RC Mwanri, hili kama ni lako tafakari upya

LENDEYSON

JF-Expert Member
Sep 27, 2013
2,996
2,659
Nikiwa mkazi wa mkoa wako, na manispaa ya Tabora, na nikiwa mmoja ya wanaokuheshimu kwa kazi kubwa na kujitolea kwako kwa mkoa uliopewa, niseme tu, changamoto ya eneo la Ipuli hususani Freemason au kwa Sonda sio hao wanaolima Majaruba ya Mpunga.

Tabora, kama ilivyo maeneo mengi ya nchi, kuna wataalamu ambao hawakupaswa kabisa kuwepo kwenye ofisi za umma, mojawapo ni Maafisa Ardhi walioshiriki zoezi la upimaji na ugawaji viwanja Ipuli. Historia ya eneo hilo inafahamika vizuri hasa linapokuja suala la mvua, wataalamu wako walipaswa kuweka miundombinu itakayokabiliana na hali kama iliyopo sasa.

Wataalamu wa TARURA nao walipaswa ku oversee adha watakazopata wakazi wa maeneo hayo baada ya ujenzi wa miundombinu na kuweka mifumo kukabiliana na tatizo, badala yake kazi yao imekuwa kukatiza mitaa hiyo kila mvua zinaponyesha bila kusaidia wala kufanya lolote.

Cha kusikitisha, kama kawaida, katika hili mheshimiwa, serikali yako imeona tatizo ni hao wanaojitafutia chakula kwa kulima Majaruba ya Mpunga kama walivyozoea siku zote. Tumeacha ku deal na real problem, tumeanza kuwakamata kina mama wanaokutwa wakilima, nimesikitika sana leo asubuhi kuwaona mgambo wa Manispaa wakiwa wanawakamata waliokuwa wakilima, is this the solution?

Mheshimiwa Mwanri, naamini katika hili, suluhu ya kudumu itapatikana na kwa ninavyokufahamu, hakuna atakaeonewa.

HERI YA MWAKA MPYA 2020.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duuh,kama ni kweli awamu hii tumejikamata,majaluba ni ya kwao na wanalima miaka yote,wale wananchi serikali ya mkoa imewapa viwanja kwenye majaluba,ajabu ya 2020 wenyemajaluba wanakamatwa ,wakalime wapi?au uwanja wa Mwinyi?
 
Back
Top Bottom