Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,278
- 25,846
Kwanza nikiri kuwa Serikali ina mkono mrefu wa kutafuta na kupata taarifa au mtu fulani. Nikiri pia kuwa kuna kauli au vitendo vya viongozi wa Serikali vina kinga ya kutoshtakiwa. Mfano wa haraka na hai ni wa vitendo vya Rais. Kikatiba, Rais hawezi kushtakiwa kwa vitendo alivyovifanya akiwa madarakani.
Lakini, kauli au vitendo vya viongozi wa kiserikali vyaweza kuhojiwa kwa njia ya mashtaka mahakamani. Kauli aliyoitoa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kuhusu kuwataja askari na wananchi wanaoshirikiana na wauza madawa ya kulevya jijini Dar es Salaam si kauli nyepesi. Ni kauli nzito na inayopaswa kuambatana na ushahidi tosha.
Tayari waliotajwa wameshapata picha tofauti katika jamii inayowazunguka. Wameshapata madhara ya kisaikolojia, kifamilia na kijamii kwa ujumla. Mwaka 1991, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani wakati huo, Mhe. Augustine Lyatonga Mrema alimtuhumu kimaneno Hayati Mchungaji Christopher Mtikila kwa kupanga utekaji wake kwa kutumia wanajeshi wa kukodi.Ni katika shauri hili:REV. CHRISTOPHER MTIKILA v. THE EDITOR, BUSINESS TIMES & AUGUSTINE LYATONGA MREMA [1993] TLR 60
Mchungaji Mtikila alimburuza Mrema mahakamani kwa shauri la kudhalilishwa na kutwezwa (defamation) pamoja na Mhariri wa Gazeti lililochapisha habari hiyo. Upande wa Waziri Mrema uliwahi kuweka pingamizi la awali. Pingamizi lililenga kuweka kinga ya maneno au vitendo vya kiongozi wa kiserikali akiwa katika utumishi wake.
Jaji Kiongozi wa wakati huo (Jaji Samatta) alitupilia mbali pingamizi la Mrema kwa kusema,pamoja na mambo mengine, ifuatavyo: (i) No provision of the Government Proceedings Act 1967 or any other legislation takes away the common law right to sue a Government servant who commits a tort in the course of his official duties (ii) There is no law conferring immunity upon Ministers or public officials from being sued personally for torts they commit in the course of their official duties; when they are so sued in their personal capacity, it is not a suit against the Government;
Kimsingi, Mahakama Kuu ya Tanzania chini ya Jaji Kiongozi Samatta (kama alivyokuwa) ilitenganisha kauli na matendo ya Serikali pamoja na maneno na matendo ya Afisa wa Serikali. Ikaruhusu Afisa wa Serikali kushtakiwa mwenyewe na kuitenga Serikali katika maneno na matendo yake.
Nauliza, kama hakutakuwa na ushahidi wa kutosha kuhusu tuhuma nzito alizozitoa, Makonda amejiandaa kwa mashauri mahakamani juu ya aliyoyasema? Yasije yakamkuta ya Augustine Mrema ya mwaka 1991-1993 aliyeamini kauli ya Waziri ina kinga ya kisheria.