Inawezekana Mengi ana matatizo yake lakini hoja aliyoiwekamezani ina mashiko. Wapo matajiri wengi wasio wazawa nchi hii ambao wameiibiaserikali na wengi bado wanafanya hivyo kwa kukwepa kodi, kwa hiyo Mengialipoanzia na alipo, si exception. Ni ukweli usiopingika kuwa serikali yetutoka uhuru umeipa uwezeshaji wa wazawa kisogo. Wazawa wamekuwa watu wakusindikiza hoja zote za maendeleo huku serikali, labda kwa sababu ya rushwaimekuwa ikikumbatia wageni hata kwenye sekta ambazo hazihitaji wageni. Hakunataifa duniani lililoibuka kutoka kwenyelindi la umaskini linaloendelea kwa kudharau watu wake (nenda India, S.Korea, China,Malaysia, etc). Kwa jinsi ilivyo nashawishika kulinganisha mawazo ya ProfMuhongo na mawazo ya kikoloni, kuwa mtu mweusi hawezi chochote na nashawishikakukubali kuwa hiyo ndiyo sera ya serikali iliyopo madarakani. Nina imaniMtanzania akiwezesha na akapewa fursa ya kufanya anaweza kufanya. Nakumbukawakati wa awamu ya Mkapa kulikuwa na uundaaji wa sera ya Kuwawezesha WananchiKiuchumi. Waandaaji walifanya tafiti nahata kupata uzoefu wa mataifa mengine. Mwisho wa siku, labda kwa sababu yaubinafsi, andiko lile limetupwa kapuni na kwa maoni yangu hata Baraza laUwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) ni kiini macho kwani sioni ilichosaidiampaka sasa. Tumekuwa na uandaaji wa sera ya gesi, labda kwa sababu ya rushwaambayo Prof. Muhongo hakuijua alipokuwa anaingia ofisini, imeitupwa pembeni. Kwamaoni yangu huwezi futa sera na sheria inayoweza kulinda rasilimali ya kizazicha sasa na baadaye kwa kuja na mikataba ambayo mwisho wa siku inawezakubadilika bila hata kuwashirikisha wananchi --- nikimaanisha 75% foreign/25% localownership kwenye visima vya gesi na mafuta na kinyume chake mara baada yamwekezaji wa kigeni kurudisha gharama zake. Hii ni muhimu iwe kwenye sheria nasera na si azimio la rais na baraza lake la mawaziri ambao nadhani upeo waounaweza kuathiriwa na rushwa na ushwawishi wa mapepari kutoka nje.