenga vituo na hiyo reli yenyewe kutoka Dar hadi Kigali mkandarasi ni mmoja tu? Hiyo itakamilika baada ya miaka mingapi? Mipango ya vichwa vya treni na mabehewa yake ikoje? Mafunzo kwa wazalendo yatakuwepo? Je NEMC wamepitisha hiyo?
 
Mkuu shikamoo,
nadhani wewe peke yako ndo unaelewa, kuna watu wanakurupuka tu kuandika..
wanazingua wanakulupuka mara wanajenga hiki mara hiki mwishowe wanavitekeleza wekeza sehemu moja nguvu yote mnaamishia huko mpk kinakamilika yaan hata ufatiliaji unakuwa rahisi kujua maendeleo ya mladi
unajua sisi tushazoea kelele ya kitu kimoja mfan ilikuwa muhimbili MRI kelele nyingi leo kimya
ikaja bandalini blahblah kibao inazizima now
bomoabomoa ndo hiyo inapoapoa
U DART haisomeki UDA nayo chalii
yaan mambo lukuki mwishowe vinayeyuka hatusikii tena vinazuka vingine yaan tunageuzwa vikatuni sisi
eeeh BABAMKUBWA ebu panga mambo vizuri yaeleweke kamilisha moja amia jingine ni bora ukamilishe moja lenye maana na halaka zaidi kwa wananchi kuliko kuhangaika na mambo kumi na usikamilishe hta 1 yaa inakuwa tunachelewesha maendeleo kurudishana nyuma
 
Back
Top Bottom