Red Devils' dakika 3 za maajabu Nou Camp (Final)

Matanga

JF-Expert Member
Nov 13, 2019
2,281
3,973
.
Mishale ya saa tatu usiku Avenida Diagonal ilipo hoteli ya Gran Melia, siku moja kabla ya fainali wakati Sir Alex Ferguson na Steve McLaren (Kocha Msaidizi) wakiwa wanakuna vichwa nani aanze kikosini, hawana Paul Scholes wala Roy Keane
.
Baada ya kupokea ripoti ya msoma mbinu wao walielekea kwenye chumba cha mkutano, waliitwa wachezaji wote kwa ajili ya maamuzi ya kikosi cha fainali, Fergie alimpanga David Beckham na Nick Butt kama viungo wa kati, watu walistaajabu ila Fergie alimtaka Becks kwa kazi maalum
.
Giggs aliwekwa winga kulia na Jesper Blomqvist kushoto, United bila Henning Berg hapo ila Babu Fergie anacheza karata za hatari mno, Ronny Johnsen aliyetarajiwa acheze Kiungo akapelekwa beki ya kati na Jaap Stam, golini alikaa Schmeichel na kitambaa chake kwenye mechi yake ya mwisho
.
Wakati Babu kashafanya uchaguzi wa kikosi, alicheza na akili ya adui yake Ottmar Hitzfeld alitegemea White ila Babu kaja na Black, inaitwa Tactical Wizard and Prophetic ile pete ya Babu ilikua na Uchawi pamoja na Unabii, Babu kamaliza kazi anasubiri maajabu
.
Alasiri ile ya Mei 26, Mashetani Wekundu wanaagwa hotelini kuelekea Nou Camp ni mwendo wa dakika kadhaa tu, nalikumbuka bus aina ya 'Hyundai Faire' linashika njia, huku bendera za United njiani zinapepea, wanakwambia "The Red Devils and the Famous United" watu washalewa sana hapo
.
Ngoma inaanza kwa presha kubwa mno, United wanafanya makosa Johnsen anamchezea rafu Jancker kilichotokea ni faulo ya Mario Basler wanaingia kambani, United wanapigwa msako mkubwa sana Fergie hajui wapi atazame, Beckham kapotezwa mno eneo la Kiungo
.
Dakika zile tatu za Maajabu baada ya Supersub OGS na Sherringham, namwona Becks kwenye kibendera, dakika ya 90:36 analiachia gozi la mnyama hewani, Teddiee watu kati bado United wanapiga msako wa kufa mtu, United wamecharuka mno
.
Becks nywele zimetimka, Ole Gunnar anakuja pembeni, Nick Butt anawaambia pandeni nitabaki nyuma na Jaap Stam, dakika ya 92:15 ni Becks tena kona, analiachia gozi la Mnyama NIKE Nik Geo 800, Ole Gunnaar kambani 2-1
.
Thats the end of the 1999 Treble, GGMU

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni bahati tu kaka wala sio mbinu, kuna mipira kama miwili iligonga besela la juu kila mtu kaishakubali ni goli Schumichel kaenda kuokota mpira kama nazi iliyoanguka
Ila man u walibebwa na bahati ile siku

bayern waliwazidi kila idara dakika zote za mchezo

ile bayern bhana ilikuwa sio ya mchezo mchezo, ilikuwa na watu haswa man u ilikuwa ulimi nje

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni bahati tu kaka wala sio mbinu, kuna mipira kama miwili iligonga besela la juu kila mtu kaishakubali ni goli Schumichel kaenda kuokota mpira kama nazi iliyoanguka

Sent using Jamii Forums mobile app
Naikumbuka sana ile mkuu nakumbuka aliipiga Mehmet Scholl kiufundi sana.

Bayern walistahili sana kupata ubingwa ila ndo hivo wakati mwingine mpira una matokeo ya kuumiza sana

Machoz aliyotoa Samuel Kuffour usiku ule sizan kama kama hta mama yake mzazi alimlilia namna alivyolia siku ile
 
naikumbuka sana ile mkuu nakumbuka aliipiga Mehmet Scholl kiufundi sana

Bayern walistahili sana kupata ubingwa ila ndo hivo wakati mwingine mpira una matokeo ya kuumiza sana

Machoz aliyotoa Samuel Kuffour usiku ule sizan kama kama hta mama yake mzazi alimlilia namna alivyolia siku ile
Walikuja kuchukua msimu uliofuata,hata hivyo huu mkosi Beyern unawaandama hadi leo kumbuka siku na Chelsea.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Si kweli kwamba ile game Man utd alizidiwa kila kitu ila Bayern alipata clear chances kama tatu hivi mbili za Janker na moja ya Scholl ambazo hazikuzaa matunda angalia statistics za first half na second half halafu utagundua kuwa ile mechi united ndio alikuwa ametawala mchezo licha ya kupata magoli dakika za majeruhi.

20200424_090411.jpg
20200424_090336.jpg
20200424_090311.jpg
 
Tena Buyern walikutana na Man U ambayo aina nyota wake wawili muhimu,Roy keen na Paul Scholes. Ukumbuke kwenye Makundi pia Buyern alikalishwa.
Kilicho wauma Buyern waliweza kuzuia mashambulizi Muda wote wa mchezo, walizuia Vipindi vyote viwili kwa juhudi kubwa sana ila dk 3, yaan dk za Sir Alex hazikuwaacha salama.

