RC, Mbunge, DC majembe shambani Ludewa, mfano kwa vitendo

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,883
6,883
Enzi za kumwaga sera majukwani zimeshapitwa na wakati. Tunataka viongozi wanaofanya kazi kwa vitendo, si kutandikiwa mikeka wanapopanda miti kwa ajili ya picha, ila wazame kwenye tope na kuchimba mashimo ya kupanda kahawa. Kiongozi akiingia jikoni avae aplon, na akiwa michezoni vulana za michezo. Tumechoshwa na usanii wa majukwani.

DSCF8091.JPG
DSCF8125.JPG

Picha Kushoto:
Mkuu wa mkoa wa Iringa Dkt Christina Ishengoma (kulia) akishirikiana na viongozi na wanachama wa kikundi cha umoja Mawengi kinachojishughulisha na uoteshaji wa miche ya kahawa kupalilia kahawa jana kushoto kwake ni mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe, na mkuu wa wilaya ya Ludewa Geogina Bundala pamoja na wanachama wa kikundi hicho

Picha Kulia:
Mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe kushoto na mkuu wa mkoa wa Iringa Dkt Christina Ishengoma kulia wakitazama shamba la kahawa na mkulima wa kijiji cha Mawengi

DSCF8095.JPG
DSCF8180.JPG

Picha Kushoto:
Mkuu wa mkoa wa Iringa Dkt Ishengoma aking'olea nyasi mche wa kahawa,

Picha Kulia:
Makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya Ludewa MOnicha Mchilo ,mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe na mkuu wa mkoa wa Iringa Dkt Ishengoma wakitazama mashine ya kukoboa kahawa kata ya Mawengi
 
Viongozi wengi nimegundua wanakosa chachu, kama tukiwa na wabunge walao robo ya tulio nao watendaji kama Filikunjombe, naamini inaweza kuwa chachu ya kuumusha wengi kuiga. Tazama hapa hata Mkuu wa Mkoa na Wilaya wamejumuika naye katika kushiriki shughuli za maendeleo ya wanakijiji cha Mawengi mkoani Njombe wilaya ya Ludewa, kule alikokwenda karibuni Rais Kikwete kufungua mradi wa umeme uliojengwa na Kanisa Katoliki.
 
Waigizaji tu hawa, Shambani huendi na suti wala huchomekei, kama wewe si mkulima danganyika!

Ingekuwa maigizo wangetandikiwa kanga au mikeka kama baadhi ya viongozi wanavyofanyiwa wanapojifanya wanashiriki upandaji wa miti, huo ndio usanii wa maigizo, lakini hii ya kushika jembe na kuzama topeni huku waking'oa nyasi na kuzikung'uta kwa mikono vigumu kunisakikisha kwamba ni fani ya uigizaji. Bora tu tuungane kuwapongeza, maana hata Nyerere ndivyo alivyokuwa na hulka ya kushiriki maendeleo ya wananchi.
 
Well said. Uliona wapi watu wanaenda shambani kulima wakati kuna wengine nyuma yao wamesimama tu hawalimi wala hawana majembe? Mbwembwe za picha tu hizo.

Hawa viongozi hawakutembea na majembe ya kwenda kulima kijijini Mawengi, ila walipopita na kukuta hiki kitalu cha miche ya kahawa kikiandaliwa na wananchi, walisimama na kuteremka kwenda kushiriki na wananchi kwa dakika kadhaa. Sidhani kama wanakijiji walifika shambani hapo na majembe ya ziada. Jambo hili ni common sense tu wala si la kuumiza kichwa yakhe.

Pili huu ulikuwa msafara wa viongozi wa serikali ambao unakuwa na vyombo kadhaa vya usalama, habari na wasindikizaji, si ajabu vyombo vya usalama vikawa tayari kuwalinda viongozi hawa wakati we unawaona kama wamesimama na kuangalia kwa vile hukuzungukia nyuma ya upeno wa nyumba kuangalia kuna nini.
 
Pengine wewe si mkulima au hujui kuangalia mapozi ya kupigia Picha. Chunguza vizuri picha ya kwanza utaona kuwa, wakulima halisi ni kama waliambiwa wawapishe wakupwa wapige picha. Kwa mkulima halisi anatambua pozi na mavazi ya shambani. Wapongeze wewe mimi siwezi kumpongeza muigizaji, anaetaka kujizolea umaarufu kwa staili kama hii! Chema chajiuza...Kibaya chajitangaza!
 
