Real Madrid (‎Los Blancos) | Special Thread

Tatizo beki aisee, na hivi Cancelo na Grealish ndani ya nyumba. Tuna kazi kwelikweli!
Siku za hivi karibuni tumekuwa na shida sana kwenye upande wa Ulinzi, Militao na mwenzie Alaba wamekuwa na makosa ya kujirudia sana, wakati msimu unaanza walikuwa na tatizo hili baadae wakajirekebisha, ni matumaini yangu kuwa wakajirekebisha tena wakati huu tunakabiliwa na mechi ngumu na muhimu.,
Kuwepo kwa Grealish na Cancelo wala halinisumbui kichwa, ishu ni sisi kucheza kwa uangalifu mkubwa haswa upande wa ulinzi, lakini pia uwepo wa Casemiro unaweza kutusaidia kiulinzi pia, ninajua tutakuwa na game plan nzuri Sana, HalaMadrid, #Hasta El final
 
Bado msimu mmoja tuone kama wata deliver. Natamani waendelee kupewa muda zaidi wa kucheza. Nafikiri hizi game zilizobaki laliga zinawatosha.

Wish nije nione timu iko na cebalos, Valverde, camavinga, rodrigo, vin
Mpaka walipofikia sio mbaya sana,ila ni ukweli acha tuone msimu ujao utakuwa vp kwa hawa vijana, Ceballos ninaona ameimarika sana siku za hivi karibuni kwenye nafasi alizopewa kucheza, ninadhani club itambakisha, ana uwezo mzuri tu, tatizo ni kutengeneza hatari kwa adui ndio bado hilo eneo hajalifanyia kazi, ila dirty game pale kati anaiweza.

Camavinga huyu ni mtu na nusu, akiepuka kufanya makosa na kuepuka kadi za njano basi atakuwa na wakati mzuri sana.,

Rodrygo yupo poa huyu kijana, shida ni kwamba na yeye anakuwa anacheza vizuri sana akitokea wing ya kushoto, tatizo eneo hilo yupo Vinicius Jr ambaye ameonyesha uwezo mkubwa sana, so anacheza wingi ya kulia hivyo hivyo na anajitahid sana japokuwa sio eneo lake sahihi.,

Vini Jr, huyu amekuwa, Sina haja ya kumwelezea.
 
Alaba anaweza ukosa mchezo wa kesho. Nacho mzee wa kuchomesha atacheza kama mbadala. Tunahitaji kucheza kwa kujilinda tukifanya mashambulizi ya kustukiza ya uhakika.
Tukiwa na casemiro kroos na modric huku valvelde akicheza kama mid field ya juu namba kumi kazi ya kiungo itakuwa imeisha.
Kisha baadae dogo camavinga aingie
 
Kama kocha atakuja kusoma huu ushauri basi mnaenda kuoga magoli mengi ,kwa hiyo mnataka kupark bus ,
mtasakwa kokoto mliko ,mashimoni ,chini ya uvungu ,kitandani ,kila vitobo movement za Mahrez ,kDB ,benardo Silva ,foden zitawatafuta mpaka mtaachia tu goli
 
Yeah, Alaba amejumuishwa kwenye kikosi ila kwa hali aliyonayo hataweza kucheza hiyo kesho, kwahiyo hapo tupo na Nacho., hopefully atakuwa na mchezo mzuri.

Casemiro atakuwepo hiyo kesho, so mtihani kwa Ancelotti ni kwamba aanze na Rodrygo ama Valverde!? Hicho ni kitendawili ambacho atakitegua Mzee mwenyewe.
Nilitamani Camavinga aanze badala na Kroos, ila sioni hilo lilitokea, na pia ninaona Valverde akianza mbele ya Rodrygo.! Kwa vyovyote vile Tumaini ni moja tu USHINDI.
#HALAMADRID
 
Binafsi naona Camavinga anakuwa ni mzuri akianzia benchi,ni kama Ozil enzi zile...hapo kwa Nacho ndo tumbo joto,hope atafanya vyema...
 

Real Madrid vs Manchester City - Official line-ups​

Real Madrid XI: Courtois; Carvajal, Militao, Nacho, Mendy; Casemiro, Kroos, Modric; Valverde, Vinicius, Benzema
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…