Reax to Jakaya's Speech

Selemani

JF-Expert Member
Aug 26, 2006
947
292
Off Mwananchi


RAIS Jakaya Kikwete jana alilihutubia taifa, huku akitumia muda mwingi kujibu mapigo ya kauli za Chadema dhidi yake na kutahadharisha kuwa chama hicho, kina lengo la kuleta machafuko nchini."Kauli na vitendo vya wenzetu hao vyenye dhamira ya kutaka kuleta machafuko makubwa na uvunjifu wa amani nchini." alisema Rais Kikwete ambaye amekuwa kimya bila kulihutubia taifa kwa muda wa miezi miwili.

Onyo la Rais Kikwete limekuja siku chache baada ya Chadema kumpa siku tisa ikitaka mkuu huyo wa nchi atekeleze baadhi ya mambo ikiwamo kutoilipa fidia ya Sh94 bilioni kampuni ya Dowans.

Lakini, jana katika hotuba yake, Rais Kikwete pamoja na kufafanua hoja kadhaa, alisisitiza "Hayo si matatizo ya kumalizika ndani ya siku tisa."

Rais Kikwete alifafanua kwamba, hivi karibuni wananchi wengi wameingiwa na hofu kubwa kuhusu usalama wa nchi yao hali ambayo ni ngeni kwa Watanzania.

"Hofu hiyo inatokana na kauli na vitendo vya wenzetu wa Chadema vyenye dhamira ya kutaka kuleta machafuko makubwa na uvunjifu wa amani nchini," alieleza Rais Kikwete.

Mkuu huyo wa nchi ambaye tayari amemaliza siku 100 za ngwe yake ya pili akiwa Ikulu, aliweka bayana kuwa kufanya maandamano na mikutano ni haki ya msingi ya vyama vya siasa na raia, lakini, akaonya kuigeuza fursa hiyo kuwa jukwaa la kuchochea ghasia kwa nia ya kuindoa Serikali iliyoko madarakani kwa mabavu.

Kikwete alisisitiza kuwa hatua hiyo ni matumizi mabaya ya fursa ya kufanya maandamano na isiyostahili kuungwa mkono na Watanzania wazalendo, wapenda amani na nchi yao.

Rais alisema Tanzani ni nchi ya kidemokrasia na kila miaka mitano hufanyika uchaguzi wa kuchagua viongozi na kuweka bayana.

"Uchaguzi wa mwisho tumefanya tarehe 31 Oktoba, 2010. Kabla ya hapo tulikuwa na kampeni zilizochukua karibu miezi mwili na nusu. "

Kwa mujibu wa Rais Kikwete, katika kampeni hizo, kila chama kilielezea jinsi kitakavyokabiliana na matatizo yanayowakabili wananchi ikiwa ni pamoja na hayo yanayoyazungumzwa sasa na Chadema.

"Hatimaye siku ya uchaguzi wananchi walifanya uamuzi wa kuchagua chama walichokiamini, nacho ni Chama cha Mapinduzi.,"alieleza

"Iweje leo, miezi mitatu baadaye kwa mtu au chama cha siasa kufanya maandamano kwa masuala yale yale waliyoyasema kwenye kampeni. Siyo sawa hata kidogo," alisema Rais Kikwete.

"Kuchochea ghasia ati kwa nia ya kuiondoa Serikali madarakani ni kinyume cha Katiba na ni kuiingiza nchi katika mgogoro usiokuwa wa lazima. Tutasababisha umwagaji wa damu, watu kupoteza maisha na mali zao kuharibiwa bila sababu yoyote ya msingi,"alionya Rais Kikwete.

Kikwete alisema katika nchi ya kidemokrasia na kwa wanademokrasia wa kweli, wanapomaliza uchaguzi mmoja, hujiandaa kwa uchaguzi mwingine kwa kujenga upya chama , kuongeza wanachama, kuboresha sera na hoja pamoja na namna ya kuziwasilisha ili watu wawakubali na kuwachagua.

Rais Kikwete aliitaka Chadema kutumia Bunge kuwasilisha hoja zao badala ya mikutano ya hadhara inayotoa kauli za chuki kwa Serikali.

"Na, uwanja muhimu wa kufanya sehemu kubwa ya hayo ni katika Bunge na Halmashauri za Wilaya kupitia wabunge na madiwani wenu,"alieleza Rais Kikwete

Kikwete ambaye mara ya mwisho alitoa hotuba ya mwezi wakati wa mwaka mpya wa 2011, alisema kuacha kufanya hivyo na badala yake kuamua kuzunguka nchi nzima na kuchochea ghasia kwa lengo la kuwaondoa walioshinda ni kinyume na misingi ya demokrasia na kusisitiza

Alisisitiza "Tutajenga misingi ya hovyo na nchi yetu itakosa amani na utulivu daima."

Aliwataka Chadema kukaa chini na kujiuliza wanachokifanya na athari zake kwa wananchi akisema, "kama kila atakayeshindwa uchaguzi anafanya hivyo tutakuwa nchi ya namna gani?"

"Tanzania yetu hii yenye sifa na heshima ya kuwa nchi ya amani na utulivu itapoteza kabisa sifa hiyo na badala yake umwagaji wa damu na mateso kwa watu wasiokuwa na hatia vitageuka kuwa maisha ya kawaida." alisema.

Rais alisema kitendo hicho haikiitendei haki nchi na hata wananchi ambao viongozi wa siasa wamekuwa wakidai kuwapenda na kuwatetea.

"Ndugu Zangu, Watanzania Wenzangu; ndugu zetu wa Chadema wanayajua yote haya, lakini wanalo lao jambo. Wanataka kuipeleka nchi yetu pabaya kwa kukidhi uchu wao wa madaraka. Kwao sasa demokrasia haina maana, inaweza kusubiri," alifafanua Rais.

Aliwataka Watanzania kuwa makini na Chadema akisema "naomba tuyakatae mambo yao. Tusiwafuate. Waambieni mchezo wao ni hatari na ni mauti yetu. Sisi katika Serikali tutajitahidi kutimiza wajibu wetu wa kulinda usalama wa nchi yetu, watu wake na mali zao."

Hali ngumu ya maisha
Rais alikiri, "Ni kweli kuna hali ngumu ya maisha, na kukabiliana nayo ndiyo kazi tunayoendelea nayo kufanya kila siku."

"Tumeelekeza nguvu zetu na rasilimali zetu huko na mafanikio yanaonekana katika nyanja mbalimbali na maeneo mbalimbali, lakini akisisitiza, "hayo si matatizo ya kumalizika ndani ya siku tisa."

