Tatizo linaloikabili Madrid kwa sasa ni kutokuwepo kwa Christiano ronaldo. Hili wengi wanaogopa kulisema. Zidane ni kocha wa kawaida kabisa, kama walivyo kina Moyes, Pulis, na wengine wa aina hiyo.
Mafanikio yake kwa % kubwa yalibebwa na Mnyama mkatili CR7. Kitendo cha kurudi kuifundisha baada ya kujiuzuli alikosea sana. Alishindwa kusoma nyakati. Ameamua kuichafua cv yake ya ukocha ambayo kwa haki kaandikiwa na ronaldo.
Huu msimu sijui nini kitatokea. Ila nachoamini, hamwezi kuwa juu ya barcelona, Atletico de madrid, na Sevilla. Kwa maana hiyo ni kwamba ubingwa kwa msimu huu hamwezi kupata.