Usiyoyajua:Haya ndiyo yalikuwa maisha ya David Beckham ndani ya Manchester United (Red devils)

Deadbody

JF-Expert Member
May 30, 2015
4,166
2,000
1550588966314.png


Kutoka siku ya kwanza David Beckham alipopiga mpira kwa miguu yake alionyesha ni mtu bora na mwenye kipaji cha hali ya juu,anaandika Ferguson."Mimi na Beckham tulitandika daruga msimu mmoja huku yeye akiwa ni bora na maarufu zaidi huku akiwa na nafasi ya kufanya mambo mengi kutokana na umaarufu wake "

Alienda PSG kama mimi nilivyoondoka Man United,kwa hiari yangu.


Wengine inabidi utoe kitu fulani kwao kwa nia ya wao kuona ni namna gani wanakipenda kitu hicho.
Kipindi Beckham anaenda America kujiunga na LA Galaxy niliamini anaanza kutambua kuwa sasa ameshindwa katika fani yake ya mpira.Alijitahidi kwa kila hali kurudi katika ubora wake aliokuwa nao alipokuwa nasi(United)

David Beckham hakuwa na machaguo mengi kipindi Real Madrid walipoamua kumuuza kwenda LA Galaxy mwaka 2007.Niliwaza kuwa sasa jicho la Beckham ni Hollywood ambapo niliamini ndio maisha yajayo ya David baada ya kuachana na Soccer.

Hakukuwa na sababu za kimpira wa miguu kwa Beckham kwenda America.Alikuwa anaachana na team ya kiwango cha juu na mechi za kimataifa pia,ingawaje alipigana sana arudi kwenye team ya Taifa ya England.Hii ilinithibitishia pasi na shaka kuwa moyo wa Becks ulikuwa unaanza kuaga career yake ya football.

Alifanya kila kitu kinachowezekana ili kumuweka katika umaarufu wa juu kabisa,ila umaarufu huo nje ya Career yake ya Soka.Kwa siri nikagundua David anajiaandaa kuwa muingizaji wa Hollywood

Kwasababu nilimuona akikua pamoja na Giggs ba Scholes,ila Beckham alikuwa zaidi ya mwanangu ,nilimpenda sana Beckham.Alijiunga United kutokea kwao London july 1991 na ndani ya mwaka mmoja tu alifanikiwa kujiunga kikosi cha mauaji cha mwaka 92 ambacho kwangu ndio kikosi bora kabisa kuwahi kukishuhudia kwenye ulimwangu wa mpira wa miguu,ni kikosi kilichoshinda FA Youth Cup kukiwa na vipaji kama Gary Neville ,Nick Butt na Ryan Giggs.Amecheza mechi 394 na kufunga magoli 85.

Goal alilofunga dhidi ya FC Wimbledon katikati ya uwanja ndio goal lililomtambulisha duniani na wote kufahamu kuwa man united kuna kipaji kinaitwa David Beckham.


1550587854467.png

1996


Kipindi naachana na ukocha Manchester United ,may 2013 ,Giggs na Scholes walikuwa bado wapo nasi.Jumatano 18 june 2003 tulitangaza kuwa tutaingia mazungumzo na Real Madrid kwa Uhamisho wa £24.5 million kumuuza David ambaye kwa wakati huo alikuwa na miaka 28.Habari zilisambaa dunia nzima.Sikuwa na kinyongo tena na Beckham ,nilimpenda sana.Nafifiri ni kijana wa kipekee kwangu lakini huwezi kukubali kushindwa kitu ambacho upo vizuri nacho hata siku moja hivyo nikaamua kumuuza David kwa kile nachokiamini.

David alikuwa mchezaji pekee niliyemuongoza aliyechagua kuwa maarufu ,ambaye aliamua na kuweka kuwa maarufu nje ya football.Rooney alikuwa kwenye rada kufuata nyayo za Beckham ambaye niliwahi mapema kumbadilisha.

Beckham alikuwa anaingiza mara mbili nje ya football kuliko kile tulichokuwa tunamlipa sisi.Maisha hayo yalikuwa yanamtaka sana Giggs lakini hakuyahitaji kabisa ila kwa Beckham ndio ilikuwa kila kitu kwake

Uwezo wa David kufanya kazi nasi ukapungua na akawa hajitumia kabisa uwanja kwenye mechi na hata kwenye mazoezi yetu.Wakati hayo yakiendelea nikawa nasikia tetesi huko nje kuwa Beckham yupo kwenye mazungumzo na Real Madrid

The confrontation between us that caused so much excitement around the game was an FA Cup
fifth-round tie against Arsenal at Old Trafford in February 2003, which we lost 2–0.

Kutoelewana kwetu sisi na Beckham kuliibuka kwenye mechi ya FA Round ya 5 uwanjani Old Trafford Feb 2003 ambapo tulipoteza mchezo kwa kufungwa 2-0 na Arsenal.


Kosa la David kwenye mechi ile ni kitendo cha yeye kuamua kuwa mzururaji tu uwanjani.Mchezaji wa Arsenal angeweza kuzuiwa na Beckham na kushindwa kufunga goal la 2 lilifanya kuwa nyuma 2-0.Beckham alikuwa anamfukuzia kwa nyuma huku mchezaji wa Arsenal Sylvain Wiltord akienda kufunga.Beckham alikuwa ana jogi na sio kumzuia adui,kwa namna nyingine ni kuwa beckham alikuwa anajogi na mchezaji wa Arsenal.

Nilianza kuamini tetesi nilizozisikia kuwa Beckham anampango wa kuhamia Real Madrid hivyo sasa ana cha kupoteza kwetu hivyo anafanya anachojisikia yeye.
1550590371632.png


Tulipoenda Vyumba vya kubadilishia nguo nikajikuta nipo umbali wa futi 12 tu kutoka alipo Beckham na kati yetu kulikuwa na viatu vingi na nikainuka kumfuata alipo na kupiga teke vuti lililokuwa kati yetu na kumpiga juu ya jicho lak.Aliinuka na kunifuata kwa hasira kunipiga na kwa bahati nzuri wachezaji wengine wakamuwahi na kumtuliza.Nikamwambia ,"Beckham kaa chini,umeiangusha timu ,hata ukibisha ila umeiangusha timu na goli la pili ni uzembe wako"

Siku iliyofuata nikamuita ofisi ili tupitie video ya uzembe aliofanya na bado hakukubali kosa alilofanya,alipokuwa amekaa akinisikiliza hakuongea kitu chochote ,alikuwa ananisikiliza tu na nilipomaliza aliinuka na kuondoka huku akiwa hajasema neno lolote.

Wakati anainuka anaondoka nikamuuliza,"David unaelewa nachokwambia ?" hakujibu na kuondoka zake,nikashuhudia kwa macho yangu David akitokomea

Siku iliyofuata stori nzima ikawa hewani kwenye magazeti na vyombo vyote vya habari,Mwandishi Alice ali-highlight juu ya jicho la David nilipomuumiza na buti na kuifanya habari ya kitaifa na ndio siku hizo hizo nikwaambia bodi kuwa Beckham anatakiwa kuuzwa.Dakika ambayo mchezaji wa machester anapojiona ni mkubwa kuliko meneja anatakiwa kuruhusiwa kuondoka , Nilirudia kusema kuwa ,siku ambayo meneja atapoteza mamlaka huna klabu.

Na hapo ndipo wachezaji watakapoongoza team

David alijiona yeye ni bora na mkubwa kuliko Alex FergusonBaada ya kumaliza top kwenye group letu la UCL tukapangwa dhidi ya Real Madrid.Tulipoenda Spain tulifungwa 3-1 huku Beckham akiwa na furaha na kupeana mkono na Roberto Carlos,beki wa kushoto wa Real Madrid.Jumamosi iliyofuata Beckham alijitoa kwenye team kwenye mechi dhidi ya Newcastle kwa kisingizio kuwa hayupo fit.Nikamchezesha Ole Gunnar Solskjaer ambaye alikuwa mwiba wa kuotea mbali siku hiyo na tukashinda 6-2,alikaa jukwaani akitazama.

Kiwango cha Beckham hakikuwa vizuri kiasi cha kunifanya kumuweka Soskjaer nje mechi ya marudiano dhidi ya Real Madrid,nilimuita David ofisini nikamwambia ,"nitamuanzisha Solskjaer ",aliguna kwa dharau na akaondoka zake.

Siku ya mechi ilipofika David nikamuweka Benchi na kumuanzisha Solskjaer mpaka dakika ya 63 ndipo nilipomtoa Veron akaingia David na alifanya tukio lililoonyesha kuwa anaaga rasmi mashabiki.Alifunga free-kick dakika 85 ambayo ilithibitisha kuwa sasa ni mwisho wa Beckham OLD TRAFFORD.Tulishinda 4-3 na kutolewa


Mechi na Real Madrid ni ishara tosha kabisa kuwa sasa David anawaaga mashabiki kiana na hakukuwa na kwere yoyote kuwa alikuwa ananitupia madongo mimi.Kuelekea madrid kuliongezeka kasi ,kwa kile tulichokiona mbele ya macho yetu ,ni kwamba kulikuwa na mazungumzo kati ya agent wake na Real Madrid.

