John John Msakuzi
JF-Expert Member
- Jun 17, 2025
- 279
- 99
===
Akiongea na wanahabari mkuwa mkoa wa Tabora amesekuwa Chini ya Rais Samia uzalishaji wa asali Tabora umeongezeka kutoka tani 1,800 mwaka 2020 hadi Tani 2,000 mwaka 2025
Kupitia filamu ya Royal Tour iliyoanzishwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mkoa wa Tabora umepata mafanikio makubwa katika sekta ya utalii, ikiwemo ongezeko la watalii wa ndani kutoka 1,283 mwaka 2020 hadi 7,397 mwaka 2025.
Mapato kuongezeka kutoka TZS6.17milioni hadi TZS26.62milioni. Viwanda 4 vya kuchakata na kufungasha asali vimejengwa huku uzalishaji wa asali ukiongezeka kutoka tani 1,868.6 hadi tani 2,002.48. Aidha, misitu ya vijiji imeongezeka kutoka 6 (ekari 11,952.5) hadi 37 (ekari 330,780.75) na miti milioni 1.5 imepandwa, sawa na asilimia 80 ya lengo la Serikali