Wanabodi
Huu mtindo wa viongozi wetu wenye dhamana kutoa kauli za hovyo hovyo, kauli za udhalilishaji na za kimipasho mipasho zinazidi kushika kasi, japo najua wanamuiga nani kwa utoaji wa kauli hizi, hivi hawamuoni Makamo wa rais Mhe. Mama Samia Suhuhu Hassan, kwani yeye hana mdomo?. Ua hawamuoni Waziri Mkuu, Mhe. Kasim Majaliwa Majaliwa, kwani yeye hana mdomo?
Mbona viongozi hawa hawatumii lugha za kuudhi?. Mwalimu Nyerere aliwahi kuwashangaa viongozi wa taifa lete kwa kukuri kuwa kila awamu, ina mazuri yake na mabaya yake, akawashangaa viongozi badala ya kuiga mazuri, wao wanaiga mabaya!. Hivyo viongozi wetu pia wana mazuri yao na mabaya yao, hivyo nyie viongozi, msiige kile kitu cha viongozi wakuu wenu, igeni mazuri yao, mabaya yao waachieni. Nyie mnaiga tuu yote yakiwemo mabaya!. Miongoni mwa baadhi ya mabaya ya awamu hii, ni kauli za hovyo hovyo za baadhi ya viongozi ambazo badala ya kujenga umoja na mshikamano, zinachochea utengano na mifarakano.
Mimeisikia hii kauli ya hii ya RC Makonda
Kiukweli kauli hii sio kauli nzuri. RC Makonda, Makonda ni Mkuu wa Mkoa wetu wa Dar es Salaam. Jiji la Dar es Salaam ni metropolitan society, lina watu wa aina zote na vyama vyote dini zote, hali zote. Ni Jiji la wote. Makonda amemuita Mhe. Mbowe ni mwanasiasa uchwala aliyefilisika, amemuita Mhe. Zitto ni mganga wa kienyeji na mshirikina!. Hizo ni lugha za matukano, ni lugha za kuudhi.
Kwa wanaopenda makala fupi, tuishie hapa
kwa wale wakata issues tuendelee
Pascal mayalla,Ana unguli wa kinafiki.
Naamini anaendesha maisha kwa njia hiyo pia. Aliandika bandiko la kusifia muamala unasoma.
Leo hapa ana danganya kumkosoa makonda akiamini sisi ni watoto.
Sent using
Jamii Forums mobile app