Fainali Tatu Kali Zaidi za UCL | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Fainali Tatu Kali Zaidi za UCL

Discussion in 'Sports' started by Observer2010, May 10, 2012.

 1. Observer2010

  Observer2010 Senior Member

  #1
  May 10, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 198
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Niliahidi kuwaletea tathmini ya fainali tatu kali zaidi nilizowahi kuzishuhudia live za UCL kabla ya fainali ya mwaka huu May 19. Hapa naziandika kwa kifupi mno na pia kama kawaida sijazipanga kwa grade, wewe ndiye utakayeamua ipi ni kali zaidi.

  Manchester United vs Bayern Munich 1999


  Hiki kipute kilipigwa ndani ya 98,787 seater stadium, Estadio Camp Nou. Mario Basler anafungua lango la Man U dakika ya 6 kipindi cha kwanza kwa faulo nje kidogo ya 18. Game linakuwa tite sana kwa Man U sababu Bayern walikuwa wanapush mashambulizi makali. Kipindi cha kwanza kinaisha bao ni 1-0. Kipindi cha pili kinaenda mpk dakika ya 90 Man U wako nyuma bao 1. Dakika 3 za nyongeza zinatolewa na refarii Collina. Man u wanapata kona. David Beckham anapiga kona, inatokea piga nikupige, Giggs anapiga shuti dhaifu, Sheringham anasupport mpira unaingia golini na kufanya matokeo yawe 1-1. Mpira unaelekea kuisha, inatokea kona nyingine. David Beckham anapiga kona, Teddy Sheringham anashusha header miguuni mwa Ole Gunar Soskjaer, goli la pili, Man U wanatawazwa ubingwa. Bonge la game.

  Real Madrid vs Bayer Liverkusen 2002

  Mpambano ulifanyika ndani ya Hampden Park, Glasgow. Raul anaipatia Madrid goli dakika ya 8, dakika ya 13 Lucio anaisawazishia Liverkusen goli. Mpira unaendelea kuwa tite kwa pande zote, dakika ya 45, booonge ya goli katika historia ya soka linawekwa kimiani na mmoja kati ya binadamu waliowahi kuonyesha uwezo wa juu kabisa katika ulimwengu wa soka, Zinedine Zidane linafanya matokeo yawe 2-1 kwa Madrid. Dk ya 68, kipa namba moja wa Madrid Cesar anaumia , kijana mdogo wa miaka 21 Iker Casillas anaingia kumbadili, Dk takribani 22 ongeza za ziada zilizobaki zinakuwa ngumu mno kwa huyu kijana, maan Liverkusen walikuwa wanapeleka mashambulizi ya hatari sana. Mpk mpira unaisha, Madrid 2-1 Liverkusen huku Casillas akiwa amefanya kazi ya ziada mnoooo.

  FC Liverpool vs AC Milan 2005

  Huku dunia nzima ya wapenda soka ikijua game lishaisha ndani ya dk 45 za kwanza katika uwanja wa Ataturk Olympic Stadium, Instanbul baada ya goli la captain, Paolo Mardin kabla ya Hernan Crespo kuongeza mawili na kufanya matokeo yawe 3-0. Katika muda wa dk 6 ndani ya kipindi cha pili Liverpool wanapata magoli matatu kuanzia dk ya 54 hadi 60 kupitia kwa Stephen Gerald, Vladimir Smicer na Xabi Alonso, huku Shevchenko akikosa penati. Game inaendelea kuwa ya mashambulizi makali sana kwa Liverpool lakini Dudek anakuwa anafanya kazi ya ziada sana. Dk 90 zinaisha, zinaongezwa 30 mambo yanabaki ni 3-3. Bingwa anaamuliwa kwa penati na Liverpool wanachukua kombe la 5. Moja kati ya fainali kali zaidi katika historia ya UCL huku watu wakiita the Miracle of Instanbul


  Cheerz !!!
   
 2. l

  lycan Senior Member

  #2
  May 11, 2012
  Joined: Apr 28, 2012
  Messages: 171
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  hyo ya liva na ac milan ndo kali
   
 3. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #3
  May 11, 2012
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,790
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  1. Uefa champions league final 1994.
  Ac milan vs barcelona.

  2. Uefa champions league final 2003.
  Juventus vs ac milan.

  3. Uefa champions league final 2007.
  Liverpool vs super pippo filipo inzaghi...
   
Loading...