RC Makonda : Nani alikuwa anampigia simu uwanja wa ndege wa mwalimu Nyerere

kinondoniilala

JF-Expert Member
Feb 27, 2015
987
765
Habarini wana jamvi.

Jana tarehe 13 February, 2017 tulimsikia RC wa mkoa wa DSM, Bwana Makonda, akituhumu mmoja wa watoto wa viongozi wa awamu zilizopita, alikuwa anahusika kuwapigia simu wana usalama wa pale JNIA ili kurahisisha usafirishaji au uingizaji wa madawa ya kulevya nchini.

Na inasemekana katika list aliyokabidhi kwa Commissioner General wa Drugs Control and Enforcement Authority, jina la huyo muhusika yupo.

Wananchi wa mkoa wa Dar es salaam, tumechoka na kero za dawa za kulevya, tunamtaka RC MAKONDA amtaje hadharani ili tumjue na ikibidi afikishwe mahakamani kushitakiwa.

Nawasilisha.
 
Mbona bwa shemela kamtaja ama kumtaja yule sio kinyume cha sheria,mimi nadhani game imeanza kufigiswa.....ni mtizamo tu.
 
Back
Top Bottom