Uko sahihi kabisa mkuu sema watu wengi huchangia hoja kutokana na chuki zao dhidi ya United

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Si kweli kwamba ile game Man utd alizidiwa kila kitu ila Bayern alipata clear chances kama tatu hivi mbili za Janker na moja ya Scholl ambazo hazikuzaa matunda angalia statistics za first half na second half halafu utagundua kuwa ile mechi united ndio alikuwa ametawala mchezo licha ya kupata magoli dakika za majeruhi.

Umemaliza kila kitu kiongozi wangu ahsante sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
.
Mishale ya saa tatu usiku Avenida Diagonal ilipo hoteli ya Gran Melia, siku moja kabla ya fainali wakati Sir Alex Ferguson na Steve McLaren (Kocha Msaidizi) wakiwa wanakuna vichwa nani aanze kikosini, hawana Paul Scholes wala Roy Keane
.
Baada ya kupokea ripoti ya msoma mbinu wao walielekea kwenye chumba cha mkutano, waliitwa wachezaji wote kwa ajili ya maamuzi ya kikosi cha fainali, Fergie alimpanga David Beckham na Nick Butt kama viungo wa kati, watu walistaajabu ila Fergie alimtaka Becks kwa kazi maalum
.
Giggs aliwekwa winga kulia na Jesper Blomqvist kushoto, United bila Henning Berg hapo ila Babu Fergie anacheza karata za hatari mno, Ronny Johnsen aliyetarajiwa acheze Kiungo akapelekwa beki ya kati na Jaap Stam, golini alikaa Schmeichel na kitambaa chake kwenye mechi yake ya mwisho
.
Wakati Babu kashafanya uchaguzi wa kikosi, alicheza na akili ya adui yake Ottmar Hitzfeld alitegemea White ila Babu kaja na Black, inaitwa Tactical Wizard and Prophetic ile pete ya Babu ilikua na Uchawi pamoja na Unabii, Babu kamaliza kazi anasubiri maajabu
.
Alasiri ile ya Mei 26, Mashetani Wekundu wanaagwa hotelini kuelekea Nou Camp ni mwendo wa dakika kadhaa tu, nalikumbuka bus aina ya 'Hyundai Faire' linashika njia, huku bendera za United njiani zinapepea, wanakwambia "The Red Devils and the Famous United" watu washalewa sana hapo
.
Ngoma inaanza kwa presha kubwa mno, United wanafanya makosa Johnsen anamchezea rafu Jancker kilichotokea ni faulo ya Mario Basler wanaingia kambani, United wanapigwa msako mkubwa sana Fergie hajui wapi atazame, Beckham kapotezwa mno eneo la Kiungo
.
Dakika zile tatu za Maajabu baada ya Supersub OGS na Sherringham, namwona Becks kwenye kibendera, dakika ya 90:36 analiachia gozi la mnyama hewani, Teddiee watu kati bado United wanapiga msako wa kufa mtu, United wamecharuka mno
.
Becks nywele zimetimka, Ole Gunnar anakuja pembeni, Nick Butt anawaambia pandeni nitabaki nyuma na Jaap Stam, dakika ya 92:15 ni Becks tena kona, analiachia gozi la Mnyama NIKE Nik Geo 800, Ole Gunnaar kambani 2-1
.
Thats the end of the 1999 Treble, GGMU

Sent using Jamii Forums mobile app
Kumbe hawa jamaa mnawapenda sana. Yaani usipomuona wiki na ushee tu mnaumwa.
 
Si kweli kwamba ile game Man utd alizidiwa kila kitu ila Bayern alipata clear chances kama tatu hivi mbili za Janker na moja ya Scholl ambazo hazikuzaa matunda angalia statistics za first half na second half halafu utagundua kuwa ile mechi united ndio alikuwa ametawala mchezo licha ya kupata magoli dakika za majeruhi.

hizi statics hazionyeshi uhalisia wowote wa ile game

kiukweli man u walikuwa dhaifu mnoo kwa bayern acheni kubisha
 
Si kweli kwamba ile game Man utd alizidiwa kila kitu ila Bayern alipata clear chances kama tatu hivi mbili za Janker na moja ya Scholl ambazo hazikuzaa matunda angalia statistics za first half na second half halafu utagundua kuwa ile mechi united ndio alikuwa ametawala mchezo licha ya kupata magoli dakika za majeruhi.

kama mtu anapata clear chances tatu na bado yey ndo anaongoza mechi ina maana kakuweka mfukoni huyo

hizo clear chance ilitakiwa wazipate man u kwa vile walikuwa nyuma so ilikuwa ni lazima wapress ili wasawazishe ila hawakuweza kwa vile bayern walikuwa bora kila sehemu

umetutajia clear chance za janker na scholl hizo za man u ni zipi??kama mechi ilikuwa imembalance??zaidi ya yale magoli ya kindondocha tena ya kona

ila mechi uliingalia kweli wewe au unatazama highlight za you tube????
 
Kuna watu mnaubishi wa kiukoo jamani yaani unabishana na takwimu??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna watu mnaubishi wa kiukoo jamani yaani unabishana na takwimu??

Sent using Jamii Forums mobile app
STATISTICBRAZILGERMANY
Total shots1814
Shots on target810
Ball possession52%48%
Corner kicks75
Fouls committed1114
Offsides30
Yellow cards10
Red cards00

Hizi pia ni takwimu 2014 world cup!!! bila kuambiwa na waliongalia mechi ungeweza kutabiri kwamba brazili walichezea goli 7 katika hii mechi??basi kutokana na hizi takwimu tuambie pia kwamba brazil hawakuzidiwa game ilikuwa 50-50

mkuu yabidi pia ujue kwamba hizi ni karatasi tuu, ila mpira unachezwa uwanjani
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom