PreGE2025 REA yakamilisha miradi ya umeme vijiji 5,259

PreGE2025 REA yakamilisha miradi ya umeme vijiji 5,259

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Nipe Maji

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2025
Posts
335
Reaction score
190
Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (Rea), Mhandisi Hassan Said ametangaza kukamilika kwa miradi minne mikubwa ya umeme inayolenga kuleta nishati katika vijiji 5,259, ikijumuisha vijiji 4,071 na vitongoji 188, katika awamu ya tatu, mzunguko wa pili.

Miradi hii ni sehemu ya juhudi za Serikali kuhakikisha vijiji na vitongoji vingi vinapata huduma ya umeme kama sehemu ya majukumu yake ya kuunga mkono maendeleo ya maeneo ya vijijini.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao cha Baraza la Wafanyakazi la Rea, Mhandisi Said alieleza kuwa miradi hii ni matokeo ya ombi la viongozi wa serikali kuu linalohimiza kufikishwa kwa huduma ya umeme katika maeneo hayo, ili kuboresha maisha ya wananchi wa vijijini.

"Miradi hii ni hatua kubwa katika kufikia lengo letu la kuhakikisha nishati inafika vijijini na maeneo yaliyokuwa hayafikiki. Tunajivunia mafanikio haya, na tutaendelea kufanya juhudi kuongeza maeneo yanayohudumiwa," alisema Mhandisi Said.

Mbali na miradi hiyo, Rea pia imeanzisha mradi mwingine wa kupeleka umeme katika vitongoji vipatavyo 9,000.

Hatua hii inatarajiwa kuongeza wigo wa umeme na kupunguza changanmoto za upatikanaji wa nishati kwa wananchỉ wa maeneo hayo.
1743243849442.png
ea ucha
 
Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (Rea), Mhandisi Hassan Said ametangaza kukamilika kwa miradi minne mikubwa ya umeme inayolenga kuleta nishati katika vijiji 5,259, ikijumuisha vijiji 4,071 na vitongoji 188, katika awamu ya tatu, mzunguko wa pili.
Kuhesabu idadi ya vijiji na vitongoji badala ya idadi ya kaya ni ujinga.

Lengo ni kuunganisha vijiji au kaya? Umeme siyo barabara kwamba lengo liwe kuunganisha vijiji.

Kuna vijiji umeme umeunganishwa kwenye shule na zahanati tu,kaya hazifiki hata 50.
 
Back
Top Bottom