Alifafanua kwamba, kikwazo siyo upungufu wa sera wala dhamira, bali ni kiwango cha maendeleo madogo ya uchumi wa nchi na hivyo uwezo siyo mkubwa wa kuyakabili na kuyamaliza matatizo yote haraka kama ambavyo ingepaswa iwe.

Kikwete akirejea zama mbali za viongozi mbalimbali tangu uhuru, alisema hata Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere aliongoza kwa miaka 23 na hakuyamaliza matatizo ya maendeleo ya nchi hii.

"Na wale wa umri wangu au kunizidi wanakumbuka hali ilivyokuwa wakati anang’atuka. Hakuacha nchi ikiwa tajiri. Mzee Mwinyi kakaa miaka 10 hakuyamaliza, Mzee Mkapa nae kakaa miaka 10 hakuyamaliza. Mie nimekaa miaka mitano hayakwisha na nitamaliza mitano hayataisha yote." alisema

Alisema jambo la muhimu ni kuwa katika kila awamu nchi iweke malengo ya kupiga hatua ya kusonga mbele katika kujiletea maendeleo na kuongeza, hali iliyokuwa wakati ule sivyo ilivyokuwa mwaka 1985, wala 1995 au 2005 na ilivyo sasa.

Kuhusu mafanikio yake alisema, "Katika miaka mitano hii kuna maendeleo yanayoonekana wazi, pamoja na changamoto nyingi tumefanya juhudi kubwa na mafanikio yanaonekana katika nyanja zote za maisha ya Watanzania. Mwenye macho haambiwi tazama.''

Rais alirejea matukio mbalimbali yanayoitikisa dunia, akisema ni muhimu watu kutambua ukweli kwamba uchumi kama wetu ambao haujajenga uwezo wake wa ndani wa kujitosheleza kwa mahitaji yake, huathirika sana na yanayotokea katika uchumi wa dunia.

"Unapoyumba na sisi tunayumba. Bei za mafuta katika soko la dunia zikipanda na kwetu kupitia gharama za uchukuzi na uzalishaji huongezeka na kusababisha bei za bidhaa kupanda," alifafanua Rais akitaka wananchi wafahamu jinsi athari za dunia zinavyoweza kugusa uchumi wa nchi.

Mfumuko wa bei ukipanda China, nguo na bidhaa tunazonunua kutoka China hupanda bei. Hivi sasa mataifa yote makubwa tunakonunua bidhaa mfumuko wa bei umepanda na sisi tunaathirika.

Alihoji, "mvua ikikosekana kunakuwa na uhaba wa chakula, bei za vyakula hupanda na watu wengine hukosa chakula. Lawama kwa Serikali au Rais Kikwete inaanzia wapi?

Hali ya Umeme
Rais alikiri pia hali ya upatikanaji wa umeme nchini kwamba ni mbaya na kuweka bayana, "chanzo cha matatizo ni kupungua sana kwa maji katika bwawa kubwa la Mtera.

"Hadi jana kina cha bwawa hilo kimeshuka hadi kufikia mita 691.25 ambacho ni pungufu kwa mita 7. Kwa sasa zimebaki mita 1.25 tu juu ya kiwango cha chini kinachoruhusiwa kuendesha mitambo ya kuzalisha umeme,"alisema.

Hata hivyo, alisema 15 Februari, 2011, Baraza la Mawaziri lilijadili na kuidhinisha mpango wa dharura wa Tanesco wa kukodi mitambo ya kuzalisha MW 260 za umeme na kuongeza, baraza limeitaka bodi na menejimenti ya shirika hilo kuhakikisha mchakato huo unakamilika mapema iwezekanavyo ili kupunguza makali na athari za ukosefu mkubwa wa umeme kwa jamii na uchumi wa nchi.

Akionekana kukwepa jinamizi la Richmond aliyowahi kuita kuwa ni 'Phantom,' Rais alisema, ilisisitizwa pamoja na udharura uliokuwepo sheria na taratibu za manunuzi ya umma vizingatiwe kwa kuhakikisha mkataba utakaoingiwa uwe ni wenye maslahi kwa taifa na watoa huduma wawe ni makampuni yanayofahamika na yenye sifa stahiki na kuaminika.

Milipuko ya Gongo la Mboto

Kikwete ambaye ni Amiri Jeshi Mkuu, alitangaza kwamba Serikali itawalipa fidia waathirika wa mambomu yao na kwamba Shirika la Uchumi la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMA -JKT) limepewa wajibu wa kujenga upya nyumba zilizobomolewa na mabomu hayo.

Rais alifafanua, "Nimeagiza Jeshi la Kujenga Taifa lifanye kazi hiyo kupitia Shirika lake la Uchumi. Nimeamua hivyo ili kuhakikisha kuwa maisha ya ndugu zetu waliokumbwa na maafa haya yanarejea kuwa ya kawaida mapema iwezekanavyo."

Aliongeza kwamba, ameagiza Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa ishirikiane na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na Kitengo cha Taifa cha Maafa kuhakikisha kuwa utekelezaji unaanza mapema iwezekanavyo.

Hali ya chakula
Akizungumzia tatizo hilo Rais alisema, katika baadhi ya maeneo nchini kumeanza kujitokeza matatizo ya upungufu wa chakula kuanzia mwezi Januari 2011 na kuongeza, mengi ya maeneo hayo ni yale yanayopata mvua za vuli ambazo bahati mbaya hazikuwa nzuri.

" Imetambuliwa katika Halmashauri 36 za mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Morogoro, Mwanza, Shinyanga, Mara, Tabora, Singida, Dodoma, Lindi, Mtwara na Iringa ndiko kwenye maeneo mengi yenye upungufu mkubwa, " alisema Rais.

Hata hivyo, alisema tayari serikali imeidhinisha kutolewa kwa jumla ya tani 13,760 za chakula kutoka Akiba ya Taifa ya Chakula (NFRA) kwa ajili ya kuhudumia watu 423,530 walioathiriwa na upungufu wa chakula katika maeneo hayo huku kazi ya usambazaji ikiendelea.

" Hadi sasa jumla ya tani 4,822 za chakula cha msaada kimekwishatolewa katika mikoa ya Arusha, Iringa, Morogoro na Lindi. Napenda kuwathibitishia kuwa tutafanya kila tuwezalo kuhakikisha kuwa hakuna Mtanzania atakayekufa kwa njaa. Tutawahudumia ipasavyo hawa waliokwishatambulika na wengineo watakaojitokeza siku za usoni, " alifafanua.

Mbowe amjibu

MWENYEKITI wa Chadema, Freeman Mbowe amesema chama chake hakitaacha maandamano licha ya kushutumiwa na Rais Jakaya Kikwete kuwa wanachochea vurugu katika hotuba yake ya mwisho wa mwezi.

Mbowe ambaye alikuwa akihutubia katika Uwanja wa Josho Mjini Shinyanga, alisema kuwa ameamua kuijibu mapema ili kueleza msimamo wa chama chake kuwa hawataacha maandamano hata wakikamatwa na kuwekwa ndani.

“Kikwete leo atahutubia taifa na kusema maandamano yetu yanachochea vurugu, namjibu kuwa tutaandamana na tutaendelea kuandamana. Tunaandamana kwa sababu hatutaki Dowans ailipe kama ambavyo yeye na Kamati Kuu ya chama chake wameamua kuilipa kwa fedha za walipa kodi,” alieleza.

Alisema Rais Kikwete anazungumzia bei ya sukari wakati akijua fika kuwa tatizo ambalo limesababisha kupanda kwa bei ya sukari na kuyafanya maisha ya Watanzania kuwa magumu ni sera mbovu za chama chake na kushindwa kwa utawala wake.

“Kikwete anazungumzia mgao wa umeme, taifa gani limekaa na mgao wa umeme kwa miaka saba na halitatuliwi. Halafu anataka tuheshimu Serikali, tusiandamane, tutaendelea kuandamana na tutaandamana,” alisema Mbowe.

Alisema katika hotuba yake ya mwezi amezungumzia juu ya Serikali yake kununua mitambo mingine ya kufua umeme kwa kutumia kiasi cha Sh 400 milioni fedha za walipa kodi wakati la Dowans halijaisha.

“Haki ya Mungu tutaendela kuandamana na kama anatuona sisi ni wachochezi basi anikamate Mbowe na wengine anaowaona wachochezi na akatushitaki, leo tunaandamana Shinyanga na kurudi makwetu kwa amani, lakini kuna siku tutaandamana na hatutarudi ila sijui tutakwenda wapi kama hapa Shinyanga tutaenda kwa mkuu wa mkoa sijui…” alieleza Mbowe.
 
Off Daily News

Local News
Kikwete: Chadema should behave


By DAILY NEWS Reporter, 28th February 2011 @ 20:00, Total Comments: 0, Hits: 299

PRESIDENT Jakaya Kikwete has warned the opposition Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) against abuse of the principles of democracy through provocative statements likely to lead to breach of peace and unnecessary suffering to innocent people.

Through televised end-of-month address to the nation, President Kikwete said the constitution allowed peaceful demonstrations to political parties or individual citizens but it appeared as if Chadema misused the opportunity to advance own agenda to incite violence.

"No other times in the country's history that people were gripped by fear, only this time when Chadema organizes demonstrations countrywide to incite violence with the intention to unseat the legitimate government that came to power through the ballot box. The claims are unjustifiable, don't listen to them. Tell them that their joy was nothing but a dangerous situation to the nation," President Kikwete stressed.

He said after every five years, Tanzania goes for democratic elections. They were last held on October 31, 2010, adding each political party held election campaign rallies explaining how to address problems facing the nation but finally CCM was given the mandate by voters to form the government.

"It is strange to see the same party that went around making similar arguments three months down the line, organize demonstrations accusing the government of not doing enough to solve problems the way it suits them. There are reasons for ongoing power rationing and deliberate efforts are underway to address the challenges. Incitement is against the constitution and should never be entertained," Mr Kikwete stated.

The president said in a democratic country like Tanzania the post election period is the time for each political party to reflect on the previous performance and make corrections where the presentation was not impressive instead of moving across the regions to propel seditious proclamations.

"If such trends which lead to anarchy are allowed to prevail, the nation will end up building chaotic system of governance. What kind of a country would that be if every defeated party decides to take to the street to demand for powers through mob action? This is undemocratic and unjustifiable means to stand for the people the party claims to love most. The government will always safeguard the principles of democracy for sustainable peace, unity and stability," he emphasized.

Commenting on the rising cost of living, President Kikwete said the situation had nothing to do with policies or the degree of commitment but rather the economic ability of the nation to address the challenges the way everyone would appreciate.

"These are not problems that can be resolved within nine days. The first phase government under Mwalimu Nyerere did not solve all problems, likewise the second and the third government under President Ali Hassan Mwinyi and Benjamin Mkapa respectively. Some levels of development are realized successively," he explained.

He said in case of global inflation, developing nations like Tanzania with unstable economic bases were equally affected, adding exception of import taxes to some commodities has been one of the strategies employed to alleviate the situation.

With regard to measures taken to arrest the situation in Gongo la Mboto bomb blasts that claimed 27 lives, President Kikwete said the government in collaboration with foreign experts from the United States of America has embarked on factors behind the tragic incident and work out measures to prevent it from happening again.

The president announced to have instructed authorities to grant the contract to the National Service Construction Agency (SUMA) to ensure timely and quality construction of all the destroyed houses that rendered 539 people homeless.

He thanked all generous parties who were moved in the heart and shared sympathy through material contributions to the victims ranging from mattresses, bed sheets, food, water, utensils, medicine and cash money.
 
Off Uhuru

JK: Chadema ni hatari kwa taifa
TUESDAY, 01 MARCH 2011 07:49 NEWSROOM
* Imelenga kuleta machafuko
*Mchezo wao ni mauti kwa raia
* Afafanua tatizo la umeme

Na Mwandishi Wetu

RAIS Jakaya Kikwete amesema viongozi wa CHADEMA wana lengo la kuleta machafuko nchini, kukidhi kiu yao ya uchu wa madaraka. Amesema viongozi hao wanataka kutumia mabavu kuindoa serikali iliyoingia madarakani kwa njia ya demokrasia. Rais Kikwete akilihutubia taifa jana katika hotuba yake ya mwisho wa mwezi, alisema CHADEMA wana lao jambo. "Wanataka kuipeleka nchi pabaya kwa kukidhi uchu wao wa madaraka, kwao sasa demokrasia haina maana, inaweza kusubiri, wanataka kutumia mabavu. Naomba tuyakatae mambo yao, tusiwafuate. "Waambieni mchezo wao ni hatari na ni mauti yetu. Sisi katika serikali tutajitahidi kutimiza wajibu wetu wa kulinda usalama wa nchi, watu wake na mali zao," alisema.

Alisema katika kipindi cha karibuni wananchi wengi wameingiwa hofu juu ya usalama wa nchi, na ni mara ya kwanza Watanzania kuwa katika hali hiyo. Rais Kikwete alisema kauli na vitendo vya CHADEMA vinaonyesha wana dhamira ya kutaka kuleta machafuko makubwa na uvunjifu wa amani nchini.

Alisema kufanya maandamano na mikutano ni haki ya msingi ya vyama vya siasa na raia, lakini kuigeuza fursa hiyo kuwa jukwaa la kuchochea ghasia kwa nia ya kuiondoa serikali iliyoko madarakani kwa mabavu ni matumizi mabaya ya fursa hiyo.

Rais Kikwete alisema Tanzania ni nchi ya kidemokrasia na kila baada ya miaka mitano inafanya uchaguzi wa viongozi kwa uwazi na mtu hutumia miezi mwili na nusu kujinadi kwa Watanzania.

"Wananchi walifanya uamuzi wa kuchagua chama walichokiamini, nacho ni CCM, sasa iweje leo miezi mitatu baadae kwa mtu au chama cha siasa kufanya maandamano kwa masuala yale yale waliyoyasema kwenye kampeni.

"Si sawa hata kidogo kuchochea ghasia kwa nia ya kuiondoa serikali madarakani, ni kinyume cha Katiba na ni kuiingiza nchi katika mgogoro usiokuwa wa lazima," alisema.

Rais Kikwete aliongeza: "Tutasababisha umwagaji wa damu, watu kupoteza maisha na mali zao kuharibiwa bila sababu ya msingi."

Alisema katika nchi ya kidemokrasia na kwa wanademokrasia wa kweli, mnapomaliza uchaguzi mmoja, mnajiandaa kwa uchaguzi mwingine.

Rais Kikwete alisema kuamua kuzunguka nchi nzima na kuchochea ghasia kwa lengo la kuwaondoa walioshinda ili waingie madarakani ni kinyume cha misingi ya demokrasia.

"Tutajenga misingi ya ovyo na nchi yetu itakosa amani na utulivu daima. Hebu fikirieni kama kila atakayeshindwa uchaguzi anafanya hivyo, tutakuwa nchi ya namna gani?

"Tanzania yenye sifa na heshima ya kuwa nchi ya amani na utulivu itapoteza kabisa sifa hiyo na badala yake umwagaji wa damu na mateso kwa watu wasio na hatia vitageuka kuwa maisha ya kawaida," alionya.

TATIZO LA UMEME

Kuhusu tatizo la umeme, alisema chanzo ni kupungua maji katika bwawa la Mtera, ambapo kina kimeshuka hadi kufikia mita 691.25, ambacho ni pungufu kwa mita saba.

Alisema kwa sasa zimebaki mita 1.25 juu ya kiwango cha chini kinachoruhusiwa kuendesha mitambo ya kuzalisha umeme na kwamba, Baraza la Mawaziri lilijadili na kuidhinisha mpango wa dharura wa TANESCO wa kukodi mitambo ya kuzalisha megawati 260 za umeme.

Rais Kikwete alisema baraza limeitaka Bodi na Menejimenti ya TANESCO kuhakikisha mchakato huo unakamilika mapema iwezekanavyo, ili kupunguza makali na athari za ukosefu wa umeme kwa jamii na uchumi wa nchi.

Hata hivyo, alisema sheria na taratibu za ununuzi wa umma vizingatiwe na kuhakikisha mkataba utakaoingiwa uwe na maslahi kwa taifa.

Alisema watoa huduma wawe kampuni zinazofahamika, zenye sifa na kuaminika.

"Natambua Bodi na Menejimenti ya TANESCO wanaendelea na mchakato wa kupata umeme huo wa dharura kati ya sasa na Julai, 2011," alisema.

HALI YA MAISHA

Rais Kikwete alisema ni kweli kuna hali ngumu ya maisha, na serikali inaendelea kukabiliana nayo.

"Tumeelekeza nguvu na rasilimali zetu huko, na mafanikio yanaonekana katika nyanja na maeneo mbalimbali," alisema.

Alisema kikwazo si upungufu wa sera wala dhamira, bali kiwango cha maendeleo madogo ya uchumi, hivyo uwezo si mkubwa wa kuyakabili na kuyamaliza matatizo kwa haraka.

"Hayo si matatizo ya kumalizika ndani ya siku tisa. Mzee Nyerere (Julius Nyerere) aliongoza kwa miaka 23 na hakuyamaliza matatizo ya maendeleo ya nchi hii.

"Na wale wa umri wangu au kunizidi wanakumbuka hali ilivyokuwa wakati anang'atuka. Hakuacha nchi ikiwa tajiri. Mzee Mwinyi (Ali Hassan Mwinyi) kakaa miaka 10 hakuyamaliza, Mzee Mkapa (Benjamin Mkapa) naye kakaa miaka 10 hakuyamaliza," alisema.

Rais Kikwete aliongeza: "Nimekaa miaka mitano hayakwisha na nitamaliza mitano hayataisha yote. Lililo muhimu kuliko yote ni kuwa katika kila awamu nchi yetu imekuwa inapiga hatua ya kusonga mbele katika kujiletea maendeleo."

Alisema bei za mafuta katika soko la dunia zikipanda na nchini gharama za uchukuzi na uzalishaji huongezeka na kusababisha bei za bidhaa kupanda.

"Mvua ikikosekana kunakuwa na uhaba wa chakula, bei za vyakula hupanda na watu wengine hukosa chakula. Lawama kwa serikali au Rais Kikwete inaanzia wapi?" alihoji na kuongeza:

"Hata kwa matatizo yote hayo na mengine tumekuwa tunatafuta nafuu kwa kiwango tunachoweza. Aghalabu, hutoa nafuu ya kodi kama tulivyofanya kwa sukari na tulivyowahi kufanya kwa saruji. Tutaendelea kufanya hivyo inapobidi," alisema.
 
Off Habari Leo

Jumanne Machi 01, 2011
Habari za Kitaifa

Kikwete aionya Chadema
Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 1st March 2011 @ 07:52 Imesomwa na watu: 379; Jumla ya maoni: 3



RAIS Jakaya Kikwete amekionya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuacha vitendo na kauli za kuwajengea wananchi hofu kuhusu usalama wa nchi yao.

Amesema, vitendo hivyo vya Chadema vina dhamira ya kutaka kuleta machafuko makubwa na uvunjifu wa amani nchini.

