Mimi ni miongoni mwa watu wasioiamini video iliyowekwa humu jamvini kuhusu Rwakatale. Naona video hiyo imetengenezwa kwa lengo la kuwabebesha CHADEMA mzigo wa laana na shutuma za mauaji walionao polisi machoni mwa jamii ya Watanzania. Pia video hiyo ni kama sinema ya Babu wa Loliondo kuibuka katika mijadala muhimu ya kitaifa. CHADEMA wametangaza maandamano tarehe 25 March mwaka huu kutaka Waziri wa Elimu ajiuzulu.Polisi wanataka kuwapotezea muda CHADEMA kujadili swala la Rwakatale na kusahau Maandamano hayo na mambo mengine muhimu.
Pia Polisi wanataka Wananchi waogope kushiriki shughuli za CHADEMA kwa hofu kuwa wataweza kufa au kupatwa na Madhara. Wasahahau hoja za msingi kwa sasa na kujadili mambo haya ya kutunga na uzushi mtupu.
Kwa maoni yangu kitengo cha ulinzi cha CHADEMA kinapaswa kuwa imara zaidi ya hata ambavyo propaganda ile ya video inataka kutuaminisha. Lazima Chama kiwe na ulinzi mkali kiasi cha wasaliti, Mashushu wa ndani na wa nje kukiogopa. Hoja ya Pingu, Spray dawa ya Usingizi sio kitu cha ajabu matumizi yake kujadiliwa na mtu yoyote anayewaza habari ya usalama wake binafsi au wa taasis ndio maana watu wanamiliki mpaka bastola. Spray, pingu, mapanga, mikia ya taa nasikia vinauzwa hata pale katika duka la Jeshi Lugalo. (Mtakumbuka hata Jery Muro alikuwa na Pingu anamiliki na ameshinda kesi). Ni silaha za kawaida za mtu anayezungumzia usalama wake au wa taasisi yoyote. Wapo Madereva wa Magari makubwa yanayoenda nchi jirani pia nao wanamili vitu hivyo kwa usalama wao wawapo njiani.
Nitashangaa sana kwa Chama kama CHADEMA ambacho watu wengi wamefilisika kwa ajili yake, wengine wako jela na mahabusu, wengine wameachika katika ndoa zao, wengine wamefukuzwa vyuoni, wengine wameuawa kikatili na polisi na katika kampeni mbalimbali kwa ajili ya Chama chao halafu kiwachekee watu wanaosaliti sucrifices zote hizo eti kwa sababu tu kitaonekana ni chama cha watekaji au eti kwa sababu anayehusika na kusaliti jitihada zote hizo ni mwandishi wa habari, kiongozi au mtu mwingine awaye yoyote. Nitashangaa sana
Red Brigade ya Chadema kama ilivyo greegard na vikosi vya ulinzi vya vyama vyote vinavyokaribia kushika au vilivyoshika dola duniani lazima ilinde kujitolea kwa watu, damu za wanaharakati zilizomwagika kwa ajili ya Chama bila kujali nani anahusika kutaka kudharau na kupuuza harakati na thamani za kujitolea kwa watu wote hao kuanzia waasis na wengineo. Red Brigade inapaswa kuwa tishio mpaka kwa Polisi wenyewe na Usalama wa Taifa. Ifike mahali wanapotaka kufanya kitu kinyume na sheria au kwa lengo la kukidhorotesha Chama wawaze mara mbilimbili.
Binafsi nilishangaa kuona vijana wanatukana viongozi wakuu wa Chama hadharani, kuna watu wanaweza kuwa hata wanaingia makao makuu ya Chama bila hofu yoyote kwa lengo la ushushu na usaliti. Lazima Red Brigade iimarishwe hasa wakati huu CHADEMA inapoelekea kuchukua dola ili yoyote asiye na mapenzi mema na Chama ajiulize mara mbili au tatu kuhusu usalama wake pindi akibainika na mifumo ya ulinzi na usalama na intelijensia ya Chama. Hayo ni maoni yangu.