Unadhani hapo Ishengoma anang'oa magugu, hebu cheki jinsi anavyong'oa magugu utadhani anazoa kinyesi cha mbwa. Si bora angeacha tu?

moz-screenshot-2.png
 
Pengine wewe si mkulima au hujui kuangalia mapozi ya kupigia Picha. Chunguza vizuri picha ya kwanza utaona kuwa, wakulima halisi ni kama waliambiwa wawapishe wakupwa wapige picha. Kwa mkulima halisi anatambua pozi na mavazi ya shambani. Wapongeze wewe mimi siwezi kumpongeza muigizaji, anaetaka kujizolea umaarufu kwa staili kama hii! Chema chajiuza...Kibaya chajitangaza!

Kitu kimoja naweza kujifunza katika tukio hili ni kwamba, wamediriki kuondoka maofisini kwao tena kutoka Iringa mjini kwenda porini huko kando ya milima ya Livingstone kuteremkia Ziwa Nyasa. Kama ni kwa ajili ya kupiga picha tu wasingepoteza muda mwingi na kupangua gear kwenye matope wakati Iringa kuna mashamba na wakulima wengi tu ambao wangeweza kwenda kupinga picha hizo kwa gharama nafuu.

Nasema mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.
 
Siasa kama zilivyo biashara nyingine zinahitaji matangazo ili ziendelee kuonekana bado zipo. Sishangai hizo kampeni za hao waheshimiwa za kununua ufahamu wetu. Ni mambo ya kawaida kwenye biashara!!
 
Siasa kama zilivyo biashara nyingine zinahitaji matangazo ili ziendelee kuonekana bado zipo. Sishangai hizo kampeni za hao waheshimiwa za kununua ufahamu wetu. Ni mambo ya kawaida kwenye biashara!!

Lipi bora? Kuhongwa mapesa wakati wa kampeni na baada ya uchaguzi wanaingia mitini hatuwaoni tena mpaka kipindi cha uchaguzi wanarudi tena? Au hii ya wanaojitangaza kwa kuwa karibu na wananchi muda wote wa kipindi cha utumishi wao?
 
Kitu kimoja naweza kujifunza katika tukio hili ni kwamba, wamediriki kuondoka maofisini kwao tena kutoka Iringa mjini kwenda porini huko kando ya milima ya Livingstone kuteremkia Ziwa Nyasa. Kama ni kwa ajili ya kupiga picha tu wasingepoteza muda mwingi na kupangua gear kwenye matope wakati Iringa kuna mashamba na wakulima wengi tu ambao wangeweza kwenda kupinga picha hizo kwa gharama nafuu.

Nasema mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.

Wewe huna kitu cha kufanya au? Umeona lolote wanalofanya hao unaonadi, utadhani wamekulipa kwa kelele zako hizo. Kama unataka kuona mfano wa kiongozi bora anayeshirikiana vizuri ktk shughuli za kujenga nchi kama kilimo basi jaribu kurudi nyuma wakati wa ujenzi wa vijiji vya ujamaa. Cheki sehemu zote alizoshiriki Mwalimu mfano: kilimo, ujenzi. Halafu angalia alivyovalia ndio utajua hawa viongozi wetu wa sasa wanaigiza tu hawana lolote.

Na wewe kama umezaliwa mjini ambapo watu hawalimi basi kaa kimya. Hujui kutofautisha mtu anayelima au aliyesimama au mtu anayelima na mtu anayeigiza.
 
Deo una kazi sana ndugu yangu, hii nunua nunua utaendelea nayo mpaka lini?Na mipango yako yoote ya kimafia tunainote. wee endeleea tu.Candid scope ni mwanajamvi wa muda mrefu sana hapa jamvini sikutegemea kama angelizwa na deo. Muulize mwenzako Franscis Godwin mpiga picha wa matukio iringa jinsi anavyotumikishwa.
 
Pengine wewe si mkulima au hujui kuangalia mapozi ya kupigia Picha. Chunguza vizuri picha ya kwanza utaona kuwa, wakulima halisi ni kama waliambiwa wawapishe wakupwa wapige picha. Kwa mkulima halisi anatambua pozi na mavazi ya shambani. Wapongeze wewe mimi siwezi kumpongeza muigizaji, anaetaka kujizolea umaarufu kwa staili kama hii! Chema chajiuza...Kibaya chajitangaza!

umenena vema
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom