Record za utendaji wa Edward Lowassa zinashangaza sana

Record za utendaji wa Edward Lowassa zinashangaza sana

TeamLowassa

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2013
Posts
1,495
Reaction score
937
Edward Lowassa ndio waziri mkuu aliewai kukaa katika kiti cha uwaziri mkuu kwa muda mfupi zaidi kuliko waziri mkuu yeyote yule; sasa angalia hii record yake ya kushangaza!!!!

One,
Ndani ya muda mfupi sana alionyesha nia ya dhati kukabiliana na foleni ya jiji la dsm; ambalo kimsingi ni kama jinamizi kwa sasa!!!!

Two,
Ndani ya muda mfupi sana alionyesha kukabiliana na tatizo la ajira kwa vijana. Pale Bandarini kulikuwa na watu waliokuwa vibarua kwa muda wa zaidi ya miaka 15 lakini alipoingia uwaziri mkuu, ile hali kaisimamia jamaa wale wakapa mkataba wa kudumu.

Three,
Ndani ya muda mfupi alionyesha kujali elimu kwa wananchi. Hizi shule za kata ambazo ndizo zinazosaidia wananchi kuamka kwa sasa ni matunda ya Lowassa.

Four,
Tatizo la mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu. Akiwa bungeni mara nyingi amekuwa akiongelea suala hili la mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu kiasi kwamba ilibaki kidogo tu ingekuwa malalamiko ya mikopo kwa wanafunzi ingekuwa historia.

Five,
Wakati akiwa waziri mkuu, kwa muda mfupi sana ilionekana kuwa uchumi sasa utapaa; na tayari kulikuwa na indicators za kutosha kuashiria hilo

Six,
Kwa muda mfupi sana utendaji serikalini ulikuwa unaenda kwa kasi ya ajabu. Kuanzia mdogo hadi mkubwa.

Seven,
Kwa muda aliokaa hajawahi hata mara moja kutoa kauli tata za kuashiria ubabe kwa wale wanaopingana naye. Kauli zake siku zote zimekuwa very straight kuwakabili watumishi wazembe na watendaji wanaotenda kazi katika mfumo wa business as usual.

Eight,
Ndio kiongozi pekee serikalini ambae ana record ya kutoa individual support kwa mwananchi mmoja mmoja pale atakapobaini kuwa panahitajika support kwa ajili ya huyo mwananchi. Hata bbc swahili walishawahi kuripoti kuhusu hili.

Nine,
Akiwa waziri mkuu alimbeba sana Kikwete kwenye utendaji wa kiserikali! Hadi sasa Kikwete amekata tamaa kabisa na mambo ya serikali. Anatamani siku anarudi toka maryland akute tayari 2015 imefika maana hana hamu kabisa na mwenendo wa mambo ndani ta taifa hili.

Ten,
Kikwete hatakaa amsahau kwa kumpoteza katika utendaji wa serikali yake. Na ndo maana uchaguzi wa 2010 Kikwete alipata shida sana! Na hadi leo anamlilia sana, ila mfumo wa chama chake unamgandamuiza sana.

etc,


HAYA SASA
Kuna waliokaa kwa muda waliokaa waliishia kuwaambia wafanyabiashara ukitaka mambo yako yawe mazuri jiunge na ccm!!!

Kuna waliokaa kwa kipindi walichokaa lakini kwa muda mfupi sana walionekana mara kidume kinalia bungeni, mara katoa kauli tata za kuwatisha wapinzani; eti wapigwe tu. Uwapige wapinzani ili iweje?

Hii nchi ya kwako peke yako?

Ahsanteni wakuu
 
hatujakataa ila ccm watampa nafasi ya kugombea......?
 
Eleven,

Alithubutu kuhoji uhalali wa matumizi ya maji ya ziwa Victoria na kupelekea kutengua mkataba wa muda mrefu uliokuwepo wa matumizi ya maji kwa nchi ya Misri,hivi leo watanzania wa mikoa ya kaskazini wanatumia maji hayo kitu ambacho ilikuwa ni ndoto!
 
Hii rekodi haiwezi kupingika wala kufutika.
Tatizo ni jee CCM magamba watamuweka kwenye list ya wagombea?
 
