Re. Kiingereza..na dada zetu wa ki tz

Naunga mkono hoja,ofisini kwetu kuna kabinti kanakaribia kumaliza ofisi sababu ya waghana niliowaleta kwenye project kwa kweli ni noma.
 
mi huwa wananichekesha sana wanapochanganya kiswahili na kizungu, kuna mmoja alisema NAPENDELEA CHIPS ZILIZOKONFYUZIWA NA MAYAI
 
hata mm napendaga yan....mboy akija anabonga kithungu nampendajeee....lkn kuongea nae tu co mambo mngn ....kuongea kiswahl mfululio inaboaje....swaenglish ndo mpango mzimaaaa..
 
NAPINGA HOJA...

hizo ni few exceptional cases na nadhani ni for few tanzanian girls/ladies wanaopata nafasi ya kukutana na hao foreign experts..UKIJA HUKU KWETU TANDALE NA KWA MAMA ZAKARIA KINYAMALA MWENDO NI KISWAHILI NA WAGENI WA KICHINA WANAISHIA KUJICHUA MAANA BILA KISWAHILI HUPATI MZIGO...

samaki mmoja akioza hasa baharini haimaanaishi wote waliomo baharini wameoza na hawafai.....

BIG UPS DADA ZETU KWA KUENDELEA KUTUPATIA HUDUMA HATA KAMA HATUJUI KIZUNGU.
 
The grass always look greener on the other side.Just give them what they are missin' an' everythin' will b Ok.
 
Ni kweli siku hizi watu wanapenda kuongea english which is gd. Mi pia napenda mwanamke awe anajua english coz maneno mengi ya kimapenzi au niseme kimahaba hayapendezei kwa kiswahili
 
ushamba!!!! na kukosa umahiri wa lugha yao....
Mie nikikutokea na kiswahili changu.....wallah utalegea mwenyewe kwa maneno yenye utamu masikioni na moyoni yananata...
Kingreza chenyewe cha "ze nibu za peni za dog anda ze trii" kinaudhi
 
unajua dada zetu cjui ubongo gani wanatumia kufanya maamuz ya yale wanayokutana nayo,yaan muda mwingine unaweza kuzubaa unawaza the way wanavyoact,asa cjui kiingereza ndio ndoa,dah kazi ipo kulea hivi viumbe
 
Nimegundua dada zetu wa ki Tz wanavutiwa sana na wanaume wanoongea Kiingereza...haijalishi wa nchi gani.
Pia huwa ni vigumu kukataa kama wakitongozwa kwa kidhungu.... ndo maana wakaka wa kikenya wanatumalizia dada zetu... mfano hai ni wadada wengi wanaofanya kazi ofisi moja na wakaka wakenya eti nao wana lafudhi ya kikenya kwenye kiinglish chao...au kama kuna mgeni ambaye hajui kiswahili ofisini basi utakuta anajistorisha na huyo mkaka kwa kizungu kwa sauti alafu utakuta anacheka hata kama kitu hakichekeshi.
wakaka wa kikenya wanamaliza wadada zako?. sasa unataka wewe ndo uwamalize hao dada zako?. mimi ningekuwa na uwezo ningefanya kampeni duniani kote kuwa wanaume waje tanzania wajenge mapenzi na dada zetu. sisi wenyewe ( wanaume wa tanzania) hatuwatoshi hawa wadada, bado unazuia wageni, unataka nini? kuwa na moyo wa upendo kijana , wapende dada zako, wape furaha ya kuwa na wanaume
 
washamba kweli....mi nafanya kazi na wachina....nikiongea kiswahili kama kichina....nikicheka ni kichina tupu....nikitembea ndo utadhani shaolin....nini kizungu bana....
 
hiyo sio kwa wanawake tu hata vijiweni utakuta mtu anapiga stori ili aonekane yuko sahihi na kuwazuga malofa wenzie anatia kiingereza na kwa ulofa wao wale jamaa wanamuona msomi kweli kweli.we jiulize tu mtu hawezi kusema nakupenda eti anaona aibu lakini akisema i love you anajiamiiini.mwisho, tatizo watanzania wamejiaminisha kwamba ukijua kingereza basi umesoma.
 
kuna mmoja alikuwa ndo ameingia tu form one kipindi hicho mimi nipo form two sasa kule kujifanya anajua akawa anawaaga wenzie ikawa hivi ''hallow dears tomorrow morning i just coming now''akimaanisha ataonana na wapendwa wake kesho yake.
 
Mambo ya kuongea kizungu, kwa waafrika ni kuonesha kama umestaarabika na ni usomi.
 
Back
Top Bottom