wambagusta
JF-Expert Member
- Nov 28, 2014
- 2,804
- 2,252
Kiana chotakiwa viwepo vyama viwili tu
BARAZA la wanawake wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAWACHA) wametakiwa kuungana na kuweka mipango mikakati ya nguvu ili kuhakikisha wanaiondoa CCM madarakani katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2020 Kauli hiyo imetolewa leo na Mama Regina Lowassa alipokuwa akizungumza na wanawake wa baraza hilo katika mkutano wao wa kikao cha ndani na kikao cha kazi kilichofanyika mjini Dodoma.
Amesema juhudi za akina mama wa Chadema zilizofanyika katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 zilikuwa na nguvu kubwa hivyo kuna kila sababu ya kuongeza nguvu zaidi ili kuhakikisha akina mama wanagombea nafasi mbalimbali kuanzia ngazi ya tawi hadi taifa.
“Kwa sasa akina mama wenzangu kinachotakiwa ni kushikamana na kuwa na mikakati ya pamoja ili kuhakikisha mapambano ya kuing’oa CCM madarakani yanafanikiwa.
“Hakuna sababu ya kugombana wala kutofautiana ,wala kutegeana katika kufanya kazi, umefika wakati sasa wa kuanza nikakati ya pamoja katika kujenga chama,kujengeana uwezo pamoja na kutokuwa waoga katika kufanya maamuzi.
“Ni ukweli usiopingika katika uchaguzi wa mwaka 2015 CCM ilikuwa na wakati mgumu sana kwani akima mama mlionesha ujasiri mkubwa na mlifanya kazi nzuri na matokeo yake yalionekana,sasa uchaguzi umekwisha ni wakati wa kujipanga na kusonga mbele zaidi ili kuhakikisha CCM inaondoka madarakani ili kuwapa unafuu watanzania ambao wameteseka kwa muda mrefu sasa kutoka na na chama hicho kuwa na mfumo kandamizi” amesema Mama Lowassa.
Naye Halima Mdee, Mwenyekiti wa BAWACHA akifungua kikao cha kazi cha baraza hilo amewataka akina mama kuhakikisha wanafanya kazi kwa ujasiri na kuhakikisha wanapata nafasi mbalimbali katika ngazi za maamuzi.
Mdee ametolea mfano wa mkutano wa baraza kuu la Chadema Taifa na kueleza kuwa katika baraza hilo watoa maamuzi wengi walikuwa wanaume jambo ambalo linaonesha wazi kuwa akina mama wengi hawajitokezi kugombea nafasi mbalimbali za kimaamuzi.
Kutokana na hali hiyo sasa napenda kuwahamasisha wabunge wote wa Viti Maalum, kuhakikisha wanatafuta majimbo na kutafuta nafasi mbalimbali za maamuzi badala ya kuwa na hofu na kujiona kana kwamba zipo nafasi mbalimbali ambazo zinafaa kugombewa na na wanaume na siyo wanawake
Hizo mbinu kwanini asingempa mumewe hadi akapigwa chini na Kikwete dodoma na hatimaye kugalagazwa na Magufuli kwenye uchaguzi mkuu.
Siyo kwa kiwango cha wafuasi wa cdmInawezekana na wewe ni mpuuzi
..sasa na wewe hukuona kuwa Mzee Lowassa alikuwa mgonjwa taabani hawezi kukampeni?
Hahhahàaa haya bana, na wale ambao mikono yao imeota sugu kwa kushangilia wasichokijua bungeni alafu baadae yakiwageuka wanaanza kishangaa tuwaitejeSiyo kwa kiwango cha wafuasi wa cdm
Ngoja nyumbu waone unasema mgombea wao alikuwa mgonjwa taabani.
..Pia hakuna anayefikiria 2020 mgombea wa aina gani awe ndiye mpeperusha bendera wa CDM.
