Libya
JF-Expert Member
- Nov 11, 2016
- 783
- 1,918
------------
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Paulo Makonda amesema kuwa kwa fedha ya kitanzia ni kipato cha mtanzania kuwa na dola milioni mbili mpaka tatu kwenda mpaka milioni tisa mpaka kumi, ameongeza kuwa benki ya dunia imekubali kuwa Tanzania imefika kwenye hivyo vigezo vya uchumi mdogo wa kati.
Mh. Makonda amesema kuwa zipo faida nyingi kwa kufikia hatua hiyo, nazo ni:
- Taifa linaondoka kwenye kuwekewa vikwazo linapotaka kujipangia mambo yake ya kiuchumi.
- Taifa linakuwa na uwezo wa kujitegemea kutoka kwenye maisha ya kuwa ombaomba na kuwa na uwezo wa kujitegemea.
- Taifa lina kuwa na uwezo wa kukopa na kukopesheka kwa sababu uchumi wake unakuwa imara na una sifa ya kulipa na ndio maana unapata nafasi ya kutangazwa kuingia kwenye Uchumi wa kati.
Mh. Makonda aliendelea kwa kumuita Mh. Zitto Kabwe kuwa ni mtu mbishi, na kuwa Mh. Zitto anampango wa kuandika barua kwenda benki ya Dunia kupinga Benki ya Dunia kuitangaza Tanzania kuingia Uchumi wa kati na kuwa miongoni mwa nchi tano duniani zilizoingia kwenye uchumi wa kati mwaka 2020 tena kwenye kipindi ambacho uchumi umetikisika kwa mataifa mengine lakini Tanzania imebaki kuwa salama.