"Kufanya maandamano na mikutano ni haki ya msingi ya vyama vya siasa na raia. Lakini, kuigeuza fursa hiyo kuwa jukwaa la kuchochea ghasia kwa nia ya kuiondoa Serikali iliyoko madarakani kwa mabavu, ni matumizi mabaya ya fursa hiyo," amesema Rais.

Rais Kikwete alikuwa akilihutubia Taifa jana katika utaratibu wake wa kuzungumza na wananchi kwa njia ya televisheni na redio.

Alisema, Tanzania ni nchi ya kidemokrasia na kila miaka mitano uchaguzi wa viongozi unafanyika na wa mwisho ukiwa ni uliofanyika Oktoba 31 mwaka jana.

"Kabla ya hapo tulikuwa na kampeni zilizochukua karibu miezi miwili na nusu. Kila chama kilielezea jinsi kitakavyokabiliana na matatizo ya wananchi wa nchi yetu, ikiwa ni pamoja na haya wanayoyazungumza sasa.

"Iweje leo, miezi mitatu baadaye kwa mtu au chama cha siasa kufanya maandamano kwa masuala yale yale waliyoyasema kwenye kampeni? Si sawa hata kidogo. Kuchochea ghasia eti kwa nia ya kuiondoa Serikali madarakani ni kinyume cha Katiba na ni kuiingiza nchi katika mgogoro usiokuwa wa lazima. Tutasababisha umwagaji wa damu, watu kupoteza maisha na mali zao kuharibiwa bila sababu yoyote ya msingi," alihadharisha Rais.

Aliwaasa Chadema kutumia Bunge na halmashauri za wilaya kuboresha sera na hoja zao na kuziwasilisha kwa watu badala ya kuzunguka nchi nzima kuchochea ghasia kwa lengo la kuingia madarakani.

"Tutajenga misingi ya hovyo na nchi yetu itakosa amani na utulivu daima. Hebu fikirieni, kama kila atakayeshindwa uchaguzi anafanya hivyo tutakuwa nchi ya namna gani? Tanzania yetu hii yenye sifa na heshima ya kuwa nchi ya amani na utulivu itapoteza kabisa sifa hiyo, na badala yake umwagaji damu na mateso kwa watu wasiokuwa na hatia vitageuka kuwa maisha ya kawaida," alisema Rais.

Alikiri kuwa hali ya maisha ni ngumu na kukabiliana nayo ndiyo kazi inayofanywa kila siku na Serikali na ndiko ilikoelekeza nguvu zake na mafanikio yanaonekana katika nyanja mbalimbali na maeneo mbalimbali.

"Kikwazo si upungufu wa sera wala dhamira, bali kikubwa ni kiwango cha maendeleo madogo ya uchumi wetu na hivyo uwezo wetu si mkubwa wa kuyakabili na kuyamaliza matatizo yote haraka kama ambavyo tunapenda iwe.

"Hayo si matatizo ya kumalizika ndani ya siku tisa. Mzee Nyerere aliongoza kwa miaka 23 na hakuyamaliza matatizo ya maendeleo ya nchi hii. Na wale wa umri wangu au kunizidi, wanakumbuka hali ilivyokuwa wakati anang'atuka. Hakuacha nchi ikiwa tajiri.

"Mzee Mwinyi kakaa miaka 10 hakuyamaliza, Mzee Mkapa naye miaka 10 hakuyamaliza.

Miye nimekaa miaka mitano hayakwisha na nitamaliza mitano hayataisha yote. Lililo muhimu kuliko yote ni kuwa katika kila awamu nchi yetu imekuwa inapiga hatua ya kusonga mbele katika kujiletea maendeleo," alisema.

Viongozi wa Chadema wanazunguka mikoani wakifanya mikutano ya kuhamasisha wananchi kuichukia Serikali iliyoko madarakani kwa madai kuwa imeshindwa kumaliza matatizo ya wananchi na hata kufikia kumwekea Rais muda wa kutatua matatizo hayo.

Rais Kikwete alisema ni kweli kuna hali ngumu ya maisha, na kwamba kukabiliana nayo ndiyo kazi wanayoendelea nayo kufanya kila siku.

"Tumeelekeza nguvu zetu na rasilimali zetu huko na mafanikio yanaonekana katika nyanja mbalimbali na maeneo mbalimbali. Kikwazo siyo upungufu wa sera wala dhamira, kikwazo kikubwa ni kiwango cha maendeleo madogo ya uchumi wetu na hivyo uwezo wetu siyo mkubwa wa kuyakabili na kuyamaliza matatizo yote haraka kama ambavyo tunapenda iwe.

Lakini, pia ni muhimu watu kutambua ukweli kwamba uchumi kama wetu ambao haujajenga uwezo wake wa ndani wa kujitosheleza kwa mahitaji yake, huathirika sana na yale yanayotokea katika uchumi wa dunia. Unapoyumba na sisi tunayumba. Bei za mafuta katika soko la dunia zikipanda na kwetu kupitia gharama za uchukuzi na uzalishaji huongezeka na kusababisha bei za bidhaa kupanda," alieleza Rais.

"Mfumuko wa bei ukipanda China, nguo na bidhaa tunazonunua kutoka China hupanda bei. Hivi sasa mataifa yote makubwa tunakonunua bidhaa mfumuko wa bei umepanda na sisi tunaathirika. Mvua ikikosekana kunakuwa na uhaba wa chakula, bei za vyakula hupanda na watu wengine hukosa chakula

"Lawama kwa Serikali au Rais Kikwete inaanzia wapi? Hata kwa matatizo yote hayo na mengine tumekuwa tunatafuta nafuu kwa kiwango tunachoweza. Aghalabu, hutoa nafuu ya kodi kama tulivyofanya kwa sukari na tulivyowahi kufanya kwa saruji na kadhalika. Tutaendelea kufanya hivyo inapobidi."

Kuhusu umeme, Rais alisema imekubalika kukodi mitambo ya megawati 260, lakini ikasisitizwa kuwa pamoja na udharura uliopo, sheria na taratibu za ununuzi wa umma vizingatiwe. Pia, ihakikishwe kuwa mikataba inayoingiwa iwe ni yenye maslahi kwa Taifa.

Vilevile, watoa huduma wawe ni kampuni zinazofahamika na zenye sifa stahiki na kuaminika.

"Bahati mbaya sana tatizo la ukame limetukuta tena wakati mipango mingi ya umeme imeanza lakini haijakamilika. Miaka miwili ijayo, hali itakuwa tofauti sana, kwani miradi hii na mingine kadhaa itakuwa imekamilika na kulihakikishia Taifa uhakika wa umeme," alisema.