BARAZA la wanawake wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAWACHA) wametakiwa kuungana na kuweka mipango mikakati ya nguvu ili kuhakikisha wanaiondoa CCM madarakani katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2020 Kauli hiyo imetolewa leo na Mama Regina Lowassa alipokuwa akizungumza na wanawake wa baraza hilo katika mkutano wao wa kikao cha ndani na kikao cha kazi kilichofanyika mjini Dodoma.
Amesema juhudi za akina mama wa Chadema zilizofanyika katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 zilikuwa na nguvu kubwa hivyo kuna kila sababu ya kuongeza nguvu zaidi ili kuhakikisha akina mama wanagombea nafasi mbalimbali kuanzia ngazi ya tawi hadi taifa.
“Kwa sasa akina mama wenzangu kinachotakiwa ni kushikamana na kuwa na mikakati ya pamoja ili kuhakikisha mapambano ya kuing’oa CCM madarakani yanafanikiwa.
“Hakuna sababu ya kugombana wala kutofautiana ,wala kutegeana katika kufanya kazi, umefika wakati sasa wa kuanza nikakati ya pamoja katika kujenga chama,kujengeana uwezo pamoja na kutokuwa waoga katika kufanya maamuzi.
“Ni ukweli usiopingika katika uchaguzi wa mwaka 2015 CCM ilikuwa na wakati mgumu sana kwani akima mama mlionesha ujasiri mkubwa na mlifanya kazi nzuri na matokeo yake yalionekana,sasa uchaguzi umekwisha ni wakati wa kujipanga na kusonga mbele zaidi ili kuhakikisha CCM inaondoka madarakani ili kuwapa unafuu watanzania ambao wameteseka kwa muda mrefu sasa kutoka na na chama hicho kuwa na mfumo kandamizi” amesema Mama Lowassa.
Naye Halima Mdee, Mwenyekiti wa BAWACHA akifungua kikao cha kazi cha baraza hilo amewataka akina mama kuhakikisha wanafanya kazi kwa ujasiri na kuhakikisha wanapata nafasi mbalimbali katika ngazi za maamuzi.
Mdee ametolea mfano wa mkutano wa baraza kuu la Chadema Taifa na kueleza kuwa katika baraza hilo watoa maamuzi wengi walikuwa wanaume jambo ambalo linaonesha wazi kuwa akina mama wengi hawajitokezi kugombea nafasi mbalimbali za kimaamuzi.
Kutokana na hali hiyo sasa napenda kuwahamasisha wabunge wote wa Viti Maalum, kuhakikisha wanatafuta majimbo na kutafuta nafasi mbalimbali za maamuzi badala ya kuwa na hofu na kujiona kana kwamba zipo nafasi mbalimbali ambazo zinafaa kugombewa na na wanaume na siyo wanawake
Wa 2020 si ni Lissu, au..?
Tena huyo ni grade oneInawezekana na wewe ni mpuuzi
Haoti kwani hata Magufuli anajua 2015 hakushinda uchaguziKuing'oa CCM 2020?
Anaota huyo mama!
Kuweka mtandao ni jambo chanya sana. Ikumbwe vuguvugu la maendeleo sehemu nyingi duniani huanzishwa na Wanawake. Pia Roma hakujengwa siku moja.Mbona hakuweza kumsaidia Mzee Lowassa kuingia ikulu 2015?
Uishinde ccm? Unaota huku unatembea weweKuweka mtandao ni jambo chanya sana. Ikumbwe vuguvugu la maendeleo sehemu nyingi duniani huanzishwa na Wanawake. Pia Roma hakujengwa siku moja.
Uchanguzi wa 2015 , baada ya kuwa na UKAWA , ilileta changamoto kubwa sana kwa CCM . Hivyo wakiboresha mbinu( ingawa hata CCM nao huenda wakazinduka) wataleta ushindani mkubwa na hata kuweza kushinda uchanguzi wa 2020. Nani ajuaye?
Inawezekana ni wewe unaotaKuing'oa CCM 2020?
Anaota huyo mama!