Safi sana comrade.........Tusisahau ni lowassa alipeleka maji Shinyanga, aliwafukuza wahindi wavamizi katika kiwanja cha mnazi moja, aliwafukuza wahindi wavamiza katika kiwanja cha PPF tower, Alifanya wakurugenzi na wakuu wa wilaya wawajibike.......Kwa kifupi Lowassa ni kama mvua ya mawe
 
hatujakataa ila ccm watampa nafasi ya kugombea......?
Mkuu kwa hilo usiwe na shaka hata JK CC na kamati ya maadili walimkataa wakina Sozigwa waliandika kitabu kizima kumzuia ila at the end alitoboa.......Naomba kukuondoa wasiwasi katika hilo mkuu
 
Mkuu kama umeamua kumkampenia Lowassa unafanya vyema.

Ila Kwanini unamkejeli Rais aliye madarakani?

Hakuna mantiki yeyote ya kufanya hivyo.
 
Safi sana comrade.........Tusisahau ni lowassa alipeleka maji Shinyanga, aliwafukuza wahindi wavamizi katika kiwanja cha mnazi moja, aliwafukuza wahindi wavamiza katika kiwanja cha PPF tower, Alifanya wakurugenzi na wakuu wa wilaya wawajibike.......Kwa kifupi Lowassa ni kama mvua ya mawe

mkuu I salute you. watanzania wanampenda huyu mtu Wa watu lowasa. watanzania wana imani naye

cc: msalani
 
Ulichokisema lazima kiwe kinapimika(Should be measurable) , hebu tuambie tunapimaje namba 4, 5, 6, 7, 8, 9, 10.
 
Eleven,

Alithubutu kuhoji uhalali wa matumizi ya maji ya ziwa Victoria na kupelekea kutengua mkataba wa muda mrefu uliokuwepo wa matumizi ya maji kwa nchi ya Misri,hivi leo watanzania wa mikoa ya kaskazini wanatumia maji hayo kitu ambacho ilikuwa ni ndoto!
team LOWASSA vs team SLAA kazi kwenu. Wote wa Kaskazini.
 
Ndiyo waziri mkuu, aliejilimbikizia mali nyingi na kukumbwa na kashifa ya ufisadi ya richmond, asee m nkiwaza hako ka kipengere naishiwa hamu na huyu jamaa.
 
Ndiyo waziri mkuu, aliejilimbikizia mali nyingi na kukumbwa na kashifa ya ufisadi ya richmond, asee m nkiwaza hako ka kipengere naishiwa hamu na huyu jamaa.

Sijajua hasa hasa wanaompigia chapuo LOWASSA wanasukumwa na nini, kweli hata mimi nikikumbuka RICHARDMONDULI sithamani tena kumuona akiwa hata balozi wa shina.
 
katika kipindi kifupi aliweka historia ya waziri mkuu fisadi kuliko wote na ndio waziri mkuu pekee aliwahi kujiuzuru kwa wizi
 
Hivi wale RICHMOND wangekuwa bado wanalipwa ule mlungula, si Watanzania tungeshakufa wote? hili hatulifikirii?

Kwani alivyojibu kwenye kamati kuu ya chama kule dodoma hukusoma umeona kama wanamsema tena kina nape na chiligati.ile ngoma sio yake yeye mbuzi wa kafara tu
 
Hivyo vyote viini macho. Ukitaka kulikamata jibwa zururaji (sawa na wapumbavu), likija kwako siku ya kwanza unalitupia vipande vya nyama, siku ya pili likija unalitupia tena vipande vya nyama, likija siku ya tatu unalitupia tena, litazoea kuja. Siku ya nne unalikamata unalipa kipigo. Yote haya yanafanyika ndani ya wiki (siku 7) kati ya siku 365 za mwaka. Huyu ndugu alitupatupa vinyama, wapumbavu wakaingia kichwa kichwa na kumuona anafaa. Je huyu Lowassa ni Kwa nini aliachia kiti cha uwaziri mkuu ndani ya muda mfupi kuliko waziri yeyote yule wa Tz?? Msisahau hilo.
 
Usitaje mazuri tu taja na mapungufu yake sisi tumjadili. Wakati alipokuwa wizara ya ardhi, maji nk.
 
Back
Top Bottom