Alisema miradi hiyo ya umeme huchukua muda kukamilika. Mitambo huchukua muda kutengenezwa na ujenzi wa vituo pia. "Ingekuwa ni mitambo ya kununua tu dukani tungefanya hivyo na kulimaliza mara moja tatizo hili. Tena lingeisha zamani na wala sisi tusingelikuta," alisema.

Akizungumzia chakula, Rais alisema hali ya upatikanaji wa chakula nchini katika maeneo mengi ni ya kuridhisha isipokuwa katika maeneo machache. Taarifa ya Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, inaonesha kwamba kuna akiba ya kutosha ya chakula katika maghala ya Serikali, ya wafanyabiashara wakubwa na ya wakulima mashambani.

"Maghala ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula yana tani 216,012 za mahindi na mpunga, nafaka ambazo zinatuhakikishia kuwa upungufu wowote wa chakula tutaukabili bila matatizo. Kiasi hicho ndicho kikubwa kuliko chote kilichowahi kuhifadhiwa tangu hifadhi hiyo ianzishwe na shabaha yetu ni kufikia tani 400,000 mwaka 2015," alisema.

Kuhusu waathirika wa mabomu, Rais alisema maiti wote 25 wameshazikwa kwa gharama ya Serikali kule ambako ndugu waliamua wakazikwe. Kwa ajili hiyo maiti 10 wamezikwa Dar es Salaam na wengineo mikoani kama ifuatavyo.

Mara walizikwa wanne, Pwani watatu, Tanga wawili, Lindi mmoja, Kagera mmoja, Kilimanjaro mmoja, Mbeya mmoja na Mtwara mmoja. Majeruhi wameendelea kupatiwa matibabu na huduma stahili.

Mpaka sasa alisema kuna majeruhi 36 ambao bado wamelazwa katika hospitali za Amana, Temeke na Muhimbili.

Watoto 857 waliopotezana na wazazi wao wameshaunganishwa na familia zao. Hata hivyo, 15 bado hawajatambuliwa na wazazi au walezi wao. Kwa sasa watoto hao wamepelekwa kwenye kituo cha kulelea watoto cha Kurasini.

Kuhusu nyumba zilizobomoka kutokana na milipuko hiyo ya Februari 16, Rais Kikwete alisema utekelezaji wa agizo la kutambua na kufanya tathmini ya nyumba zilizoharibiwa unaendelea kwa nia ya kuwafidia ipasavyo.

"Kwa upande wa fidia, tumeamua kuwa Serikali ibebe jukumu la kujenga upya nyumba hizo kwa mujibu wa kiwango cha uharibifu. Nimeagiza Jeshi la Kujenga Taifa lifanye kazi hiyo kupitia Shirika lake la Uchumi. Nimeamua hivyo ili kuhakikisha kuwa maisha ya ndugu zetu waliokumbwa na maafa haya, yanarejea kuwa ya kawaida mapema iwezekanavyo.
Hata hivyo, aliwasihi Watanzania kuwa na subira na kuacha tabia za kueneza uvumi kwenye vijiwe vya kahawa na kwenye vikao vya kinywaji, kuhusu chanzo cha milipuko hiyo.

"Wakati mwingine watu wanageuza dhana zao kuwa ndiyo ukweli na kupotosha au hata kuwatia watu hofu. Wataalamu wamekwishafika, ukweli wenyewe utajulikana baada ya muda si mrefu," alisema
 
Hoja za Rais kuhusu Chadema zinatia kichefuchefu. Ni kweli imefika wakati Rais wetu anajibu altimutum ya siku 9!! Kauli ya siku 9 inamtisha Rais na Amiri Jeshi Mkuu! Come on guyz! He is not serious!!
 
off Majira


Kikwete alia na CHADEMA
*Ahofia maandamano yao na mikutano inayoendelea mikoani
*Asema yanachochea ghasia kuiondoa serikali madarakani

Na Edmund Mihale

RAIS Jakaya Kikwete jana kwa mara ya kwanza amezungumzia maandamano ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) yanayoendelea
katika mikoa mbalimbali nchini kupinga gharama za maisha akiyaelezea kuwa yenye dhamira ya kutaka kuleta machafuko na uvunjifu wa amani nchini.

Akilihutubia Taifa katika hotuba yake kila mwezi, Ikulu jana, Rais Kikwete alisema kufanya maandamano na mikutano ni haki ya msingi ya vyama vya siasa na raia. Lakini, kuigeuza fursa hiyo kuwa ni jukwaa la kuchochea ghasia na kwa nia ya kuiondoa serikali iliyoko madarakani kwa mabavu ni matumizi mabaya ya fursa hiyo.

"Nchi yetu ni ya kidemokrasia na kila miaka mitano tunafanya uchaguzi wa kuchagua viongozi wetu. Uchaguzi wa mwisho tumefanya Oktoba 31, 2010. Kabla ya hapo tulikuwa na kampeni zilizochukua karibu miezi mwili na nusu. Kila chama kilielezea jinsi kitakavyokabiliana na matatizo yanayowakabili wananchi wa nchi yetu ikiwa ni pamoja na haya wanayoyazungumza sasa.

"Hatimaye siku ya uchaguzi wananchi walifanya uamuzi wa kuchagua chama walichokiamini, nacho ni Chama Cha Mapinduzi (CCM). Iweje leo, miezi mitatu baadaye kwa mtu au chama cha siasa kufanya maandamano kwa masuala yale yale waliyoyasema kwenye kampeni.

"Siyo sawa hata kidogo, kuchochea ghasia ati kwa nia ya kuiondoa serikali madarakani ni kinyume cha katiba na ni kuiingiza nchi katika mgogoro usiokuwa wa lazima.

"Tutasababisha umwagaji wa damu, watu kupoteza maisha na mali zao kuharibiwa bila sababu yoyote ya msingi," alisema Rais Kikwete.

Alisema katika nchi ya kidemokrasia na kwa wanademokrasia wa kweli, wanapomaliza uchaguzi mmoja, wanajiandaa kwa mwingine. Wanajenga upya chama chao, wanaongeza wanachama, wanaboresha sera na hoja zao pamoja na namna ya kuziwasilisha ili watu wawakubali wao na kuwakataa wenzao.

Alisema uwanja muhimu wa kufanya hivyo ni sehemu ya bunge na halmashauri za wilaya kupitia wabunge na madiwani

Alisema kitendo kinachofanywa na Chadema cha kuzunguka nchi nzima na kuchochea ghasia kwa lengo la kuwaondoa walioshinda ili waingie ni kinyume na misingi ya demokrasia.

"Tutajenga misingi ya hovyo na nchi yetu itakosa amani na utulivu daima. Hebu fikirieni, kama kila atakayeshindwa uchaguzi anafanya hivyo tutakuwa nchi ya namna gani?

"Tanzania yetu hii yenye sifa na heshima ya kuwa nchi ya amani na utulivu itapoteza kabisa sifa hiyo na badala yake umwagaji wa damu na mateso kwa watu wasiokuwa na hatia vitageuka kuwa maisha ya kawaida. Hatuitendei haki nchi yetu na hatuwatendei haki wananchi tunaodai tunawapenda na kuwatetea.

"Ndugu zetu wa CHADEMA wanayajua yote haya, lakini wanalo lao jambo. Wanataka kuipeleka nchi yetu pabaya kwa kukidhi uchu wao wa madaraka. Kwao sasa demokrasia haina maana, inaweza kusubiri. Wanataka kutumia mabavu. Naomba tuyakatae mambo yao. Tusiwafuate. Waambieni mchezo wao ni hatari na ni mauti yetu. Sisi katika serikali tutajitahidi kutimiza wajibu wetu wa kulinda usalama wa nchi yetu, watu wake na mali zao," alisema Rais Kikwete.

Akizungmuzia hali ya maisha ya Mtanzania, Rais Kikwete amekiri kuwa kwa sasa hali ni ngumu ya kimaisha, hivyo amewataka kukabiliana nayo.

Alisema kuwa serikali kwa upande wake imeelekeza nguvu na rasilimali zote na mafanikio yanaonekana katika nyanja mbalimbali na maeneo mbalimbali. hivyo kikwazo siyo upungufu wa sera wala dhamira, bali kikwazo kikubwa ni kiwango cha maendeleo madogo ya uchumi nchini na hivyo uwezo siyo mkubwa wa kuyakabili na kuyamaliza matatizo yote haraka kama ambavyo Watanzania wengi wanapenda iwe.

"Hayo si matatizo ya kumalizika ndani ya siku tisa. Mzee Nyerere aliongoza kwa miaka 23 na hakuyamaliza matatizo ya maendeleo ya nchi hii. Wa wale wa umri wangu au kunizidi wanakumbuka hali ilivyokuwa wakati anang’atuka. Hakuacha nchi ikiwa tajiri.

"Mzee Mwinyi kakaa miaka 10 hakuyamaliza, Mzee Mkapa naye kakaa miaka 10 hakuyamaliza. Mie nimekaa miaka mitano hayakwisha na nitamaliza mitano hayataisha yote. Lililo muhimu kuliko yote ni kuwa katika kila awamu nchi yetu imekuwa inapiga hatua ya kusonga mbele katika kujiletea maendeleo.

"Hali iliyokuwa wakati ule sivyo ilivyokuwa mwaka 1985, wala 1995 au 2005 na ilivyo sasa. Katika miaka mitano hii kuna maendeleo yanayoonekana wazi, pamoja na changamoto nyingi tumefanya juhudi kubwa na mafanikio yanaonekana katika nyanja zote za maisha ya Watanzania. Mwenye macho haambiwi tazama.

"Lakini, pia ni muhimu watu kutambua ukweli kwamba uchumi kama wetu ambao haujajenga uwezo wake wa ndani wa kujitosheleza kwa mahitaji yake, huathirika sana na yale yanayotokea katika uchumi wa dunia. Unapoyumba na sisi tunayumba," alisema Rais Kikwete.

Alisema kupanda kwa bei za mafuta katika soko la dunia zinasababisha gharama za uchukuzi na uzalishaji huongezeka na kusababisha bei za bidhaa kupanda hivyo mfumuko wa bei ukipanda China, nguo na bidhaa zinazonunuliwa kutoka China hupanda navyo hupanda bei.

Hivi sasa mataifa yote makubwa mfumuko wa bei umepanda na kuathiri uchumi wa nchi, kukosekana kwa mvua nako kunasababisha uhaba wa chakula, bei za vyakula hupanda na watu wengine hukosa chakula. Hivyo hivyo lawama kwa serikali au Rais Kikwete inaanzia wapi? aliahoji.

Alisema hata hivyo serikali imekuwa ikitafuta ufumbuzi wa matatizo yote kwa lengo la kutafuta unafuu kwa kiwango tunachowezekana ikiwemo kutoa unafuu wa kodi kama ilivyofanya kwa sukari na saruji pale. inapobidi.

Jana gazeti la serikali la Daily News lilimkariri Msajili wa Vyama vya Siasa, Bw. John Tendwa akisema kauli zinazotolewa kwenye maandamano hayo za kumpa muda wa siku tisa Rais Kikwete kutekeleza mahitaji yao ni za kichochezi na zinaweza kuingizwa katika makosa ya uhaini kwa kuwa kinawachichea wananchi waichukie serikali yao.

Hali ya umeme

Akizungumuzia hali ya umeme nchini alisema hali ya upatikanaji wa umeme nchini ni mbaya kutokana na kupungua kwa maji katika bwawa la Mtera ambayo juzi kina cha bwawa hilo kilishuka hadi kufikia mita 691.25 ambacho ni pungufu kwa mita 7 na kubaki mita 1.25 juu ya kiwango cha chini kinachoruhusiwa kuendesha mitambo ya kuzalisha umeme.

Alisema Februari 15 , 2011, Baraza la Mawaziri lilijadili na kuidhinisha mpango wa dharura wa TANESCO wa kukodi mitambo ya kuzalisha MW 260 za umeme. hivyo baraza hilo liliitaka Bodi na Menejimenti ya TANESCO kuhakikisha kuwa mchakato huo unakamilika mapema iwezekanavyo ili kupunguza makali na athari za ukosefu mkubwa wa umeme kwa jamii na uchumi wa nchi.

Alisema baraza hilo pia lilisisitizwa kuwa pamoja na udharura uliokuwepo sheria na taratibu za manunuzi ya umma vizingatiwe. Pia, wahakikishe kuwa mkataba watakaoingia uwe ni wenye maslahi kwa taifa na watoa huduma wawe ni kampuni zinazofahamika na zenye sifa stahiki na kuaminika.

"Natambua kuwa Bodi na Mejemienti ya Shirika la Umeme, wanaendelea na mchakato wa kupata umeme huo wa dharura kati ya sasa na Julai, 2011," alisema Rais Kikwete.

Alisema kuwa mwaka 2006/7 serikali iliamua kupunguza kutegemea umeme wa nguvu ya maji kwa kuongeza matumizi ya vyanzo vingine vya nishati.

Alisema mpango umetengenezwa na utekelezaji wake unaendelea na tayari umeme wa MW 145 wa kutokana na gesi asilia umeongezwa kwa kugharamiwa na serikali. na mwisho wa mwaka huu MW 160 zitaongezeka MW 100 Dar es Salaam na MW 60 Mwanza kwa gharama za serikali.

"Bahati mbaya kutokana na matatizo ya fedha ya kimataifa, wawekezaji wa sekta binafsi wa kuzalisha MW 300 za umeme wa gesi asilia pale Mtwara walijiondoa. Umeme huo ungekuwa tayari umeshaingizwa katika gridi ya taifa hivi sasa na kuondoa tatizo la sasa. Wawekezaji wengine wamepatikana na mazungumzo yanaendelea vizuri," alisema Rais Kikwete.

Alisema Mradi wa Kiwira umecheleweshwa na mchakato wa kubadili milki na kupata mkopo wa dola za Marekani milioni 400 za kuwezesha ujenzi wa kituo cha kuzalisha MW 200. Lakini suala la kubadili milki limefikia ukingoni na mchakato wa kupata mkopo unaendelea kwa matumaini.

Hali ya chakula nchini

Rais Kikwete tayari Halmashauri 36 za mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Morogoro, Mwanza, Shinyanga, Mara, Tabora, Singida, Dodoma, Lindi, Mtwara na Iringa imeripotiwa kuwa na upungufu mkubwa.

Alisema serikali imeidhinisha kutolewa kwa tani 13,760 za chakula kutoka Akiba ya Taifa ya Chakula (NFRA) kwa ajili ya kuhudumia watu 423,530 walioathiriwa na upungufu wa chakula katika maeneo hayo.

Alisema kazi ya usambazaji inaendelea. Hadi sasa jumla ya tani 4,822 za chakula cha msaada zimetolewa katika mikoa ya Arusha, Iringa, Morogoro na Lindi.

Fidia ya Gongolamboto

Alisema serikali imebeba jukumu la kujenga upya nyumba za wakazi wa eneo hilo kwa mujibu wa kiwango cha uharibifu.

"Nimeagiza Jeshi la Kujenga Taifa lifanye kazi hiyo kupitia Shirika lake la Uchumi. Nimeamua hivyo ili kuhakikisha kuwa maisha ya ndugu zetu waliokumbwa na maafa haya yanarejea kuwa ya kawaida mapema iwezekanavyo," alisema Rais Kikwete.

Alisema ameagiza Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na Kitengo cha Taifa cha Maafa kuhakikisha kuwa utekelezaji unaanza mapema iwezekanavyo
 
kwa sasa haitaji kuonewa huruma kwa sababu mabaya kayapika mwenyewe.
Alidhani baada ya uchaguzi hakuna maisha.
 
yaani sijawahi kuona rais duniani ***** na mlalamishi kama huyu mzeee.lever yake ilikuwa awe katibu tarafa
 
Off Mwananchi


PHP:
"Ndugu Zangu, Watanzania Wenzangu; ndugu zetu wa Chadema wanayajua yote haya, lakini wanalo lao jambo.  Wanataka kuipeleka nchi yetu pabaya kwa kukidhi uchu wao wa madaraka.  Kwao sasa demokrasia haina maana, inaweza kusubiri," alifafanua Rais. 

Aliwataka Watanzania kuwa makini na Chadema akisema "naomba  tuyakatae mambo yao.  Tusiwafuate.  Waambieni mchezo wao ni hatari na ni mauti yetu.  Sisi katika Serikali tutajitahidi kutimiza wajibu wetu wa kulinda usalama wa nchi yetu, watu wake na mali zao."

Hali ngumu ya maisha
Rais alikiri, "Ni kweli kuna hali ngumu ya maisha, na kukabiliana nayo ndiyo kazi tunayoendelea nayo kufanya kila siku."

"Tumeelekeza nguvu zetu na rasilimali zetu huko na mafanikio yanaonekana katika nyanja mbalimbali na maeneo mbalimbali, lakini akisisitiza,
"

Siku hizi haitwi Doctor Tena??

Huyu babu atuona sie wazee saaaana au??. Anatufundisha kufumbia macho ukeketaji wa Nchi??

Asilalamikie CDM anatakiwa kushughulikia kero za wananchi, Yeye anadhani tunamsapoti???

Kweli MJINGA hujifunza kutokana na Makosa yake Mwenyewe!!!!!!!!
 
mbona selemani ameipost hii topic mara nyingi?.....au kuna kitu anataka kusema?
 
Rais hapaswi kuwa mzushi hivyo. Anasema CDM wanaandamana kwa lengo la kuiondoa serikali madarakani? Nani anawaruhusu kuandamana kama malengo ni uhaini? Kama Mkuu wa Nchi anachukuakua hatua gani kuzuia maandamano yenye malengo ya uhaini? JK aache uongo - Rais mzima anakuwa mzushi ni hatari kwa usalama wa nchi.
 
Selemani sometimes huwa ananifanya nikumbuke ule mwimbo wa msondo uliokua unaitwa kaka selemani...
 
... ulevi wa madaraka una hangover isiyokwisha. Bahati mbaya sana mwisho wake ni pale walevi hao wanapokimbia makwao au wanapolipuliwa.. Angalieni tu walevi wengine walivyofanya. Latest, angalia ya Gadhafi. Bado nayakumbuka sana yaliyompata Nikolai Causescu. Hadi dakika ya mwisho alifikiri yuko ndotoni, ndoto mbaya ya kulipuliwa. Hata wale securitate wake aliowakirimu kwa maraha hawakumwokoa. It had just become overbearable. Arobaini ya mwizi!
Ukali wa maisha Romania enzi zile ni kama inavyoonekana kwenye failed states nyingine. Hautaofautiani na jehanamu yetu Tanzania. Ni mwehu tu anayethubutu kujigamba eti mafanikio yalopatikana ni makubwa mno na kwamba mwenye macho haambiwi ayaone!!!
Magonjwa ya akili yapo ya aina nyingi sana na majina yake kibao. Bado natafuta the appropriate one for this case.
 
Hoja hujibiwa kwa hoja sio na mkwara wala vitisho!!! Tumeona kwa makinda ss na rais ccm when will u ever learn!!
 
Back
Top Bottom