Nakumbuka baada ya game ya kwanza na Madrid kushinda 2-1, ribery aliandika kwenye page "we are still the champions of three titles" alafu Matt humels yeye akaandika "it is still far from over".
Na kweli Leo majamaa yamesimamia maneno yao sio kwa msako ule kipindi cha pili. Majamaa yalitaka kufia bernabeu ilimradi yaende fainali. Hata Barcelona hajawahi kupata corner nyingi hivi dhidi ya madrid hali ilikuwa mbaya kiukweli sema combination murua ya Ramos na Varane imesaidia sana na hawakuwa na papara yoyote.
Pia pengo la isco limeonekana pakubwa sana, hakuna mtu aliyekuwa ana weza kukaa na mpira mguuni tofauti na modric wakati Bayern walikuwa na watu watatu wanaomiliki mpira kwa muda mrefu alcantara,ribery na James ndio maana walikuwa wanafika langoni kila mara kwa urahisi. Naona Gareth bale nae benchi limemzoea anacheza kama mchezaji wa benchi kabisa.
Cha mwisho ninachoweza kusema hii ndio ilikuwa fainali kwa maana kwamba Leo ndio tumepata bingwa. Samahanini mfalme Ngwamba na ndugu zako tatizo timu yako haina sub ndio maana nime wa write off