RC Mwanza atumbua watano Ilemela

Zurie

JF-Expert Member
Jul 6, 2014
2,005
5,550
Mkuu wa wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella amewasimamisha kazi maofisa watano wa Halmashauri ya Wilaya ya Ilemela kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha za umma na matumizi mabaya ya madaraka.

Akiwa katika ziara ya siku moja ya kujitambulisha wilayani Ilemela leo, Mongella ameagiza kushushwa cheo kwa ofisa wa ardhi wa wilaya hiyo, Anicet Rweyemamu kwa tuhuma za kushindwa kusimamia watumishi walio chini yake wanaotuhumiwa kupokea Sh12 milioni kutoka kwa mwananchi mmoja aliyekuwa akitaka ardhi, lakini hajapewa hati hadi sasa.

Wengine walioangukiwa na rungu la mkuu huyo ni Debora Tongora ambaye pamoja na Alex Chigulu wanatuhumiwa kupokea fedha hizo kutoka kwa wananchi kwa ahadi ya kuwapatia viwanja.

Wakati Tongola tayari amefunguliwa mashtaka dhidi ya tuhuma hizo, Chigulu amehamishiwa mkoani Singida lakini Mongella ameagiza arejeshwe Mwanza ili afikishwe mahakamani.

“RPC wasiliana na mwenzako wa Singida ili huyo mtumishi atiwe mbaroni muda huu na kesho arejeshwe Mwanza kukabiliana na mashtaka dhidi yake. Hatuwezi kuwavumilia watumishi wanaoharibu sehemu moja halafu wanakimbia uhamisho kwenye maeneo mengine,” amesema Mongella

Ofisa uvuvi wa Kituo cha Kirumba, Ivon Maha ameshushwa cheo huku Peter Revelian akiondolewa kutoka nafasi ya mweka hazina.

Watumishi hao wa Idara ya Uvuvi wameondolewa madarakani baada ya kutuhumiwa kuhusika na upotevu wa zaidi Sh40 milioni zilizotokana na kodi na ushuru.

Awali, Mkuu wa wilaya ya Ilemela, Manju Msambya alimweleza Mongella kuwa wilaya hiyo tayari imetengeza madawati 7, 200 kati ya 29, 000 yanayohitajika.

“Wilaya yetu inakabiliwa na changamoto ya uhaba wa walimu katika shule za umma na tayari tumewasilisha maombi ya walimu wapya,” amesema Msambya

Meya wa Manispaa ya Ilemela, Renatus Mulungi alimuahidi mkuu huyo wa mkoa kuwa baraza lake litaongeza juhudi katika usimamizi wa utendaji kwa watumishi wa halmashauri hiyo.

Chanzo: Mwananchi
 
Sasa naona naye ameanza kuturudisha tulikotoka yaani mtu anafanya ufisadi halafu eti anashushwa cheo? Rais alishasema ni kumalizana palepale hakuna cha kuhamishiwa pale wala kushushana cheo ni kutumbua 100% sasa unamshusha je kesho akipandishwa tena na kashadisadi?
 
WAKUU WA MIKOA WAJUE MIPAKA YA MAMLAKA YAO.! SIYO KULETA SIASA NA MISIFA YA KIJINGA! WEWE KUAMBIWA HAPO TU TAYARI UMEONA MTU ANATAKIWA ASHITAKIWE KESHO! NDIYO MAANA TAKUKURU WANASHINDWA KESI. WAMEKUWA WANAAMUA TU WAMPELEKE MTU MAHAKAMANI HATA KAMA WANAJUA HAKUNA KESI KWA KUWA TU WAMEAMRISHWA NA MWANASIASA FULANI. JAPO HANA MAMLAKA YA KUWAAMURU TAKUKURU WALA OFISI YA DPP KUMPELEKA MTU MAHAKAMANI. ULIMBUKENI WA MADARAKA HUO!
 
ENZI HIZO ILA KWA MAGUFULI KAMA KAMBA ATAENDELEA KUKAZA TAIFA LITANYOOKA
 
ENZI HIZO ILA KWA MAGUFULI KAMA KAMBA ATAENDELEA KUKAZA TAIFA LITANYOOKA
TAIFA LINAHITAJI MIFUMO IMARA MKUU! NA KATIBA MPYA YA MAANA NDILO JIBU.! KATIKA NCHI HII NI BORA UKAWA MWANASIASA KULIKO KUWA MTUMISHI WA KAWAIDA WA UMMA. MAANA UFISADI WA CCM UTATUPIWA WEWE! ANGALIA YA LUGUMI NA CHARLES KITWANGA YAMEDUMU KWA MUDA GANI,!! HALAFU ANGALIA YA WILSON KABWE, MTU KAROPOKA TU, KABWE KAISHAFUKUZWA!! ANACHOSUBIRI KWA KITWANGA NI NINI?!
 
WAKUU WA MIKOA WAJUE MIPAKA YA MAMLAKA YAO.! SIYO KULETA SIASA NA MISIFA YA KIJINGA! WEWE KUAMBIWA HAPO TU TAYARI UMEONA MTU ANATAKIWA ASHITAKIWE KESHO! NDIYO MAANA TAKUKURU WANASHINDWA KESI. WAMEKUWA WANAAMUA TU WAMPELEKE MTU MAHAKAMANI HATA KAMA WANAJUA HAKUNA KESI KWA KUWA TU WAMEAMRISHWA NA MWANASIASA FULANI. JAPO HANA MAMLAKA YA KUWAAMURU TAKUKURU WALA OFISI YA DPP KUMPELEKA MTU MAHAKAMANI. ULIMBUKENI WA MADARAKA HUO!

Maafisa utumishi wanakazi. Uzuri maamuzi hayo ni kumyanganya sana sana ofisi. Kushushwa cheo! Thubutu!
 
Sasa hivi ukiwa serikalini lazima kichwa kiwe kinakuuma..maana hajui kesho yako nilini..
Ni mwendo wa kufukuzana tu.
Kama huwaga hujishughulishi na mambo ya ubadhilifu na mirushwa ya hovyo hovyo, mbona wala kichwa hakiumi na badala yake unachekelea tu kwani waliokuwa wanakutambia kwa uadilifu wako sasa wanaipata fresh toka kwa Magufuri na wasaidizi wake. Hadi raha!
 
Back
Top Bottom