Redio Clouds kurudia rudia tangazo la CDM kuna nini?

EasyFit

JF-Expert Member
Jul 4, 2011
1,269
1,082
Nimekuwa nikisiliza hii redio toka alfajiri imekuwa ikitangaza tamko la Mbowe kusitisha maandamano ya Chadema nchi nzima kila baada ya nusu saa kuna nini maana si kawaida, wanasema hii imetokana na mazungumzo yanayoendelea huko Arusha kati ya M/kiti huyo na Kamshina wa makosa ya jinai nchini Kanumba.
 
Hakuna kitu chadema maliza kabisa wewe subiri zitto arudi
Nafikiri Chadema inaifanya serikali hailali maana kwa tamko tu la M/kiti wa Bavicha leo askari wa FFU na askari kanzu wamelala barabarani Kimara-Ubungo.
 
kungekua na maandamano wala wasingetangaza! lobbying za kipuuzi kabisa
 
CLOUDSS??????????HIVI BADO KUNA WATU WANASIKILIZA CLOUDS??AISEE KWELI KAZI IPO,UKOMBOZI WA MTANZANIA NI MGUMU SANA KWA NINI USINUNUE GAZETI UKASOMA AU UKASIKILIZA RADIO NYINGINE KAMA ZA DINI UKAPATA JAPO MAFUNDISHO ILA CLOUUUUUDS??

TOKEA IMEANZISHWA IMEKUWA KIBARAKA WA CHAMA TAWALA NA MAFISADI NA SIKU NCHI HII IKISHIKILIWA NA CHADEMA HATUA ZA AWALI NI KUFUNGIA RADIO STESHENI KAMA HIZI AMBAZO ZIMEJAA VIJANA WANAOUZA ULE MTANDAO WA NUSU SHILINGi
 
kungekua na maandamano wala wasingetangaza! lobbying za kipuuzi kabisa.

Nilishaacha kusikiliza Clouds Fm Radio, Natimiza mwaka sasa. Ni radio ya kinafiki na kizandiki. Wajue kuwa wanaowaita wapinzani na wavunjifu wa amani leo, kesho watajakuwa watawala, sijui wataficha wapi aibu yao. CHUKIA CLAUDZ RADIO.

N
 
Kweli bana radio ya wendawazimu wa Magamba. Tena kama PJ na hana kitu kabisa, anasoma habari ya kusifia Magamba tu. Acha hizo PJ Sengerema haukuwa hivyo. Hizi pesa zipo ndungu fanya kazi tu utapata. Jana unasoma habari ya Slaa kujificha kwenye spika gazeti lenyewe Mtanzania!!!! Magazeti yako Mtanzania, Habari Leo, Uhuru ukijitahidi sana na Dira ya Mtanzania.
Wana JF tuikatae Clouds FM
 
Utasikiliza vp Clouds halafu uchukulie kama ni habari serious? Ni sawa na kusoma gazeti la udaku then uamini kilichoandikwa humo then usimulie watu. Viredio vya kipuuzi kama hicho vipo vingi tu, muwe mnavipotezea.
 
Nimekuwa nikisiliza hii redio toka alfajiri imekuwa ikitangaza tamko la Mbowe kusitisha maandamano ya Chadema nchi nzima kila baada ya nusu saa kuna nini maana si kawaida, wanasema hii imetokana na mazungumzo yanayoendelea huko Arusha kati ya M/kiti huyo na Kamshina wa makosa ya jinai nchini Kanumba.

Serikali ina wasiwasi sana wakuu......
 
Nimekuwa nikisiliza hii redio toka alfajiri imekuwa ikitangaza tamko la Mbowe kusitisha maandamano ya Chadema nchi nzima kila baada ya nusu saa kuna nini maana si kawaida, wanasema hii imetokana na mazungumzo yanayoendelea huko Arusha kati ya M/kiti huyo na Kamshina wa makosa ya jinai nchini Kanumba.
Manumba....
 
Nafikiri Chadema inaifanya serikali hailali maana kwa tamko tu la M/kiti wa Bavicha leo askari wa FFU na askari kanzu wamelala barabarani Kimara-Ubungo.

Wanapata taabu sana CDM inawaendesha sana hawana hamu.
 
Wakitaka tuwasikilize tutakaa mezani tutawasikiliza kama kawaida ya utaratibu wowote wa kistaarabu kwa kuwa wote tunapenda Amani, wakileta upuuzi ama wakikiuka makubaliano tutaendelea na utaratibu wetu wa kuonyesha wazi kupinga unyanyasaji mkubwa kutoka kwa hawa wakoloni weusi tunaoishi nao mitaani kwetu.
 
Nimekuwa nikisiliza hii redio toka alfajiri imekuwa ikitangaza tamko la Mbowe kusitisha maandamano ya Chadema nchi nzima kila baada ya nusu saa kuna nini maana si kawaida, wanasema hii imetokana na mazungumzo yanayoendelea huko Arusha kati ya M/kiti huyo na Kamshina wa makosa ya jinai nchini Kanumba.

Hujui kama lile ni tawi la CCM mkuu? Pale pamejaa wanafiki wanao jidai kujua kila kitu.
 
Sasa mkisema Clouds ni tawi la CCM na JF na yenyewe ni tawi la CDM? Tuacheni ushabiki usiokuwa na manufaa, Mbowe ni kiongozi ameweza kuona yatakayo tokea kama maandamano yatakuwapo, sasa yeye ametoa tamko yasitishwe, Clouds kama chombo cha habari kinawajibika kuwaambia wananchi nini kinaendelea. Na vile kurudia rudia ni kutokana na wasikilizaji wanatofautiana nyakati za usikilizaji wa redio.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom