Real estate agent (wakala wa majengo)

Real estate agent (wakala wa majengo)

Joined
Nov 28, 2010
Posts
21
Reaction score
5
REAL ESTATE AGENT (WAKALA WA MAJENGO)

Wakala wa Majengo (Estate Agent), hawa ni wataalamu wa soko la nyumba ambao ni muhimu katika kukutafutia nyumba ya stahili yako na ndani ya bajeti yako.

Aina za Wakala wa Majengo

1. Wakala wanataaluma

Wapo wale ambao taaluma zao zimejikita katika uthamini na usimamizi wa Ardhi ambao husajiliwa na Baraza la Wapimaji Tanzania (National Council of Professional Surveyors) na wanaendesha kampuni za Ushauri.



2. Wakala wafanyabiashara

Wapo ambao wameanzisha biashara ya Uwakala kwa kujiandikisha kwa Afisa Biashara wa Mkoa husika, nao hujitangaza kwenye magazeti, vipeperushi na kwenye Maonyesho mbalimbali kama vile sabasaba n.k.

Huduma zitolewazo na wakala wa majengo

Kwa ujumla kazi kubwa ya Wakala wa Majengo ni kutoa taarifa zinazohusiana na upatikanaji wa nyumba inayopangishwa au kuuzwa.

Kazi za Wataalamu wa uuzaji wa nyumba ziko kwenye mafungu matatu:

1. Kutafutia wateja nyumba ya kupangisha au kununua

Wakala hukusanya taarifa katika maeneo yao kuwajua wanaouza na wanaotafuta kununua.


2. Kujadiliana bei kwa niaba ya mnunuzi

Wakala anakuwakilisha katika kujadiliana au kupatana bei na mwenye kuuza. Mara nyingi Wakala atakuongoza katika mazungumzo.


3. Kushuhudia mkataba wa mauzo

Mara chache Wakala wa Majengo anaweza akakusaidia hadi kufikia ununuzi na kushuhudia mkataba unasainiwa.



Mambo ya kuzingatia kabla ya kuchagua wakala wa majengo

Kuna maswali 11 ya kujiuliza ili kujiridhisha kwa wakala:

1. Uzoefu na muda katika biashara yake;

2. Kazi ya uwakala ni kazi yake ya kudumu;

3. Uzoefu wa biashara hii katika maeneo ya makazi uliyochagua;

4. Mafanikio yake katika kazi ya uwakala;

5. Ufahamu wa bei za nyumba ambazo amekua akiuza;

6. Uzoefu katika nyumba za kundi unamotafuta;

7. Ungependa kujua kama uzoefu wake umeelemea zaidi kwa wanunuzi au wauzaji;

8. Ungetaka ufahamu kama wakala huyu anaaminika na anazingatia kanuni ya kuwa upande mmoja yaani ununuzi;

9. Unataka kufahamu ana uwezo gani wa kuwafikia wauzaji;

10. Ungetaka Wakala akuthibitishie uwezo wake walau kwa kukupa majina ya wateja wake watatu ili uweze kuwasiliana nao ili kujiridhisha;

11. Ungetaka ufahamu pia kama ukiingia naye mkataba, mkataba huu utachukua muda gani na je utajumuisha uhushwaji wa hati (Conveyancing)?.


georgepeter@terranova.co.tz
 

Attachments

Asante sana mkuu kumbe kuwa wakala wafanyabiashara sio lazima kwenda brela? Au kusajiri biashara halimashauri?
 
Mimi nataka kuuza nyumba yangu mbezi beach, nifanyeje unipatie mteja? Nataka kuhamia mkoani.
 
Umeeleza vizuri sana.
Nina shida na wewe PM mkuu,naomba ukisoma text hii usisahau kupita PM kuna text yako
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom