Re: Dr kafumu amkataa jaji mary shangali

Karikenye

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
564
279
Dk. Kafumu amkataa jaji


na Mustapha Kapalata, Nzega


amka2.gif
KATIKA hali isiyo ya kawaida jana Mbunge wa Jimbo la Igunga Dk. Peter Kafumu alimkataa Jaji Mary Nsimbo Shangali kuendelea kusikiliza kesi ya kupinga matokeo yaliyompatia ushindi mbunge huyo katika uchaguzi mdogo wa Igunga uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana.
Akisoma barua ya Kafumu mbele ya mahakama hiyo, Wakili wake, Antony Kanyama, alisema kuwa mteja wake hana imani na jaji huyo kwa kuwa baadhi ya maamuzi yanakwenda visivyo.
Alisema imani na jaji huyo imetoweka kwa madai kwamba amekuwa akiwadhalilisha na kuwatukana mashahidi wa upande wa utetezi, na kutoa mfano wa shahidi (DW14), ambapo amedai alichukua nafasi ya mawakili wa mdai kwa kuwahoji maswali mashahidi wake badala ya kutaka ufafanuzi juu ya maelezo yao.
Aliitaja sababu nyingine kuwa ni tabia ya jaji huyo ya ukali pasipo sababu dhidi ya mawakili wa utetezi kila walipohoji mashahidi wa upande wa mdai.
Aliitaja sababu nyingine kuwa ni kile alichodai kuwa ni kitendo cha jaji huyo kuwanyima mawakili wa upande wa utetezi waliomba kupewa nakala ya mwenendo wa shauri hilo, mara tu usikilizaji wa kesi kwa pande zote ulipokamilika ili kuwasaidia kuandaa hoja za majumuisho.
Wakili Kanyama alidai kuwa kutokana na hali hiyo mashahidi wake muhimu wamekataa kuja kutoa ushahidi kwa kuogopa kudhalilishwa.
Hata hivyo, wakili Prof. Abdallah Safari anayemtetea mlalamikaji, Joseph Kashindye, anayepinga ushindi wa Kafumu, alisema kuwa maombi hayo si ya msingi, na akatoa mifano mbalimbali ya kesi kama hizo na kuongeza kuwa kama wanaona hali ni mbaya wasubili wakate rufaa mara baada ya kesi hiyo kuhukumiwa.
Baada ya kupitia pande zote mbili na kusoma kwa muda jaji huyo alitupilia mbali ombi hilo la Kafumu na kusema kuwa kesi hiyo inaendelea kusikilizwa kwa kufuata taratibu na kanuni za kimahakama.
Jaji Mary alisema hakuna sababu za msingi zilizotolewa na kwamba maelezo yanayolalamikiwa yanaweza kufanywa katika rufaa.
Pamoja na kutupilia mbali ombi hilo, Wakili Kanyama aliiomba mahakama hiyo kuahirisha kesi hiyo mpaka aongee na mteja wake kama ataendelea ama vipi.
Katika hatua nyingine, Jaji Mary ametaka mahakama iachwe uhuru na isiingiliwe katika mwenendo wake, kwa vile hadi sasa haijabainika nani atakuwa mshindi katika kesi hiyo kwani bado ushahidi unaendelea kusikilizwa kwa mujibu wa madai na upande wa serikali.
“Naomba muiachie mahakama iendelee kusikiliza kesi hii na mheshimu mahakama kama jinsi tulivyoapishwa,’’ alisema Jaji Mary.

Source: TANZANIA DAIMA

 
Back
Top Bottom