Redio punguzeni matangazo

Nchi Kavu

JF-Expert Member
Joined
Sep 11, 2010
Posts
4,289
Reaction score
2,472
Ni kweli kwamba matangazo ndio yanawalipa na kuendesha shughuli zingine tatizo matangazo yakizidi sana inakuwa kero hadi wasikilizaji wanahama kituo. Mfano mzuri ni clouds Fm na kipindi cha Power Breakfast.

Wengine ni magic Fm na kipindi chao cha morning magic. Matangazo yamezidi hao wadhamini wanawajazia matangazo na wakija kugundua wasikilizaji wamepungu nao watajipunguza.

Hivyo hasa kipindi cha Morning Magic mjipime
 
Utawalipa Mishahara Yao Wewe? Na Umeonyesha Ni Jinsi Gani Ulivyo Ignorant Katika Masuala Ya Media And Communication Pamoja Na Masuala Mazima Ya Marketing And Advertising.
 
Utawalipa Mishahara Yao Wewe? Na Umeonyesha Ni Jinsi Gani Ulivyo Ignorant Katika Masuala Ya Media And Communication Pamoja Na Masuala Mazima Ya Marketing And Advertising.

i might be ignorant but too much of anything is harmful. kiufupi na wewe huwajui watu
 
i might be ignorant but too much of anything is harmful. kiufupi na wewe huwajui watu

Huwa Nikishatoa Dongo Lazima Likuumize Sana Na Sasa Najua UNALISIKILIZIA. Ungekuwa Siyo Oblivious Kamwe Usingeuliza Swali La KIPOPOMA Kama Hilo Kwa Sisi Great Thinkers Humu. Great Thinkers Huwa HATUPENDI HOJA au MASWALI MEPESI Ambayo Hata Facebook Ungeweza Tu Kujibiwa Kama Umeshindwa Pia Ku Google. Halafu Hapo Na Wewe Unajiita Ni Graduate? Shame On You.
 
Hakuna matangazo yanayoudhi kama ya kondom, hivi watu wazima wanapoyasikiliza wakiwa na watoto wao wanawaambia nini?

Mfano lile la hermet ya bodaboda, yaani aibu mpaka napata woga, sijui watu wamekufa ganzi ya mioyo?
 
unachokisema ni kweli,.. matangazo yakiwa mengi wasikilizaji wanachoka na rate za wasikilizaji zinawezapungua na mwishowe wakaondoa matangazo yao..yani hii huwa ni changamoto kubwa sana ila ni hela, huwezi kuiacha ikaondoka, hiyo hela haihitajiki kwenye mishahara tu, kuna magari (mafuta na service, branding etc), service ya vifaa na mitambo, new equipments, profit etc
 

Everyone is entitled to ask any sort of question or give an opinion..great thinker or not, it's not in your place to choose for him/her what and where to ask
 
Ni sawa uwaambie wenye daladala wasijaze sana abiria kwa kuogopa wengine kushuka
 
Ingawa ni ukweli uliowazi kuwa matangazo ndio yanaendesha vyombo vya habari( ikitegemewa kulipia gharama za uendeshaji) kuna ukweli wa kiasi chake kuwa baadhi ya vyombo vya habari havina mpangilio unaostahili wa matangazo yao ya biashara na alichokieleza mleta mada kinawakwaza wengi.

Ukisililiza RFA kwa mfano na kipindi chao cha matukio, kila baada ya habari moja, linafuata tangazo la biashara au upuuzi mwingine kama miaka 20 ya kuanzishwa, 98.... blabla, haya kwa hakina hayawasaidia wasikilizaji zaidi kwao ni kero tu.

Tunaelewa umuhimu wa kuwa na matangazo kwa ajili ya uendelevu wa vyombo hivyo lakini utaratibu unaotumika kuyapanga unawakwaza w3asikilizaji pamoja na maudhui ya baadhi ya matangazo ni majanga. Matangazo mengi yanapotosha au yanahamasisha vitu visivyokuwa na manufaa kwa umma kama lile la NMB linaloeendelea hivi sasa. Hivi haikuwa sawa kuhamasisha kilimo kwa mfano badala ya kile kinachojaribu kutengenezwa hivi sasa?
 
Mimi Power breakfast ndio kipindi changu bora kipindi cha akina Masoud kipanya lakini walivyoanza kuweka matangazo kila wakati sikutaka kuwasikiliza tena. Kibaya zaidi watangazaji wanatumia mda mwingi kuyasifia hayo matangazo na kutoa maelezo maelefu as if watu hawajasikia tangazo. Matangazo ndio yanahitajika but wangekuwa wanatangaza makampuni machache yakayo weza kuwalipa fedha ya maana
 
Miaka ya nyuma nilikuwa msikilizaji mzr sana wa redio hasa RFA, Kiss FM na Redio One. RFA walikuwa na uwezo wa kuweka matangazo ya biashara kwa dk 5 nzima. Litatoka hili linaingia jingine, baada ya dk 5 tangazo.

Sasa ni zaidi ya miaka 5, ukinikuta nasikiliza redio basi itakuwa ni matangazo ya mpira.

Niliacha kabisa kusikiliza redio.
 
Matangazo yenyewe ya kumtafuta nani yule aliyeko maghorofani Dar....... lakini unakwenda kuulizia Ukerewe! ambako nayeulizwa badala ya kuzungumza kwa lafudhi ya wenyeji wa ukerewe anaongea kama mwenyeji wa Malya!
 
Hii kumbe ni kero kwa watu wengi nilidhani ni mimi peke yangu,

Matangazo kweli ndio yanayolipia gharama zote za uendeshaji wa radio station, lakini yakizidi yanakuwa kero sana,

Bora basi kuwe na mpangilio mzuri wa kuyarusha hewani hayo Matangazo sio yote yanafuatana kama mabehewa ya Treni, inakuwa kero sana,
Mfano wa radio hizo ni radio Tumaini na Wapo radio, hasa kipindi cha asubuhi kutoka magazetini wanarundika Matangazo kwa fujo mpaka inakuwa kero, huwa naamuaga kubadilisha station, nani anataka ujinga!

Wabadirike bwana!
 

ulidhamiria kunijibu au umekosea topic? pia soma hoja za wengine ndio utaelewa zaidi.
 
.

Kutokana na kero za matangazo, watangazaji wenye uelewa duni, ratiba mbovu ya vipindi, ukosefu wa vipindi vya kuelimisha umma ( ukiondoa TBC), ikifika saa 12 asb, 7 mcjhana na 12 jioni vituo vyote kugeuka kuwa minara ya kurusha matangazo ya propaganda ya DW, BBC N.k wengine tunahamia kwenye internet ambayo hawa wenye "vyombo" vya habari hawana taarifa hadi sasa kuwa ni tishio la uwepo wao
 
Mkuu huu ni kweli kabsa, Clouds kipindi chao cha Power Breakfast daaah matangazo Mengi hadi basi, pia pale sasa wanapoanza kusifia hayo matangazo. Halafu wanakuwa wanafaki kisa kusifia matangazo. Mara hakuna simu kama Tecno BOOM, then Huawei P8 ndo yenyewe hakuna zaidi mara Samsung J LTE.
 
hahahahahahahahahahahahahahahahahah

mm ikifika hapo naijianzishia kamada kupoza makali asee, ni aibu
 
Kuna radio moja huku Zenj inaitwa Zenj fm kipindi Chao cha michezo wanapiga matangazo Zaid ya dk 15 mfululizo mbaya Zaid tangazo lenyewe ni Hilo Hilo moja tu watu wanalalamika ila hawasikii
 
Mi hakuna tangazo linalonikera kama la Joti la mzee Mwalubadu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…