niwaulize tena hivi chek namba inaishia wapi?maana mfano mimi mwalimu nina chek namba nikaenda kuomba kazi kwa agency za serikali mfano tanesco,tra je bado chek namba itasoma kwa tanesco kwamba nimeshaajiriwa hii chek namba kwa serikali wapi haipo.
Ni kwamba ukiomba kazi kupitia tume ya ajira ukapata wao watakupa barua ya kuwa umepata kazi kwenye idara fulani ambayo ndo itakamilisha taratibu za ajira yako. Sasa wewe utaandika barua ukimuadress katibu mkuu utumishi kupitia kwa mwajiri wako, km ni ticha barua itapitia kwa mkuu shulu, afsa elimu then mkurugenzi uliomba kuhamisha taarifa zako binafsi kutoka huko kwenda mwajiri mpya. Barua ikiwa tayari km uko dar peleka mwenyewe utumishi kule mitaa ya feri then taarifa zako zitapelekwa kwa mwajiri mpya ukiendelea kutumia cheque namba ileile ya zamani.
Porojo tu hapa ,hii kitu ni shida,kuna maafisa utumishi wazembe sana,lkn ukweli kama ulienda kusoma kitu ambacho hakiendani na ajira yako ya awali itakula kwako .ni kama mjumbe mmoja hapo juu alivyosema kuwa inategemeana na ikama ktk eneo husika.
Hata barua hujui kuandika then (unajiita) degree holder? Unawaabisha wenzio.
Hicho cheti ulichoombea kazi ni chako? Maana kuna mdada * F4 failure* ameajiriwa ualimu kwa kutumia cheti cha dada yake aliyefaulu na kuendelea na High school.
kwa hyo vyote vyote inawezekana kuandika barua ukiwa kazini kuomba kufanyiwa recätegorization au kupga interview na ukipata unapeleka barua kwa ktb mkuu ndugu?
Yes yote yanawezekana, andika barua kwa mwajiri wako ukiomba ufanyiwe recategorization kama kutakuw na nafasi huku ukiendelea kuomba kazi sehemu zingine. Kokote utakako tangulia kufanikiwa ndo utaenda.
Aisee, hii nimeielewa vyema, kumbe sio dili kabisaUnawasilisha cheti kwa mwajiri kuthibitisha umequalify kuwa afisa ugavi, unaomba kubadilisha kazi kuwa afisa ugavi. Mwajiri wako kama ana nafasi hiyo ana HR wako ana roho safi utabadilishwa. ila mshahara na cheo ni entry point. 3mil yako ualimu sahau na hakuna personal salary! utaanza kupanda huko kwenye fani mpya
Sio mambo mzazi! Umepiga kazi miaka kibao unaacha mavumba kisa status.Aisee, hii nimeielewa vyema, kumbe sio dili kabisa
Recategorization Hufanyiwa Mtumishi Ambaye Amejiendeleza Na Kupata Sifa Ya Kuingilia Ktk Kazi Husika, Mfano Mwalimu Akijiendeleza Kwenye Uhasibu/ Kilimo Ngazi Ya Shahada, Anaweza Kubadilishwa Kuwa Muhasibu/ Afisa Kilimo Na Kuanza Na Mshahara Wa Cheo Kipya Hata Kama Alikuwa TGTS F Kama Ni Uhasibu Ataanza Na TGS D,kwa Nilivyokuelewa Wewe Ni Mwalimu Na Huhitaji Kufanyiwa Recateg, Kama Unapenda Kufundsha Seko Omba Kubadilishwa Idara Uingia Idara Ya Elimu Sekondari, Ila Zamani Ilikuwa Bed Psyc Unasomea Somo Moja La Content, Nakushauri Uende TSD Katika Wilaya Uliopo Watakuelewesha Vizuri Zaidi.
NAOMBA unisaidie katika hili km unaufahamu nalo vizuri:
Niliajiriwa mwaka 2012 nikiwa na elimu ya Stashahada, mwaka 2016 nikaenda kusoma shahada ya kwanza lakini hadi sasa sijapandishwa daraja. Nilipofatilia nikaambiwa sikukitumikia cheo cha sasa kwa miaka 4 mfululizo kulingana na maelekezo ya sasa. Swali, je nikipeleka cheti nitabadilishiwa muundo wa utumishi na kulipwa mshahara wa shahada ya kwanza?