Regina Lowassa awapa mbinu BAWACHA kuing’oa CCM

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,259
2,000
12143312_544907869018244_4888291860371228965_n-620x308.jpg

BARAZA la wanawake wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAWACHA) wametakiwa kuungana na kuweka mipango mikakati ya nguvu ili kuhakikisha wanaiondoa CCM madarakani katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2020 Kauli hiyo imetolewa leo na Mama Regina Lowassa alipokuwa akizungumza na wanawake wa baraza hilo katika mkutano wao wa kikao cha ndani na kikao cha kazi kilichofanyika mjini Dodoma.

Amesema juhudi za akina mama wa Chadema zilizofanyika katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 zilikuwa na nguvu kubwa hivyo kuna kila sababu ya kuongeza nguvu zaidi ili kuhakikisha akina mama wanagombea nafasi mbalimbali kuanzia ngazi ya tawi hadi taifa.

“Kwa sasa akina mama wenzangu kinachotakiwa ni kushikamana na kuwa na mikakati ya pamoja ili kuhakikisha mapambano ya kuing’oa CCM madarakani yanafanikiwa.

“Hakuna sababu ya kugombana wala kutofautiana ,wala kutegeana katika kufanya kazi, umefika wakati sasa wa kuanza nikakati ya pamoja katika kujenga chama,kujengeana uwezo pamoja na kutokuwa waoga katika kufanya maamuzi.

“Ni ukweli usiopingika katika uchaguzi wa mwaka 2015 CCM ilikuwa na wakati mgumu sana kwani akima mama mlionesha ujasiri mkubwa na mlifanya kazi nzuri na matokeo yake yalionekana,sasa uchaguzi umekwisha ni wakati wa kujipanga na kusonga mbele zaidi ili kuhakikisha CCM inaondoka madarakani ili kuwapa unafuu watanzania ambao wameteseka kwa muda mrefu sasa kutoka na na chama hicho kuwa na mfumo kandamizi” amesema Mama Lowassa.

Naye Halima Mdee, Mwenyekiti wa BAWACHA akifungua kikao cha kazi cha baraza hilo amewataka akina mama kuhakikisha wanafanya kazi kwa ujasiri na kuhakikisha wanapata nafasi mbalimbali katika ngazi za maamuzi.

Mdee ametolea mfano wa mkutano wa baraza kuu la Chadema Taifa na kueleza kuwa katika baraza hilo watoa maamuzi wengi walikuwa wanaume jambo ambalo linaonesha wazi kuwa akina mama wengi hawajitokezi kugombea nafasi mbalimbali za kimaamuzi.

Kutokana na hali hiyo sasa napenda kuwahamasisha wabunge wote wa Viti Maalum, kuhakikisha wanatafuta majimbo na kutafuta nafasi mbalimbali za maamuzi badala ya kuwa na hofu na kujiona kana kwamba zipo nafasi mbalimbali ambazo zinafaa kugombewa na na wanaume na siyo wanawake
 
Ibambasi

JF-Expert Member
Jul 25, 2007
8,527

Mbona hakuweza kumsaidia Mzee Lowassa kuingia ikulu 2015?
 
aliisaac1000

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
388
500
Kuing'oa CCM 2020?

Anaota huyo mama!
Watu wanaongea kama vitu vya mchezo wa kuigiza, mmejipanga vipi kwanza na kwa timu ipi na inaongozwa na nani?, mmekubalika kwa kiwango gani na wananchi wa rika zote, kabila,dini na hata nje ya mipaka? Maana kama hamjapiga mahesabu vizuri mtatwanga maji kwenye kinu kila uchao
 
Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
88,584
2,000
Watu wanaongea kama vitu vya mchezo wa kuigiza, mmejipanga vipi kwanza na kwa timu ipi na inaongozwa na nani?, mmekubalika kwa kiwango gani na wananchi wa rika zote, kabila,dini na hata nje ya mipaka? Maana kama hamjapiga mahesabu vizuri mtatwanga maji kwenye kinu kila uchao
Hawajielewi kabisa hao CHADEMA.
 
MOTOCHINI

JF-Expert Member
Jan 20, 2014
26,145
2,000
Huyu mama kachanganyikiwa sio bure
Chdm ipi yakuiondoa ccm 2020!
Hawa watetea majizi na wapiga dili!
Hilo wasahau
 
MOTOCHINI

JF-Expert Member
Jan 20, 2014
26,145
2,000
Watu wanaongea kama vitu vya mchezo wa kuigiza, mmejipanga vipi kwanza na kwa timu ipi na inaongozwa na nani?, mmekubalika kwa kiwango gani na wananchi wa rika zote, kabila,dini na hata nje ya mipaka? Maana kama hamjapiga mahesabu vizuri mtatwanga maji kwenye kinu kila uchao
Vibendera hao hilo hawalifahamu
Wao mbwembwe na kudanganyana
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom