REDBULL (Namna ilivyoliteka soko la ulaya)

josephdeo

Member
Nov 23, 2015
95
196
Zama za leo kama wewe ni mfuasi wa kuifurahisha nafasi yako kupitia kwenye kumbi za starehi ni wazi uwezi kukosa kinywaji cha Redbull. Hichi ni kinywaji cha nguvu (energy drink) ambacho eneo lolote lile la starehe ulimwenguni uwezi kukikosa wala wahudumu wa sehemu hiyo hawawezi kukwambia kuwa hawakifahamu kinywaji hiki. Pengine unaweza kukuta kimemalizika tu eneo hilo lakini kamwe hakiwezi kukosekana.


Katika ulimwengu wa sasa hakuna kinywaji cha nguvu (energy drink) chenye umaarufu kupita Redbull. Leo tupo katika kizazi ambacho sisi tunatazama umaarufu huu kama mafunzo kwa vinywaji vipya au kwa biashara zingine ambazo zinaendana na hiyo. Kama wasemavyo wanazuoni kuwa ni muhimu kujifunza kila wakati pia sisi leo tunakuletea funzo ambalo unapaswa kujifunza nyuma ya siri ya mafanikio ya kinywaji hiki.


Wakati Redbull wanataka kuingiza bidhaa zao za vinywaji katika soko la ulaya walikutana na upinzani mkubwa kwani kulikuwa na vinywaji vingi ambavyo vilitimiza haja za watumiaji. Ilikuwa ngumu sana kwao kama bidhaa mpya kwenda kushindana na bidhaa kongwe ambazo zilikuwa tayari zimejitangazia utawala. Wataalam wa masoko wakaja na mkakati imara ambao huo ndio sababu ambayo imefanya tuyazungumzie haya.


Shida kubwa ambayo pia ilikuwa sababu ya kwanini kifanyike hichi ni kwasababu kampuni hii ilikuwa changa na pili haikuwa na bajeti kubwa katika kufanya matangazo. Walichokifanya ili kutengeneza mvuto ni kuwa walikuwa wakienda kwenye sehemu ambazo wanahifadhia taka na kujaza makopo tupu ya Redbull. Kila sehemu ambayo ilikuwa na dampo la kuhifadhia taka basi wao kulikuwa wanajaza makopo tupu ya Redbull.


Hali hii ikawafanya wakazi wa ulaya kuanza kuiingiza bidhaa mpya katika vichwa kwa sababu ilionekana inatumika sana. Kila hifadhio la taka kulikuwa na kopo tupu kumaanisha kuwa kuna mtumiaji alitumia na kutupa kopo hapo kumbe haikuwa hivyo bali kampuni yenyewe ndio ilikuwa ikifanya hivyo. Mpaka leo tunaposhuhudia ukubwa wa kinywaji hiki ulimwenguni basi fahamu nyuma yake kuna mpango kazi huo.
 
Hata jamaa wa toothpicks walifanya ujanja ujanja kama huo wao walikuwa wanapeleka kwa wauzaji halafu wanatuma vijana wao wanaenda kuzinunua hivyo wenye maduka wakaona hii dili ikawa wanachukua kwa wingi wanaweka kwenye maduka yao mpaka wateja wakaanza kumiminika kununua kumbe ile ilikuwa janja janja tu maana walikuwa wanaonunua ni wao kwa wao mpaka leo watu wanatumia na ndio maana mpaka leo Pepsi na coca cola ndio vinywaji vinavyoongozwa kwa kuuza ila ndio vinavyoongoza kwa matangazo dunia the psychology of advertising is real wabongo wengi hawajui.

Sent from my SM-N950F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom