Red Mercury

Red Mercury

wana kawaida moja ya kusingizia kuwa mecury inaharibu magari na kuwa safari zake zina mikosi sana. kwa hiyo watakwambia wamekwama njiani hata mwezi. niliuza tv yangu, redio nikawatumia kahela kangu ka akiba kalikobaki mwisho wa siku jamaa hawaonekani. nikaamua kuwafuatilia dodoma NARCO waliponiambia kuwa wamefika lakini wapi..... kumbe chenga tu. Kufika pale wakaniambia mmoja wao kaugua amepelekwa Engusero kwa matibabu. Nikawafuata hukohuko lakini wapi hawapo. Hapo ndo nikajua kuwa nimeingizwa mjini.

Mimi mwanaume interactive. nikapata mwenyeji pale nikakaa kwake siku kadhaa. naye kumbe ndo wale wale wa stori za marupia, kanipampu weeeee, tukazifuata Kibiraashi tanga huko, kufika huko chafu. Tukarudi, nikakutana na mndorobo mmoja akaniambia yeye ana maji (Mercury nyekundu). Nikaanza kudili naye siku zikaende bila mafanikio.


Nakwambia nilitoka kule kama chizi kudadadeki, ukinitazama huwezi nitambua kama mimi ni a UNIVERSITY STUDENT. Tamaa ya mahela ya haraka ni noma wakuuu

Nimecheka sana,, ila pole kijana
 
Back
Top Bottom