[FONT=lucida grande, tahoma, verdana, arial, sans-serif][/FONT]Ndugu zangu,
Baada ya tamko la Tendwa kuhusu CHADEMA, nimefikiria mambo mengi sana. Lakini kubwa kubwa kuliko yote ni kwamba hawa wenzetu, wakiwemo polisi, rais, Mwigulu, viongozi wengine wa CCM pamoja na Tendwa mwenyewe wanachanganyikiwa na hili jina la Red Brigade.
Maana ukiangalia malengo yaliyosemwa na CHADEMA yanayopelekea kuboreshwa kwa red brigade, hayana tofauti kabisa na malengo ya CCM ya kuwa na green guards.
CHADEMA wanasema wanaiboresha red brigade ili kuimalisha ulinzi wa chama. CCM nao wana kikundi cha ulinzi wa kijani (green guards) kwa ajili ya kuboresha ulinzi wa chama. Ni uhuni kutudanganya kwamba eti green guards ni kikundi cha ujasiliamali. Tangu lini vikundi vya kijasiliamali vinapewa majina ya ulinzi? Au tafsiri ya kiswahili ya neno green guard ni ujasiliamali wa kijani? CCM wasitake kutudanganya hapa. Green guard ni kikundi cha ulinzi wa chama kama aambavyo Red brigade kilivyo.
Sasa kama sheria za nchi haziruhusu vyama vya siasa kuwa na vikundi vya ulinzi, je ni sheria gani imeiruhusu CCM kuwa nacho? Au sheria za nchi hivi sasa ni selective? Kwamba sheria moja hiyo hiyo inawahusu hawa na wengine haiwahusu? Kama Mzee Tendwa anasimamia misingi na sheria za nchi, ni kwa vipi hajaona kwamba CCM wana kikosi cha ulinzi kinachoitwa green guard, na kwamba CHADEMA pia wanakiboresha kikosi kama hicho? Je mzee Tendwa hajui kama kikundi kama hicho CUF pia wanacho na wanakiita blue guard?
Hapa ndipo ninasema inawezekana tatizo ni jina. Maana CUF ambao wana blue guard hakuna anayewauliza. CCM wana green guard hakuna anayewauliza. Basi CHADEMA nao wabadilishe jina la kikundi chao na kukiita red guards. Labda kinachowasumbua hawa wakubwa ni jina hilo la red brigade.
Lakini mwisho naweza kusema, kama Tendwa angekuwa ni mtu mwenye busara ya kutosha basi badala ya kutoa tamko kama hili ambalo linamdhalilisha, basi angewaita viongozi wote wa vyama vya siasa na kujadiliana nao kuhusiana na suala zima la ulinzi wa vyama vyao. Hoja ya kwamba CHADEMA waende polisi haina mshiko, kwa kuwa CHADEMA wamekuwa wakireport matukio haya kila wakati na hakuna hatua yoyote inayochukuliwa. Tendwa anajua kabisa kwamba wakati wa uchaguzi kule Igunga Kada wa CHADEMA aliuwa na green guard. Kwnini hakutishia kuifuta CCM?
Kumekuwa na matukio mengine mengi yenye mashaka ambayo CHADEMA wameyapigia kelele, yakiwemo makambi ya mafunzo ya green guards, lakini Tendwa hakuwahi hata kuyakemea. Lakini hili la CHADEMA anaibuka na kauli nzito. Hii ina maana gani? Kwanini anafanya kazi kwa double standards za namna hiyo?
KUNA HAJA YA CHADEMA KUFIKIRIA KUBADILI JINA LA KIKUNDI CHAKE LABDA JINA NDIYO LINALOMCHANGANYA TENDWA NA VIONGOZI WENGINE WA SERIKALI.[FONT=lucida grande, tahoma, verdana, arial, sans-serif]
[/FONT]