RC Mghwira aagiza mkuu wa kituo cha polisi kuchukuliwa hatua

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,879
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira ameagiza mkuu wa kituo cha polisi Holili Wilaya ya Rombo pamoja na askari wawili kuchukuliwa hatua kwa madai ya kuzembea na kuruhusu pikipiki kutoka Kenya na Tanzania kusafirisha mahindi kwa magendo.

Amechukua uamuzi huo leo Ijumaa Aprili 2, 2021 baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika mpaka wa Holili wilayani Rombo na kushuhudia shehena ya mahindi yakiwa yamepakiwa kwa ajili ya kusafirishwa nchini Kenya.

Mahindi hayo yamekuwa yakisafirishwa kwa magendo baada ya Kenya kuweka katazo la mahindi kutoka Tanzania kuingia nchini humo kwa madai ya kuwa yana sumu kuvu.

"Jana nilikuja hapa mchana nikauliza kama kuna kitu kinaendelea hapa Holili wakaniambia hakuna kitu baada ya mizigo yetu yote kurudi Tanzania. Nilipoambiwa hivyo sikuridhika nilirudi ofisini nikafanya kazi zangu lakini baadaye nikawaambia watu wangu watangulie wakaone hali ilivyo. Walipofika wakaniambia vijana wa bodaboda wanafanya kazi kama mchwa ya kusafirisha mahindi kwa kutumia njia za panya kupeleka Kenya.”

“Cha kushangaza askari anafika kwenye lile eneo na kuwaambia wale bodaboda waondoke. Kama askari wetu ndio mnatugeuka na kufukuza watu kwa kuwaambia ondokeni na watu hao wanatuvunjia sheria, kupoteza mapato na kutuharibia biashara..., kwa utaratibu huu naomba askari hawa pamoja na mkuu wa kituo hiki wachukuliwe hatua za kinidhamu," amesema Mghwira.
 
Yaani watendaji wa jiwe wote wanapima kina Cha Mama samia, tuone hili litaishaje?
 
Mama Mghirwa jaribu kushauriana na mama Samia, watu hawawezi kukaa na mizigo yao kipindi chote hicho mpaka iwaozee, hata wewe usingekubali hasara ya mwaka mzima.

Kuna mvua zimeanza sasa, watu wanategemea waende shambani tena, wavune, wakutane na mashehena ya mwaka jana mpakani, kuna kitu inaitwa FIFO, first in first out kwenye inventory keeping, wajanja wanakwepa hilo.

Badala ya kuwakamata hao maafisa, watafutieni hao wafanyabiashara njia itakayokuwa win win situation, vinginevyo hata wewe ungefanya hivyo hivyo.
 
Weledi ni jambo muhimu sana hivi masuala ya kuingiza bidhaa au kutoa bidhaa nje ya nchi jukumu hilo ni la nani? Uhamiaji,Polisi na TRA? Hivi makubaliano ya Nchi za Afrika Mashariki kuhusiana na bidhaa zinazozalishwa ndani ya EAC yanafahamika vema?

Hivi wanasiasa bila kuwashambulia Polisi hawawezi kuthaminiwa na wananchi?

Naona kama Utendaji kazi wa Serikali unahitaji kuboreshwa mfumo wa kutoa hukumu kwa jazba ubadilishwe kila mkuu apewe job discription yake na aitendee haki. Naunga mkono hoja ya Serikali kuwa na coordination.
 
hapo Holili maisha yalivyo tight, vijana tukatae mzigo wa magendo tena mahindi na siyo miraa, na kwa taarifa sijawahi ona border ngumu kama holili bora namanga na tarakea, askari wenyewe hapo wanafanya kazi kiugumu njaa kali sana hapo Taveta kumepauka mpaka voi amna kitu.
sasa mnaleta siasa kwenye maisha ya watu aisee.
 
Weledi unahitajika hapa kutatua hili kuona ni vipi biashara inaendelea na mapato tunapata katika hali kama hii ya kuzuiwa hayo mahindi vinginevyo magendo hayataisha hata ukiwachukulia hatua wote hapo watu hawana pesa na uchumi wanao
 
Back
Top Bottom