Siku moja May nilipigiwa simu na mkurugenzi wetu Peter Kenyon na kuniambia "Nimepigiwa simu na Real Madrid"

Nikajibu , "vizuri,tulitegemea hivyo".Kwa kipindi hiko tulitegemea kupata £25 million.Nilisafiri na kuelekea Ufaransa kwa ajili ya mapumziko ,na Peter akanipigia simu kipindi nipo kwenye mgahawa napata chakula cha jioni na Jim Sheridan,director wa filamu ambaye alikuwa anaishi hapo nilipokuwa nakula,nikapokea simu ya peter na kumjibu kuwa "Haondoki bila £25 million"


David hakutokea kwenye team kabisa.Tulishinda 4-1 dhidi ya Charlton Old Trafford siku ya May 3,2003.Kwenye mechi ile Beckham alifunga na siku 8 baadae tulicheza na Everton na tulishinda 2-1 na kuwa mabingwa.Kwenye mechi hii ya mwisho dhidi ya Everton ,David alifunga kwa faulo umbali wa Yards 20 na ilitosha kabisa kuaga kuwa sasa ndio bye bye ya kuonana.

Labda naweza kusema kuwa David alikuwa hajapevuka vya kutosha kumudu kila kitu kwenye maisha yake.Saivi anaonekana anayamudu sana,naweza sema alikuwa hajakua.

Kwa mfano ,sitasahau siku hii niliwasili kwenye uwanja wa mazoezi Carrington saa 9 alasili na nilishangaa kukutana na watu wengi sana wamejipanga njiani kuelekea uwanjani hapo.Nikauliza "hivi leo kuna nini hapa" nikajibu "David Beckham atazindua style yake mpya ya nywele leo"


Mara namuona David akiwa na mzura ,ata wakati wa chakula cha usiku bado alikuwa ameuvaa mzura wake,"David vua mzura wako ,tupo kwenye mgahawa saivi",nilisema. Alikataakuvua, nikasisitiza "USIWE MPUMBAVU ,NITAKUTOA KWENYE TEAM SASA HIVI".Bado hakutoa

Siku iliyofuata wachezaji walikuwa wanaenda kupasha mwili kujiandaa na mechi inayokuja huku David akiwa amevaa mzura wake,nikamwambia "hautaenda kokote leo na mzura wako","hautacheza","nitakutoa katika team sasa hivi"


1550825660652.png


Itaendelea
 

Attachments

 • 1550587784589.png
  File size
  100 KB
  Views
  76
 • 1550589025905.png
  File size
  787.4 KB
  Views
  67

Don Clericuzio

JF-Expert Member
Dec 8, 2017
15,492
2,000
Pia baada ya Beckham kumwoa Victoria nadhani ndipo hapo jamaa umaarufu ulizidi zaidi. Na kuna habari kwamba kwa ushawishi wa Victoria kesi ilifunguliwa mahakani kuhusu issue ya kiatu, ila ilikuwa settled nje ya mahakama.
 

zipompa

JF-Expert Member
Aug 19, 2014
6,079
2,000
fergie nae alikuwa mtata,naona zahera nae kafata nyayo. lazima nidhamu iwepo kwenye timu
 

kijani11

JF-Expert Member
Jan 19, 2014
6,362
2,000
Duh miaka inakimbia yaani kumbe huu mgogoro wa Fergie na Beckham ulikuwa 2003, waweza dhani ilikuwa baada ya 2010
 

Chief-Mkwawa

Platinum Member
May 25, 2011
23,072
2,000
Fergie alipenda sana kukuza mambo,anaonekana alikuwa na mambo ya kizee sana.
Nidhamu, hakuna timu duniani inayopata mafanikio ya moja kwa moja bila nidhamu. Miaka yake yote Fergie Man u ilikuwa ikigombania ubingwa, Hata kama timu nyengine itachukua ubingwa basi Man u inakuwa ni timu iliofukuzia huo ubingwa.

Unapoacha mchezaji awe mkubwa kuliko Timu unaua lengo zima la kuitwa team. Ndio maana club kama chelsea haina consistency, mwaka huu inabeba kombe na mwaka unaoumfuatia hata top 4 haipo.
 

ze-dudu

JF-Expert Member
Jul 26, 2014
11,774
2,000
Nidhamu, hakuna timu duniani inayopata mafanikio ya moja kwa moja bila nidhamu. Miaka yake yote Fergie Man u ilikuwa ikigombania ubingwa, Hata kama timu nyengine itachukua ubingwa basi Man u inakuwa ni timu iliofukuzia huo ubingwa.

Unapoacha mchezaji awe mkubwa kuliko Timu unaua lengo zima la kuitwa team. Ndio maana club kama chelsea haina consistency, mwaka huu inabeba kombe na mwaka unaoumfuatia hata top 4 haipo.
Pogba afukuzwe
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom