Real Madrid (‎Los Blancos) | Special Thread

Haikuwa rahisi, baada ya kuwa nyuma kwa goli mbili vijana wamepambana mpka wamerudi mchezoni, tumefungwa kutokana na makosa ya kiulinzi., Marcia na mwezie Vazquez wamekuwa sio watu wa kuaminika kwenye ulinzi, kiukweli kwenye upande wa full backs tuna upungufu mkubwa tu, acha tuone kama January litafanyika jambo.
 
Tumekaa bao mbili kwa Rayo kama sio.Real Madrid. Nafikiri hii tu haiko serious kabisa.
Marcia aligeuzwa kama mtoto mdogo, huku Vazquez anashangaa watu wapiga vichwa, ajabu sana.
Ni vizuri tumeweza kusawazisha.,
Sijui ni maelekezo ya Mwalimu, Rodrygo alikuwa anacheza kama mtu wa mwisho akisubiri juu mipira iende ila hakuwa anapata mipira, ila baada ya kufungwa nimeona anashuka chini kupandisha mashambulizi, kiukweli amekuwa na impact kubwa sana, ni bora akaendelea kutokea hivi hivi huku chini.
 

Vazquez wa msimu huu sio yule tuliemzoea, hayuko sawa kwenye marking huu ni wakati wa kutafuta full back ya kweli
 
Acheni lawama zenu za 'kiduwanzi'

Mbona tukishinda game haya mapungufu hamyasemi

Sio lawama mkuu, tukubali tu wachezaji kuna muda viwango vinashuka. Kama una kumbukumbu vizuri wakongwe wa golden era waliobaki ni Vazquez, Modric na Carvajal.
Hakuna tunachowadai, lakini Vazquez na Modric speed imepungua. Jukumu la kucheza fullback kwenye timu yenye long season kama Real Madrid lazima uwe solid
 
Acheni lawama zenu za 'kiduwanzi'

Mbona tukishinda game haya mapungufu hamyasemi
Lawana gani man, tuna mapungufu kwenye full backs msimu huu, si Fran Garcia wala Lucas Vazquez anayecheza vizuri., tumefungwa goli tatu zote ni mapungufu ya kiulinzi, ulitaka mtu atoe magnificent gani?
Tumekuwa na hii shida tangia msimu unaanza., so sio jambo jipya.
 
Tunashindwa kutumia hizi nafasi za hawa jamaa kufungwa, Atletico ndio ninaona wapo serious.

Ligi imekuwa ngumu msimu timu nyingi zina vijana wazuri. Unajua wachezaji wengi sasa hivi wanakuja kucheza la liga! Wanatukamia kila game mpaka tunaonekana wa kawaida, lakini mechi bado nyingi sana huko mbele tutakaa vizuri tu
 
Umepigwa kidude dakika ya 4' mpaka sasa ni ya 35' bado huna hata shot on target
Niliiwahi game, nikawa naangalia huku najiuliza, kwa huu uchezaji tuliwezaje kumkanda mtani goli nne na Bayern? Nafasi zinatengenezwa kama mia, ila hakuna anaetaka kufunga.

Huu msimu Atletico akiwa na consistency, anaweza chukua ndoo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…