Skillionare
JF-Expert Member
- Nov 6, 2011
- 1,190
- 528
Jamani wadau naombeni kuuliza mfano mtu ni mwalimu wa shuleni ya msingi ameajiriwa na serikali alaf akawa pia na fani ya manunuzi yaani diploma in procurement and logstics management. Je? Anaweza kufanyiwa recategorization kuhamiamia fani ya procurement? Na procec zake zipoje?
Sheria inasema kama nafasi ipo utapewa ila utaanza na entry point cheo na mshahara wa kazi utakayo. Eg ulikuwa unalipwa 3mil kama ticha ukiwa recotegorized to Supplies Officer ambayo entry salary ni 6laki ndio utapewa. Tena mara moja Lawson inakusoma. Wanasema hakuna mshahara binafsi. Kubadilisha fani ni kiherehere chako adhabu yake ni kukuondolea mshahara uliotumikia 20years, 30 na utastaafu na hiyo entry salary ya recotegorization
mkuu je hzo nafac huwa znatoka na kuaply mfano u2mishi na kuomba kimyakimya au inakuaje?. Kwa mfano mm nafundisha shule x na nikaona tangazo la serikali likiitaj afisa ugavi je jukumu langu nitafanyeje ili niwe recategorized?
kaka deo, kuomba kimya kimya inawezekana. Ila sekretariati ya ajira hawafanyi recotegorization. Kama utawambia hujawahi ajiriwa, ukaajiriwa upya system itakukataa kwa kuwa una check namba tayari.
Hii imekaa vizuri sana
niwaulize tena hivi chek namba inaishia wapi?maana mfano mimi mwalimu nina chek namba nikaenda kuomba kazi kwa agency za serikali mfano tanesco,tra je bado chek namba itasoma kwa tanesco kwamba nimeshaajiriwa hii chek namba kwa serikali wapi haipo.
mimi ni mwalimu wa primary bagamoyo nataka kuhamia uhasibu maaana nilisoma accounts level ya degree je barua ya recategorization ipite kwa nani kati ya afisa elimu,mkurugenz au afisa utumish
barua yako inaanzia kwa mkuu wako wa idara then kwa utumishi ambaye ataitisha bodi ya ajira kama unakidhi vigezo wanakupitisha baada ya hapa kamati ya fedha na utawala inapitisha.unakuwa tayari umebadilishwa kazi. Angalizo mshahara unaanza mwanzo kama first entrance.
Zoezi hili linachukua muda gani kukamilika, mfano barua imeandikwa June 10/2015, na mwaka wa fedha ni July, 2015/16 je hapo awamu ya pili anaweza kuwa tayari kwenye sdystem ya ajira mpya!?
Asante sana mkuu kwa ushaurii wako sasa baada ya hapo ukithibitishwa unaweza kwenda kufanya kazi gani halmashauri??tofautu na kufundisha vyuoni?
Recategorization Hufanyiwa Mtumishi Ambaye Amejiendeleza Na Kupata Sifa Ya Kuingilia Ktk Kazi Husika, Mfano Mwalimu Akijiendeleza Kwenye Uhasibu/ Kilimo Ngazi Ya Shahada, Anaweza Kubadilishwa Kuwa Muhasibu/ Afisa Kilimo Na Kuanza Na Mshahara Wa Cheo Kipya Hata Kama Alikuwa TGTS F Kama Ni Uhasibu Ataanza Na TGS D,kwa Nilivyokuelewa Wewe Ni Mwalimu Na Huhitaji Kufanyiwa Recateg, Kama Unapenda Kufundsha Seko Omba Kubadilishwa Idara Uingia Idara Ya Elimu Sekondari, Ila Zamani Ilikuwa Bed Psyc Unasomea Somo Moja La Content, Nakushauri Uende TSD Katika Wilaya Uliopo Watakuelewesha Vizuri Zaidi.