Elimu ya Tanzania sasa imeingia katika mtizamo wa kimakundi.
Leo ITV wametuonesha mama Salma akiungwa mkono na Mengi kuchangia shule moja, moja tu Bilioni 5. Akimaanisha Milioni 200 kwa Mwaka.
Chanel 10 wao saa 1 wameonesha Lowasa katika harambee ya shule za kata na akatoa Mil 10, na jumla ya pesa yote ni takriban Mil 200 si kwa shule moja, kama 7 hivi za Kigamboni.
Wadau kama nimekosea nisaidieni.
Hoja yangu ni kuwa hivi hiyo shule ya Mama Salma itachukua wakina Kayumba wote tz wafaidi hayo mahela ya Mengi?
Kikwete amemsifia Mengi anahuruma na wa tz, je angezitoa hizo kama madawati kusambaza Tz nzima hiyo huruma si tungeiona?
Mama Salma, tumeona hizo pesa, vp usaili wa watoto wetu kuja shule ya WAWAMA si fomu mtatuuzia Mil 1? Sisi hatuna ela, jiandae tunaleta watoto na pesa ni za Mengi.
Kwako Lowasa...pole kwa kusimama kuchangisha sh mia tano tano hadi kufikia Mil 200..nimeona wananchi wakipita kuchangia.
Hoja ya tatu, nimesubiri ITV mtangaze Lowasa nae kachangisha pesa kusaidia shule za kata kama 7 hivi..labda sikuona. Ni kwa nini wakati ni kawaida yenu.
Enyi Matajiri na Enyi Masikini Mlizaliwa uchi na mtarudi mavumbini uchi.